Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 75

Bwana Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano. Naye Yesu akaichukua ile mikate, na baada ya kutoa shukrani, akagawanya kwa wanafunzi, na wanafunzi wakawapa wale waliokuwa wameketi chini; na vivyo hivyo wale samaki kadiri kiasi walichotaka. Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mnitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.

Dhana ya “mikate mitano na samaki wawili” ni ya aina gani? Ni watu wangapi ambao mikate mitano na samaki wawili hulisha kwa kawaida? Mkipima kulingana na hamu ya kula ya mtu wa kawaida, inaweza kutosha tu watu wawili. Hii ndiyo dhana ya kimsingi kabisa ya mikate mitano na samaki wawili. Hata hivyo, imeandikwa katika dondoo hii kwamba mikate mitano na samaki wawili viliwalisha watu wangapi? Imerekodiwa katika Maandiko hivi: “Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano.” Tukilinganisha na mikate mitano na samaki wawili, elfu tano ni idadi kubwa? Ni nini maana ya idadi hii kuwa kubwa sana? Kutoka kwa mtazamo wa binadamu, kugawanya mikate mitano na samaki wawili kati ya watu elfu tano haitawezekana, kwa sababu tofauti kati ya idadi hizi ni kubwa mno. Hata kama kila mtu angepata tu kipande kidogo cha kutafuna, bado mikate hiyo isingetosha watu hao elfu tano. Lakini hapa Bwana Yesu alitenda muujiza—Hakuruhusu watu elfu tano kula hadi wakashiba tu, ila kulikuwa na vyakula vilivyobaki. Maandiko yanasema: “Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mnitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.” Muujiza huu uliwaruhusu watu kutambua utambulisho na hadhi ya Bwana Yesu, na uliwaruhusu pia kuona kwamba hakuna kisichowezekana kwa Mungu—waliuona ukweli wa kudura ya Mungu. Mikate mitano na samaki wawili viliweza kutosha kuwalisha watu elfu tano lakini kama kusingekuwa na chakula chochote, Mungu angeweza kuwalisha watu hao elfu tano? Bila shaka Angeweza! Huu ulikuwa muujiza, hivyo basi bila shaka watu walihisi hali hii kutoeleweka na wakahisi kwamba haikuaminika na iliwashangaza lakini kwa Mungu kufanya kitu kama hicho halikuwa kitu. Kwa sababu hili lilikuwa jambo la kawaida kwa Mungu, kwa nini litengwe ili liweze kufasiriwa? Kwa sababu kile kilichomo nyuma ya muujiza huu kimebeba mapenzi ya Bwana Yesu, ambayo hayajawahi kugunduliwa na wanadamu.

Kwanza, hebu tujaribu kuelewa watu hawa elfu tano walikuwa wa aina gani. Walikuwa wafuasi wa Bwana Yesu? Kutoka kwa Maandiko, tunajua kwamba hawakuwa wafuasi Wake. Walijua Bwana Yesu alikuwa nani? Bila shaka hawakujua! Kwa kiwango cha chini sana, hawakujua yule mtu aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Kristo, au pengine baadhi ya watu walijua tu jina Lake lilikuwa nani, na kujua kitu kumhusu Yeye au walikuwa wamesikia kitu kuhusu mambo aliyokuwa Amefanya. Walikuwa na mshawasha tu kuhusu Bwana Yesu kutoka katika hadithi, lakini bila shaka hamwezi kusema kwamba wao walimfuata Yeye, wala hata Kumwelewa. Bwana Yesu alipowaona watu hawa elfu tano, walikuwa na njaa na Angefikiria tu kuwalisha hadi washibe, na hivyo basi ilikuwa katika muktadha huu ndipo Bwana Yesu aliporidhisha matamanio yao. Baada ya kuyaridhisha matamanio yao, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Mwelekeo Wake kwa watu hawa waliotaka tu kula hadi kushiba ulikuwa upi? Wakati huu, fikira na mwelekeo Wake Bwana Yesu lazima ungehusu tabia ya Mungu na hali Yake halisi. Kuwa mbele ya watu hawa elfu tano waliokuwa na njaa na ambao walitaka tu kula chakula hadi kushiba, kuwa mbele ya watu hawa waliojaa mshawasha na matumaini kumhusu, Bwana Yesu alifikiria tu kutumia muujiza huu ili kuwatolea neema. Hata hivyo, Hakujipa tumaini sana kwamba watakuwa wafuasi Wake, kwani Alijua walitaka kujiunga na furaha hiyo na kuweza kula hadi kushiba, hivyo basi Aliweza kutumia kwa njia bora zaidi kile Alichokuwa nacho hapo, na Akatumia mikate mitano na samaki wawili kuwalisha watu elfu tano. Aliwafumbua macho watu hawa waliofurahia burudani hiyo, waliotaka kuiona miujiza, na wakaona kwa macho yao mambo yale ambayo Mungu mwenye mwili Angeweza kukamilisha. Ingawa Bwana Yesu alitumia kitu kinachoweza kushikika ili kuridhisha mshawasha wao, tayari Alijua katika moyo Wake kwamba watu hawa elfu tano walitaka tu kuwa na mlo mzuri, hivyo basi Hakusema chochote kamwe au kuwahubiria kamwe—Aliwaacha tu kuuona muujiza ukifanyika. Bila shaka Asingeweza kuwashughulikia watu hawa kwa njia sawa ambayo aliwashughulikia wanafunzi Wake ambao walimfuata Yeye kwa kweli, lakini katika moyo wa Mungu, viumbe vyote vilikuwa katika utawala Wake, na Angeviruhusu viumbe vyote katika macho Yake kufurahia neema ya Mungu kila ilipohitajika. Hata ingawa watu hawa hawakujua Yeye alikuwa nani au kumwelewa, au kuwa na picha yoyote fulani kumhusu au kutoa shukrani Kwake hata baada ya kula mikate na samaki, hili halikuwa jambo ambalo Mungu Alijali kuhusu—Aliwapa watu hawa fursa nzuri ya kufurahia neema ya Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu ana kanuni katika kile Anachofanya, na kwamba Hawaangalii wala kuwalinda wale wasioamini, na Yeye hasa hawaruhusu kufurahia neema Yake. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika? Machoni mwa Mungu, mradi tu viwe ni viumbe vyenye uhai ambavyo Yeye Mwenyewe aliviumba, Ataweza kuvisimamia na kuvitunza; Atavitunza, Atavipangia, na Atavitawala katika njia tofauti. Hizi ndizo fikira na mtazamo wa Mungu kwa mambo yote.

Ingawa watu hawa elfu tano walioila mikate hiyo na samaki hawakupanga kumfuata Bwana Yesu, Hakuwa mkali kwao; baada ya wao kula hadi kushiba, je, mwajua kile Alichofanya Bwana Yesu? Je, Aliwahubiria chochote? Alienda wapi baada ya haya? Maandiko hayarekodi kwamba Bwana Yesu alisema chochote kwao; Alipokamilisha kutenda muujiza Wake Aliondoka kimya kimya. Hivyo basi Aliwawekea mahitaji yoyote watu hawa? Kulikuwa na chuki yoyote? Hakukuwepo na chochote kati ya hizi—Yeye hakutaka tu kutilia maanani akili yoyote kwa watu hawa ambao wasingeweza kumfuata, na kwa wakati huu moyo Wake ulikuwa katika maumivu. Kwa sababu alikuwa Ameuona upungufu wa wanadamu na Alikuwa amehisi namna ambavyo wanadamu walivyomkataa, na Alipowaona watu hawa au Alipokuwa na wao, upumbavu wa binadamu na kutojua kwao kulimfanya awe na huzuni sana na kukamwacha na maumivu katika moyo Wake, hivyo basi Alitaka tu kuwaacha watu hawa haraka iwezekanavyo. Bwana hakuwa na mahitaji yoyote kwao katika moyo Wake, Hakutaka kuwatilia maanani, Yeye hasa hakutaka kutumia nguvu Zake zozote kwao, na Alijua kwamba wasingeweza kumfuata—licha ya haya yote, mtazamo Wake kwao ulikuwa bado wazi kabisa. Alitaka tu kuwashughulikia kwa huruma, kuwarudishia neema—huu ndio uliokuwa mtazamo wa Mungu kwa kila kiumbe kilicho katika utawala Wake: kwa kila kiumbe, kishughulikie kwa huruma, watoshelezee mahitaji yao, wawaruzuku wao. Kwa sababu hasa ambayo Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, Aliweza kwa hali ya kimaumbile sana kufichua kiini cha Mungu binafsi na kuwashughulikia watu hawa kwa huruma. Aliwatendea kwa ukarimu na moyo wa rehema na uvumilivu. Haijalishi ni vipi watu hawa walimwona Bwana Yesu, na haikujalisha ni aina gani ya matokeo ambayo yangekuwepo, Alikitendea tu kila kiumbe kutokana na nafasi Yake kama Bwana wa uumbaji wote. Kile Alichofichua kilikuwa, bila kuachwa, tabia ya Mungu, na kile Alicho nacho na kile Alicho. Kwa hivyo Bwana Yesu alifanya kitu kimya kimya, kisha Akaondoka kimya kimya—hii ni sura gani ya tabia ya Mungu? Unaweza kusema kwamba hii ni rehema ya upendo wa Mungu? Unaweza kusema kwamba Mungu ni Mwenye kujitolea? Mtu wa kawaida anaweza kufanya hivi? Bila shaka hawezi! Katika kiini, wale watu elfu tano ambao Bwana Yesu aliwalisha kwa mikate mitano na samaki wawili walikuwa kina nani? Tunaweza kusema kwamba walikuwa watu waliolingana na Yeye? Unaweza kusema kwamba wote walikuwa wakatili kwa Mungu? Inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba hawakuwa kabisa wanaolingana na Bwana, na kiini chao halisi kilikuwa kikatili kabisa kwa Mungu. Lakini Mungu aliwashughulikia vipi? Alitumia mbinu ya kuutuliza ukatili wa watu kwa Mungu—mbinu hii inaitwa “huruma.” Yaani, ingawa Bwana Yesu aliwaona kama watendaji dhambi, machoni mwa Mungu walikuwa hata hivyo uumbaji Wake hivyo basi bado aliwashughulikia watendaji dhambi hawa kwa huruma. Huu ndio uvumilivu wa Mungu, na uvumilivu huu unaamuliwa na utambulisho na kiini cha Mungu binafsi. Hivyo basi, hili ni jambo ambalo hakuna mwanadamu aliyeumbwa na Mungu anaweza kufanya—Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya hivi.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp