Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 111

Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Ukijipata unakabiliwa na hukumu na kuadibiwa na Mungu, je, utasema kwamba neno la Mungu limetiwa najisi? Je, utasema kwamba kunayo hadithi inayoelezea hasira kali ya Mungu, na kwamba hasira Yake kali imetiwa najisi? Je, utamchafulia Mungu jina, ukisema kwamba tabia Yake si ya haki kwa ujumla? Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na hakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na hali halisi, isiyohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Katika dhana za binadamu, ni upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu tu kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, ambavyo havijatiwa najisi na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa najisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa hasira kali ya binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba hasira kali ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya kikao hiki cha ushirika, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu aliye hapa hatakuwa tena na dhana potovu, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa hasira ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka pembeni kuelewa kokote kwa awali kulikofikiriwa vinginevyo kuhusiana na hasira ya Mungu, kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu binafsi zilizopotoka na mitazamo ya hali halisi ya hasira ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtatumia kuwaza kokote kwa binadamu au kufikiria kuhusu tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni hali halisi ya kweli ya Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuandikwa na binadamu. Tabia Yake ni tabia Yake ya haki na haina uhusiano au miunganisho yoyote na uumbaji wowote ule. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na hali halisi Yake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si kujua kifaa; si kuchunguza kitu, wala si kuelewa mtu. Kama utatumia dhana yako au mbinu yako ya kujua kifaa au kuelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na hali halisi ya kweli ya Mungu. Hutawahi kufanikiwa kama utategemea kufikiria kwako ili kuelewa hali halisi ya Mungu. Njia ya pekee ni hivi: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya hamu yako ya kutaka ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp