Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 127

Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba

Baada ya kuwa mfuasi wa Mungu kwa miaka mingi, je, kunayo tofauti kubwa katika maarifa yenu ya hatima na yale ya watu wa ulimwengu? Je, mmeelewa kwa kweli kule kuamuliwa kabla kwa Muumba, na unaweza kujua kwa kweli ukuu wa Muumba? Baadhi ya watu wanao ufahamu mkuu, wa kina wa kauli hii “hiyo ndiyo hatima,” ilhali hawasadiki hata kidogo katika ukuu wa Mungu, hawasadiki kwamba hatima ya binadamu hupangiliwa na kupangwa na Mungu, na hawako radhi kunyenyekea mbele ya ukuu wa Mungu. Watu kama hao ni kana kwamba wanaelea baharini, wanatoswatoswa na mawimbi, huku wakielea na kufuata mkondo wa maji, wasiwe na chaguo ila kusubiri kimyakimya na kuachia maisha yao hatima. Ilhali hawatambui hatima ya binadamu inategemea ukuu wa Mungu; hawawezi kujua ukuu wa Mungu wao binafsi, na hivyo basi kutimiza utambulisho wa mamlaka ya Mungu, kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu, kuacha kukinzana na hatima na kuishi katika utunzwaji, ulinzi na mwongozo wa Mungu. Kwa maneno mengine, kukubali hatima si jambo sawa na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba; kusadiki hatima hakumaanishi kwamba mtu akubali, atambue, na ajue ukuu wa Muumba; kusadiki katika hatima ni ule utambulisho wa hoja hii na suala hili la nje, ambalo ni tofauti na kujua namna Muumba Anavyotawala hatima ya binadamu, kuanzia katika kutambua kwamba Muumba ndiye chanzo cha kutawala juu ya hatima za mambo yote na hata zaidi kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Muumba kwa ajili ya hatima ya binadamu. Kama mtu anasadiki tu katika hatima—hata anahisi kwa kina kuihusu—lakini papo hapo hawezi kujua, kutambua, kunyenyekea, na kukubali ukuu wa Muumba kuhusu ile hatima ya binadamu basi maisha yake yatakuwa kwa kweli msiba mkuu, maisha yaliyopita kwa masikitiko, utupu; yeye atakuwa hawezi kutii utawala wa Muumba, kuwa binadamu aliyeumbwa katika hali ya kweli zaidi ya kauli hiyo, na kufurahia idhini ya Muumba. Mtu anayejua na kupitia kwa kweli ukuu wa Muumba anafaa kuwa katika hali amilifu, isiyo baridi au ya kutoweza kusaidika. Huku wakati uo huo akikubali kwamba mambo yote yanategemea hatima ya maisha, yeye anafaa kumiliki ufafanuzi sahihi wa maisha na hatima: kwamba kila maisha yanategemea ukuu wa Muumba. Wakati mtu anapoangalia nyuma kwenye barabara aliyotembelea, wakati mtu anapokusanya tena kila awamu ya safari ya maisha yake, mtu anaona kila hatua, haijalishi kama barabara ya mtu inakuwa mbaya au nzuri, Mungu alikuwa akiongoza njia ya mtu, akipanga kila kitu. Ilikuwa ni mipangilio ya umakinifu ya Mungu, upangiliaji Wake makinifu ulioongoza mtu, bila kujua, hadi kufikia leo. Ili kuweza kukubali ukuu wa Muumba, ili kupokea wokovu Wake—utajiri mwingi ulioje! Kama mtazamo wa mtu katika hatima ni wa baridi, inathibitisha kwamba yeye anakinzana na kila kitu ambacho Mungu amempangilia, kwamba yeye hana mtazamo wa kunyenyekea. Kama mtazamo wa mtu katika ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni amilifu, basi mtu anapotazama nyuma katika safari yake, wakati mtu anapong’amua kwa kweli ukuu wa Mungu, mtu huyo ataweza kutamani kwa dhati kunyenyekea kila kitu ambacho Mungu amepangilia, atakuwa na jitihada zaidi na ujasiri wa kumwacha Mungu kuunda hatima yake, ili kuacha kuasi dhidi ya Mungu. Kwani mtu anaona kwamba akikosa kuelewa hatima, wakati mtu haelewi ukuu wa Mungu, wakati mtu anapotutusa mbele kwa hiari yake, akichechemea na kupenyeza kwenye ukungu, safari inakuwa ngumu sana, ya kuvunja moyo. Kwa hivyo wakati watu wanapotambua ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu, wale walio werevu wanachagua kuijua na kuikubali, kuaga kwaheri siku zenye maumivu ambapo walijaribu kuwa na maisha mazuri kwa nguvu za mikono yao miwili, badala ya kuendelea kung’ang’ana dhidi ya hatima na kuzitafuta zile shabaha maarufu za maisha kwa njia yao wenyewe. Wakati mtu hana Mungu, wakati mtu hawezi kumwona Mungu, wakati hawezi kutambua waziwazi ukuu wa Mungu, kila siku inakosa maana, inakosa thamani, na kuwa yenye taabu. Popote pale mtu yupo, kazi yoyote ile anayofanya, mbinu za mtu za kuzumbua riziki na kutafuta shabaha zake huweza kumletea kitu kimoja ambacho ni kuvunjika moyo kusikoisha na mateso yasiyopona, kiasi cha kwamba mtu hawezi kuvumilia kuangalia nyuma. Ni pale tu mtu anapokubali ukuu wa Muumba, ananyenyekea katika mipangona mipangilio Yake, na kutafuta maisha ya kweli ya binadamu, ndipo mtu atakapokuwa huru kwa utaratibu dhidi ya kuvunjika moyo na kuteseka, kutupilia mbali utupu wote wa maisha.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp