Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 200

Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake

Kwa kweli, Mungu hana mahitaji sana kwa wanadamu—au angalau, hana mahitaji kama watu wanavyodhani. Bila matamshi ya Mungu, au udhihirishaji wowote wa tabia Yake, matendo, au maneno, basi kumjua Mungu kungekuwa kugumu sana kwenu, kwa sababu watu wangelazimika kukisia nia ya Mungu na mapenzi Yake, kitu ambacho ni kigumu sana kwao. Lakini kutokana na hatua ya mwisho ya Kazi Yake, Mungu amenena maneno mengi, kufanya kiwango kikubwa cha kazi, na kufanya mahitaji mengi kwa wanadamu. Katika maneno Yake, na kiwango kikubwa cha kazi Yake, amejulisha watu anachokipenda, anachokichukia, na wanafaa kuwa aina gani ya watu. Baada ya kuelewa vitu hivi, ndani ya nyoyo watu wanafaa kuwa na maelezo sahihi ya mahitaji ya Mungu, kwa kuwa hawamwabudu tena yule Mungu asiye yakini, au kumfuata Mungu katika ukosefu uyakini na udhahania na utupu; badala yake, watu wanaweza kusikia maneno ya Mungu, wanaweza kuelewa viwango vya mahitaji ya Mungu, na kuvifikia, na Mungu hutumia lugha ya wanadamu kuwaambia watu yale yote wanafaa kujua na kulewa. Leo, kama watu hawafahamu mahitaji ya Mungu kwao, kile Mungu alicho, kwa nini wanamwamini Mungu, na jinsi wanafaa kumwamini Mungu na jinsi wanavyojichukulia mbele Zake, basi kuna shida hapa. … Mahitaji sahihi ya Mungu kwa wanadamu na wale ambao wanamfuata ni kama ifuatavyo. Mungu anahitaji mambo matano kutoka kwa wale wanaomfuata; imani ya kweli, ufuasi wenye uaminifu, utiifu kamili, ufahamu wa kweli na heshima za kutoka moyoni.

Katika mambo haya matano, Mungu anahitaji kuwa watu wasimshuku tena, wala kumfuata wakitumia fikira zao au mitazamo ikosayo uyakini na iliyo dhahania; Ni lazima wamfuate Mungu bila fikira au dhana zozote. Mungu anahitaji kuwa wote wanaomfuata wafanye hivyo kwa uaminifu, sio kwa shingo upande au bila kujizatiti. Mungu anapokupa mahitaji yoyote, au kukujaribu, kukuhukumu, kukushughulikia na kukupogoa, au kukuadhibu na kukuangamiza, unapaswa kuwa mtiifu kabisa Kwake. Hufai kuuliza kilichosababisha, au kuweka masharti, au hata uongee kuhusu sababu. Utiifu wako lazima uwe usio na shaka. Kumjua Mungu ni kipengele ambacho watu wengi wanakosea. Mara kwa mara wanamlazimishia Mungu misemo, matamshi, na maneno ambayo hayahusiani na Yeye, wakiamini kuwa haya maneno ndiyo ya kweli kuhusu kumfahamu Mungu. Kumbe hawajui kuwa hii misemo, ambayo inatoka kwa fikira za watu, ung’amuzi wao, na busara zao, havina uhusiano wowote na kiini cha Mungu. Na kwa hiyo, Ninataka kukwambia kuwa, katika ufahamu wa watu unaotamaniwa na Mungu, Mungu haulizi tu kwamba umtambue Mungu na maneno Yake, lakini kuwa ufahamu wako juu ya Mungu ni sahihi. Hata kama unaweza kusema sentensi moja tu, au una ufahamu mdogo tu, huu ufahamu mdogo ni sahihi na wa kweli, na unalingana na kiini cha Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa Mungu hapendi sifa na wao kumtukuza Yeye kwa hali isiyo halisi na yenye nia mbaya. Zaidi ya hayo, Anachukia watu wanapomchukulia kama hewa. Anachukia ambapo, wakati wa majadiliano juu ya mada kuhusu Mungu, watu wanazungumza kimzaha, wakiongea kwa hiari bila ya kujali, wakiongea wapendavyo; zaidi ya hayo, anawachukia wale wanaojifanya wanamjua Mungu, na wanaringa kuhusu ufahamu wa Mungu, wakijadili mada kuhusu Mungu bila mipaka au kipimo. La mwisho Kati ya yale mahitaji matano lilikuwa ni kumheshimu Mungu kutoka moyoni. Hili ndilo hitaji kuu la Mungu kwa wale wote wanaomfuata. Wakati mtu ana ufahamu wa kweli na sahihi kumhusu Mungu, anaweza kumheshimu Mungu na kuepuka maovu. Heshima hii hutoka ndani ya moyo wake, ni ya hiari, na sio kwa sababu Mungu amemshurutisha. Mungu hataki utoe zawadi ya mwelekeo wowote wa kupendeza, au tabia, au mienendo ya nje Kwake; badala yake, anataka kwamba umheshimu na umwogope kutoka ndani ya moyo wako. Heshima hii inaafikiwa kutokana na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, kwa sababu una ufahamu juu ya Mungu, kwa sababu unaelewa matendo ya Mungu, kwa sababu ya uelewa wako wa kiini cha Mungu, na kwa sababu umetambua ukweli kuwa wewe ni mmoja wa viumbe wa Mungu. Na kwa hiyo, nia yangu ya kutumia neno “kutoka moyoni” kwa kurejelea heshima hapa ni kwamba wanadamu waelewe kuwa heshima ya watu kwa Mungu inapaswa kutoka ndani ya mioyo yao.

Sasa yafikirie hayo matakwa matano: kuna yeyote kati yenu anaweza kupata matatu ya kwanza? Ambapo Ninamaanisha uaminifu wa kweli, ufuasi wenye uaminifu, na utiifu kamili. Kuna wowote kati yenu wanaoweza mambo haya? Najua Nikisema yote matano, basi bila kuuliza hapatakuwa na hata mmoja kati yenu anayeweza—lakini nimeyapunguza hadi matatu. Tafakari kama umeyapata au la. Je, “uaminifu wa kweli” ni rahisi kuupata? (La, sio rahisi.) Sio rahisi, kwa kuwa mara nyingi watu humtilia Mungu mashaka. Na, je, “ufuasi wenye uaminifu”? Huu “uaminifu” una maana gani? (Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote.) Sio kwa shingo upande ila kwa moyo wote. Mmegonga ndipo! Kwa hiyo, je, mna uwezo wa kupata hili hitaji? Inabidi mjitahidi zaidi—siyo? Kwa sasa bado hamjapata hili hitaji. Kuhusu “utiifu kamili”—je, mmepata hilo? (Hapana.) Bado hamjapata hilo, pia. Mara nyingi nyinyi si watiifu na ni waasi, mara nyingi hamsikilizi, au kupenda kutii, au kutaka kusikia. Haya ndiyo mahitaji matatu ya msingi wanayopata watu baada ya kuingia katika maisha yao, na bado hamjayapata. Kwa hiyo, kwa wakati huu, mna uwezo mkubwa? Leo, baada ya kunisikia nikisema maneno haya, mna wasiwasi? (Ndiyo.) Ni sawa kuwa mna wasiwasi. Msiwe na wasiwasi Ninahisi wasiwasi kwa niaba yenu. Sitakwenda katika mahitaji hayo mengine mawili; bila shaka, hakuna anayeweza kuyafikia. Mna shauku. Kwa hivyo mmebaini malengo yenu? Malengo yapi, kuelekeza upande gani, mnapaswa kuyafuata, na kujitolea jitihada zenu? Mna lengo? Hebu niongee waziwazi: mnapofikia mahitaji haya matano, mtakuwa mmemridhisha Mungu. Kila mojawapo ni ishara, ishara ya watu wakiingia katika maisha wakiwa wamefikia ukomavu, na lengo la mwisho la hii. Hata kama Ningechukua moja kati ya mahitaji na kuongea kwa kina kulihusu na kinachohitajika, haiwezi kuwa rahisi kupata; ni lazima mpitie kiwango fulani cha matatizo na kufanya kiasi fulani cha juhudi. Na ni aina gani ya mawazo mnapaswa kuwa nayo? Yanapaswa kuwa sawa na yale ya mgonjwa wa saratani anayesubiri kwenda kwenye meza ya upasuaji. Na ni kwa nini Ninasema haya? Kama ungependa kumwamini Mungu, na kumpata Mungu na kupata ridhaa Yake, basi kama hutapitia katika kiasi fulani cha shida, au kufanya kiwango fulani cha juhudi, hutaweza kupata vitu hivi. Umesikia mahubiri mengi, lakini kuyasikia hakumaanishi kuwa haya mahubiri ni yako; ni lazima uyachukue na kuyageuza yawe kitu ambacho ni chako, ni lazima uyasimilishe maishani mwako, na kuyaleta katika uwepo wako, ukiyaruhusu maneno na mahubiri haya yakuongoze katika maisha yako, na kuleta dhamana na maana ya uhai katika maisha yako—na hivyo basi itakuwa ni thamani kuwa uliyasikia maneno haya. Kama maneno haya Ninayoyanena hayaleti mabadiliko yoyote katika maisha yenu, au thamani yoyote katika uwepo wako, basi hakuna haja ya kuyasikiliza. Mnaelewa haya, ndiyo? Baada ya kuelewa haya, basi kilichobaki ni juu yenu wenyewe. Ni lazima mfanye kazi! Ni lazima muwe na bidii katika kila jambo! Msiwe huku na kule—wakati unapita upesi! Wengi wenu wameamini kwa zaidi ya miaka kumi. Tazama nyuma kwa hii miaka zaidi ya kumi ya imani katika Mungu: Umenufaika kiasi gani? Na mmesalia na miongo mingapi ya haya maisha? Sio mirefu. Sahau kuhusu iwapo kazi ya Mungu inakusubiri, iwapo Amekuachia nafasi, iwapo Atafanya kazi ile ile tena; usizungumze kuhusu hili. Unaweza kurudisha nyuma miaka yako kumi iliyopita? Kwa kila siku inayopita, na kila hatua unayochukua, siku ambazo unazo hupunguzwa kwa siku moja. Muda haumsubiri mwanadamu yeyote! Utanufaika tu kutokana na imani kwa Mungu kama utaichukulia kama kitu kikubwa zaidi maishani mwako, muhimu zaidi kuliko chakula, mavazi, au kitu kingine chochote! Kama huwa unaamini tu unapokuwa na wakati, na huwezi kutoa umakini wako wote kwa imani yako, kama siku zote umetatizwa na vurugu, basi hutafaidi chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp