Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 150

Jinsi Ambavyo Shetani Hutumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu

Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua kuhusu vitu kama ubashiri, kusoma uso, na uaguzi ni ili waweza kujua bahati zao zitakuwa vipi katika siku za baadaye na vile njia iliyo mbele inakaa, lakini mwishowe, ni mikono ya nani inadhibiti vitu hivi? (Mikono ya Mungu.) Viko katika mikono ya Mungu. Kwa kutumia mbinu hizi, Shetani anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu wanamwekea imani isiyoweza kutambua na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Nimependezwa sana na huyu mwaguzi, yuko sahihi sana! Sijawahi kumwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu?” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya?” Na kisha atasema hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…. Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema. Si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Unapofanya kile anachosema na maneno yake sasa yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, hungetaka kurudi nyuma kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anasema? Utaletwa chini ya bawa lake haraka sana, kupotoshwa, na kuwekwa chini ya udhibiti wake. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta. Hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu wa maumbile kumwamini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini Shetani wakati wowote hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, watu kweli wanaanguka katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Mbona tungesema hivyo? Hila za Shetani ni za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyikiwa kwao, watu wanasujudu mbele yake. Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kwamba kuna watatu katika familia yako, akiwemo binti ambaye ana miaka 7, na pia umri wa wazazi wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? Na kisha Shetani anaweza kusema, “Kazi imekuwa ngumu kwako leo, wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako.” Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo hayajakuwa yakienda vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi. Kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kusudi na unashawishiwa naye. Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka na hivyo ndivyo unaanza kufuata njia hiyo bila kusudi. Punde unapoanza kufuata njia hiyo, haitakuwa chochote ila shida kwako; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, udanganyifu, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, ni wachanga na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kusudi, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp