Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 128

Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli

Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu, siku zote wanakabiliana na hatima hiyo kwa kuasi, kwa mtazamo wa kuasi, na siku zote wanataka kutupilia mbali mamlaka na ukuu wa Mungu, na mambo yale ambayo hatima imewahifadhia, wakitumai kwamba watabadilisha hali zao za sasa na kubadilisha hatima yao. Lakini hawawezi kufaulu; wanazuiliwa kwa kila sehemu ya mabadiliko katika maisha. Mvutano huu, unaoendelea ndani ya nafsi ya mtu, ni wa maumivu; maumivu haya hayasahauliki; na wakati wote huu mtu anapoteza maisha yake mwenyewe. Sababu ya maumivu haya ni nini? Je, ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu au kwa sababu ya mtu kuzaliwa bila bahati? Bila shaka kati ya sababu hizi hakuna iliyo kweli. Kimsingi, ni kwa sababu ya njia ambazo watu huchukua, njia ambazo watu huchagua kuishi katika maisha yao. Baadhi ya watu huenda wasitambue mambo haya. Lakini unapojua kwa kweli, unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi unahisi maumivu yako yakipungua kwa utaratibu, na uzima wako wote unaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa. Tukiamua kutokana na hali za wingi wa watu, ingawaje kwa kiwango cha kibinafsi hawataki kuendelea kuishi kama walivyokuwa wakiishi awali, ingawaje wanataka tulizo katika maumivu yao, kimsingi hawawezi kung’amua kwa kweli thamani na maana halisi ya ukuu wa Muumba ya hatima ya binadamu; hawawezi kutambua kwa kweli na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba, isitoshe kujua namna ya kutafuta na kukubali mipango na mipangilio ya Muumba. Kwa hivyo kama watu hawawezi kutambua hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote ya binadamu, kama hawawezi kunyenyekea kwa kweli chini ya utawala wa Muumba, basi itakuwa vigumu sana kwao kutoendeshwa na kutiwa pingu za miguu na, fikira hii kwamba “hatima ya mtu imo kwenye mikono ya mtu,” itakuwa vigumu kwao kutupilia mbali maumivu ya kung’ang’ana kwao kwingi dhidi ya hatima na mamlaka ya Muumba, ni wazi kwamba hali hii pia itakuwa ngumu kwao katika kuweza kukombolewa kwa kweli na kuwa huru, kuwa watu wanaoabudu Mungu. Kunayo njia rahisi zaidi ile ya kujifanya kuwa huru kutoka katika hali hii: kuaga kwaheri njia yako ya awali ya kuishi, kuaga kwaheri shabaha zako za maisha za awali, kuhitimisha na kuchambua hali ya maisha ya awali, filosofia, mambo uliyofuatilia, matamanio, na maadili, na kisha kuyalinganisha yote haya na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya binadamu, na kuona kama yoyote kati ya haya yanakubaliana na mapenzi na mahitaji ya Mungu, kujua kama yoyote kati ya haya yanakuletea maadili sahihi ya maisha, yanakuongoza katika ufahamu mwingi zaidi wa ukweli, na kuruhusu mtu kuishi kwa ubinadamu na mfano wa binadamu. Unapochunguza mara kwa mara na kuchambua kwa makini shabaha mbalimbali za maisha ambazo watu hufuatilia na njia zao tofauti za kuishi, utapata kwamba hata hakuna moja kati ya hizo zote ambayo inaingiliana na nia ya Muumba wakati Alipoumba binadamu. Zote hizi zinawavuta watu mbali na ukuu na utunzwaji wa Muumba; zote ni mitego ambayo binadamu hujipata amenaswa nayo, na ambayo inawaelekeza jehanamu. Baada ya kutambua haya, kazi yako ni kuweka pembeni mtazamo wako wa maisha ya awali, kuwa mbali na mitego mbalimbali, kumwachia Mungu kuchukua usukani wa maisha yako na kukufanyia mipangilio, jaribu tu kunyenyekea katika mipango na mwongozo wa Mungu, kutokuwa na chaguo, na kuwa mtu anayemwabudu Mungu. Haya yote yanaonekana kuwa rahisi, lakini ni jambo gumu kufanya. Baadhi ya watu wanaweza kuvumilia maumivu yake, wengine hawawezi. Baadhi wako radhi kutii, wengine hawako radhi. Wale wasiokuwa radhi wanakosa tamanio na uamuzi wa kufanya hivyo; wanayo habari kamili kuhusu ukuu wa Mungu, wanajua vyema kabisa kwamba ni Mungu anayepangilia na kupanga hatima ya binadamu, na ilhali wangali wanang’ang’ana tu, bado hawajaridhiana na nafsi zao kuhusiana na kuziacha hatima zao kwenye kiganja cha mkono wa Mungu na kunyenyekea katika ukuu wa Mungu, na zaidi, wanachukia mipango na mipangilio ya Mungu. Kwa hivyo, siku zote kutakuwa na baadhi ya watu wanaotaka kujionea wenyewe kile wanachoweza kufanya; wanataka kubadilisha hatima zao wenyewe kwa mikono yao miwili, au kutimiza furaha kwa kutumia nguvu zao wenyewe, kuona kama wanaweza kukiuka mipaka ya mamlaka ya Mungu na kuinuka juu ya ukuu wa Mungu. Huzuni ya binadamu, si kwamba binadamu anatafuta maisha mazuri, si kwamba anatafuta umaarufu na utajiri au anang’ang’ana dhidi ya hatima yake mwenyewe kupitia kwenye ukungu, lakini kwamba baada ya yeye kuona uwepo wa Muumba, baada ya yeye kujifunza hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, bado hawezi kurekebisha njia zake, hawezi kuvuta miguu yake kutoka kwenye mtego, lakini anaufanya moyo wake kuwa mgumu na anasisitizia makosa yake. Afadhali aendelee kutapatapa kwenye matope, akiapa kwa ukaidi dhidi ya ukuu wa Muumba, akiupinga mpaka mwisho wake mchungu, bila ya hata chembechembe kidogo ya majuto, na mpaka pale anapolazwa akiwa amevunjika na anavuja damu ndipo anapoamua hatimaye kusalimu amri na kugeuka na kubadilisha mwenendo. Kwa kweli huu ni huzuni kwa binadamu. Kwa hivyo Ninasema, wale wanaochagua kunyenyekea ni werevu na wale waliochagua kutoroka ni vichwa vigumu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp