Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 92

Baraka za Mungu

Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.

Mwa 18:18-19 Kuona kwamba Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye? Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Njia na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba

Wengi hupenda kutafuta, na kufaidi, baraka za Mungu, lakini si kila mmoja anayeweza kufaidi baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Na kwa hivyo ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Huwa zinatwambia nini? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, au kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa kusudio la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.

Mafungu manne ya maandiko yaliyotajwa hapo juu yote ni rekodi kuhusu baraka za Mungu kwa binadamu. Yanatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile yanatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa kwenye baraka hizi. Ile sauti na njia ya matamshi ya Mungu, mtazamo na mahali ambapo Alitamka, huturuhusu kushukuru kwamba Yule anayetoa baraka na mpokeaji wa baraka kama hizo ni wenye utambulisho, hadhi, na hali halisi tofauti kabisa. Sauti na njia ambayo matamshi haya yanatolewa, na mahali ambapo yalitamkwa, vinaonyesha upekee wao kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na adhama isiyovumilia shaka kutoka kwa binadamu yeyote.

Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6: “Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.” Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni dhana gani ya hali halisi ya mamlaka ya Mungu unayoona? Kutoka kwa usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi na maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe …,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda,” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati uliozoeleka. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwengine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatatokana na wao, na kuwa wafalme watatoka miongoni mwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, hawathubutu kusema “Mimi nitakufanya kuwa hivi na hivi, kufanya hivi na hivi,” kwani wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia ufanisi mkubwa. Ni utajiri upi mkubwa utakaokuwepo kama mmoja wao angekuwa mfalme mkuu! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu! Haya yote ni matamanio ya watu wote, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao ni zaidi ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima ya wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema mambo kama haya ni kwa vile Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kutambua ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazomwombea binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na ili Mungu aweze kumuumba mtu atakayezidi kwa uzao ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hatawahi kufanya kazi Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujifunga mafunda mbalimbali; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.

Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Unaweza kuhisi hali isiyokuwa ya kawaida ya Muumba? Unaweza kuhisi hali ya mamlaka ya juu ya Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au kwa kuwakilisha, ujasiri Wake katika ufanisi; hayo ni, badala yake, ithibati ya mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kunazo semi mbili ambazo unafaa kutilia maanani hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” kunayo dalili ya kutoeleweka kwenye maneno haya? Kunayo dalili yoyote ya wasiwasi? Kunayo dalili yoyote ya woga? Kwa sababu ya matamshi “ataweza kwa hakika” na “atakuwa” kwenye matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna yule angethubutu kubariki mwengine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Maneno ya Mungu yanapokuwa na uhakika zaidi, ndipo yanathibitisha kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba ufanisi wake ni lazima. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, uzima wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Licha ya kilichotendeka, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uzito wenyewe wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywa cha Mungu, na kunazo nguvu, adhama na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na hoja zimethibitisha kuwa ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo ya kupitisha wakati, lakini ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp