Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 50

Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Utimilifu wa Ayubu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu Wakati wa Majaribio Yake)

Wakati Ayubu aliposikia kwamba mali yake ilikuwa imeibwa, kwamba watoto wake wa kike na kiume walikuwa wameaga dunia, na kwamba watumishi wake walikuwa wameuliwa, aliitikia hivi: “Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu” (Ayubu 1:20). Maneno haya yanatuambia ukweli mmoja: Baada ya kuzisikiza habari hizi, Ayubu hakushikwa na wasiwasi, hakulia, au kuwalaumu wale watumishi ambao walikuwa wamempa habari hizo, isitoshe hakukagua eneo la uhalifu ili kuchunguza na kuthibitisha ni kwa nini na ni vipi hali ilikuwa hivyo na kutaka kujua ni nini haswa kilichofanyika. Hakuonyesha maumivu au majuto yoyote kutokana na kupoteza mali yake wala hakuanza kupukutikwa na machozi kutokana na kuwapoteza watoto wake, wapendwa wake. Kinyume ni kwamba, akalirarua joho lake kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kuabudu. Vitendo vya Ayubu ni tofauti sana na vile vya binadamu wa kawaida. Vinawachanganya watu wengi, na kuwaruhusu kumkosoa Ayubu ndani ya mioyo yao kwa “kukosa huruma na rehema”. Kwa kupotea ghafla kwa mali yao, watu wa kawaida wangeonekana wamevunjwa moyo, au wanasikitika kweli—au kama ilivyo kwa baadhi ya watu, wanaweza hata kujipata wakiwa wamefadhaishwa moyo. Hii ni kwa sababu, katika mioyo yao, mali ya watu inawakilisha jitihada ya maisha yao yote, ndiyo ambayo maisha yao yanategemea, ndilo tumaini linalowafanya kuishi; kupoteza mali yao kunamaanisha jitihada zao zimeambulia patupu na kwamba hawana tumaini tena na kwamba pia hawana siku za usoni. Huu ndio mwelekeo wa mtu yeyote wa kawaida kuhusiana na mali yake na uhusiano wa karibu alio na mali hiyo, na huu ndio pia umuhimu wa mali katika macho ya watu. Hivyo, idadi kubwa ya watu wanahisi wakiwa wamechanganyikiwa na mwelekeo mtulivu wa Ayubu kuhusiana na kupoteza mali yake. Leo, tutauondoa mkanganyiko huo wa watu hawa wote kwa kuelezea kile kilichokuwa kikipitia moyoni mwa Ayubu.

Akili za kawaida zinakariri kwamba, kwa kuwa alikuwa amepewa rasilimali hizo nyingi na Mungu, Ayubu anafaa kuaibika mbele ya Mungu kwa sababu ya kuzipoteza rasilimali hizi, kwani alikuwa hajazitunza, alikuwa hajashikilia zile rasilimali alizopewa na Mungu. Hivyo, aliposikia kwamba mali yake ilikuwa imeibwa, mwitikio wake wa kwanza ulifaa kuwa kuenda kwenye eneo la uhalifu na kuchukua hesabu ya kila kitu kilichokuwa kimeenda na kisha kutubu kwa Mungu ili aweze kwa mara nyingine kupokea baraka za Mungu. Ayubu, hata hivyo hakufanya hivi—na kiasili alikuwa na sababu zake za kutofanya hivyo. Ndani ya Moyo wake, Ayubu alisadiki pakubwa kwamba kila kitu alichomiliki alikuwa amepewa na Mungu na hakikuwa kimetokana na jitihada zake yeye mwenyewe. Hivyo, hakuziona baraka hizo kama jambo la kutilia maanani, lakini alishikilia ile njia alifaa kuchukua kwa udi na uvumba kama kanuni zake za kuishi. Alizitunza baraka za Mungu, na akatoa shukrani kutokana nazo, lakini hakutamanishwa nazo wala hakutafuta baraka zaidi. Huo ndio uliokuwa mwelekeo wake kuhusu mali. Hakufanya chochote kwa minajili ya kupata baraka, wala kuwa na wasiwasi kuhusu au kuhuzunishwa kutokana na ukosefu au kupoteza baraka za Mungu; hakufurahi kwa njia ya kupindukia na isiyo na mipaka kwa sababu ya baraka za Mungu na wala hakupuuza njia ya Mungu wala kusahau neema ya Mungu kwa sababu ya zile baraka ambazo alifurahia mara kwa mara. Mtazamo wa Ayubu kwa mali yake unafichulia watu ubinadamu wake wa kweli: Kwanza, Ayubu hakuwa binadamu mlafi, na hakuwa na madai katika maisha yake yakinifu. Pili, Ayubu hakuwahi kuwa na wasiwasi au kuogopa kwamba Mungu angechukua kila kitu alichokuwa nacho, na ndio uliokuwa mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu ndani ya moyo wake; yaani, hakuwa na madai au malalamiko kuhusu ni lini au kama Mungu angechukua kutoka kwake, na wala hakuuliza sababu, lakini alilenga tu kutii mipango ya Mungu. Tatu, hakuwahi kusadiki kwamba rasilimali zake zilitokana na jitihada zake, lakini kwamba alipewa yeye na Mungu. Hii ilikuwa imani ya Ayubu kwa Mungu, na onyesho la imani yake. Je, ubinadamu wa Ayubu na ufuatiliaji wake wa kweli wa kila siku umefanywa kuwa wazi katika muhtasari huu wa hoja tatu kumhusu yeye? Ubinadamu na ufuatiliaji wa Ayubu ni vitu vilivyokuwa muhimu katika mwenendo wake mtulivu alipokabiliwa na hali ya kupoteza mali yake. Ilikuwa hasa kwa sababu ya ufuatiliaji wake wa kila siku ndipo Ayubu akawa na kimo na imani ya kusema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” kwenye majaribio ya Mungu. Maneno haya hayakupatwa kwa mkesha mmoja, na wala hayakujitokeza tu kwa ghafla kwenye kichwa chake Ayubu. Yalikuwa yale ambayo alikuwa ameona na kupata kwa miaka mingi ya kupitia safari ya maisha. Akilinganishwa na wale wote wanaotafuta tu baraka za Mungu na wanaoogopa Mungu atachukua kutoka kwao, nao wanachukia hali hio na wanalalamikia kuhusu hali hiyo, je utiifu wa Ayubu ni wa kweli haswa? Tukilinganisha na wale wote wanaosadiki kwamba Mungu yupo, lakini ambao hawajawahi kusadiki kwamba Mungu anatawala mambo yote, Ayubu anamiliki uaminifu na unyofu mkubwa?

Urazini wa Ayubu

Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye urazini zaidi alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake. Machaguo kama hayo ya kirazini yasingeweza kutenganishwa na shughuli zake za kila siku na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa amejua kwenye maisha yake ya siku baada ya siku. Uaminifu wa Ayubu ulimfanya kuweza kusadiki kwamba mkono wa Yehova Mungu unatawala mambo yote; imani yake ilimruhusu kujua ukweli wa ukuu wa Yehova Mungu juu ya vitu vyote; maarifa yake yalimfanya kuwa radhi na kuwa na uwezo wa kutii ukuu na mipangilio ya Yehova Mungu juu ya vitu vyote; utiifu wake ulimwezesha kuwa mkweli na mkweli zaidi katika kumcha kwake kwa Yehova Mungu; kumcha kwake kulimfanya kuwa halisi zaidi na zaidi katika kujiepusha kwake na maovu; hatimaye, Ayubu alikuwa mtimilifu kwa sababu alimcha Mungu na kujiepusha na maovu; na ukamilifu kwake kulimfanya kuwa na hekima zaidi na kukampa urazini wa kipekee.

Tunafaa kulielewa vipi neno hili “urazini”? Ufasiri wa moja kwa moja unamaanisha kwamba kuwa mwenye hisia nzuri, kuwa mwenye mantiki na wa kueleweka katika kufikiria kwako, kuwa na maneno ya kueleweka, vitendo na hukumu ya kueleweka, na kumiliki viwango visivyo na makosa na maadili ya mara kwa mara. Lakini urazini wa Ayubu hauelezwi sana kwa urahisi. Inaposemekana hapa kwamba Ayubu alimiliki urazini wa kipekee, inahusiana na ubinadamu wake na mwenendo wake mbele ya Mungu. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwaminifu, aliweza kuusadiki na kuutii ukuu wa Mungu, uliompa maarifa ambayo yasingeweza kupatikana na wengine na maarifa haya yalimfanya kuweza kutambua, kuhukumu, na kufafanua kwa usahihi zaidi yale yaliyompata, na yaliyomwezesha kuchagua ni nini cha kufanya na ni nini cha kushikilia kwa usahihi na wepesi zaidi wa kukata ushauri. Hivi ni kusema kwamba maneno, tabia, na kanuni zake ziliandamana na hatua zake, na msimbo ambao aliufanyia kazi, ulikuwa wa mara kwa mara, ulio wazi, na mahususi na haukukosa mwelekeo, wenye uamuzi wa haraka au wa kihisia. Alijua namna ya kushughulikia chochote kile kilichompata yeye, alijua namna ya kusawazisha na kushughulikia mahusiano kati ya matukio magumu, alijua namna ya kushikilia mambo kwa njia ambayo mambo hayo yalifaa kushikiliwa, na, vilevile, alijua namna ya kushughulikia ule utoaji na uchukuaji wa Yehova Mungu. Huu ndio uliokuwa urazini wenyewe wa Ayubu. Ilikuwa hasa kwa sababu Ayubu alijihami na urazini kama huu ndiposa akasema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake wa kiume na kike.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp