Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe | Dondoo 135

Ufahamu wa watu leo kuhusu Mungu wa vitendo bado unaegemea upande mmoja, na ufahamu wao kuhusu umuhimu wa kupata mwili ni mdogo sana. Kuhusu suala la mwili wa Mungu, kupitia kwa kazi na maneno Yake watu huona kuwa Roho wa Mungu ana mengi, kwamba ni tajiri. Lakini, hata hivyo, ushuhuda wa Mungu hatimaye hutoka kwa Roho wa Mungu: Anachokifanya Mungu katika Mwili, ni kanuni gani anatumia, anachokifanya katika ubinadamu, na anachokifanya katika uungu. Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya wanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya wanadamu katika miili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.

Kwa kiasi kikubwa, ni mtazamo upi watu wanapaswa kuwa nao kuhusu Mungu wa vitendo? Unajua nini kuhusu kupata mwili, kuhusu kuonekana kwa Neno katika mwili, kuhusu kuonekana kwa Mungu katika mwili, na matendo ya Mungu wa vitendo? Na nini inazungumzia zaidi leo? Kupata mwili, ujio wa Neno katika mwili, kuonekana kwa Mungu katika mwili—haya yote ni lazima yaeleweke. Kwa kuzingatia kimo chenu, na enzi, ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua, katika uzoefu wa maisha yenu, ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua, na ni lazima muwe na ufahamu ulio wazi. Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakichukuliwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo huwa amewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo huwa yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu. Ukipatwa na Mungu, hupati tu kazi ya Roho Mtakatifu; kidesturi, unaweza kuzidisha mahitaji ya Mungu wa utendaji. Kuwa tu na kazi ya Roho Mtakatifu hakumaanishi kuwa una uzima. Cha muhimu ni kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha mahitaji ya Mungu wa vitendo, ambayo inahusiana na kama unaweza kupatikana na Mungu. Haya mambo ndiyo muhimu zaidi katika kazi ya Mungu wa vitendo katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, Mungu analipata kundi la watu kwa kuonekana halisi na hakika katika mwili na kuwa wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, Akionekana na watu, hasa Akifanya kazi ya Roho katika mwili, na kwa kuwa kielelezo kwa watu wenye miili. Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu

Kupitia neno la Mungu la utendaji, unyonge wa mwanadamu na uasi yanahukumiwa na kufichuliwa. Kisha wanadamu wanapokea wanachohitaji. Wanaona kuwa Mungu amekuja katika ulimwengu huu wa binadamu. Kazi ya Mungu wa utendaji ina nia ya kumwokoa kila mmoja kutoka kwa ushawishi wa Shetani, kuwaokoa kutoka kwa uchafu na kwa tabia yao iliyopotoshwa na Shetani. Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake kama mfano kamili wa mwanadamu. Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida, fuata maneno Yake na mahitaji, fuata kile Anachosema kabisa, na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu. Mungu alichukua mwili, Akiruhusu watu kuona matendo Yake. Roho Wake alichukua mwili, ili mwanadamu amguse Mungu, ili watu wamtazame Mungu na kuja kumjua. Kwa njia hii ya matendo pekee ndiyo Mungu huwafanya watu kuwa wakamilifu. Wale wanaoweza kuishi maisha yao kulingana na Yeye na kufuata moyo Wake, ni wale wanaopatwa na Mungu. Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake kama mfano kamili wa mwanadamu. Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida, fuata maneno Yake na mahitaji, fuata kile Anachosema kabisa, na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu. Kama Mungu angenena tu mbinguni na asije chini duniani, watu wangewezaje kumjua Yeye? Na maneno matupu tu kuonyesha kazi Yake, na sio maneno Yake kama ukweli. Mungu anakuja kama mfano, ili mwanadamu amwone na kumgusa, amwone na kupatwa na Yeye. Kupatwa na Mungu kunamaanisha kufuata mfano Wake kama mfano kamili wa mwanadamu. Mfuate Mungu wa matendo, ishi ubinadamu wa kawaida, fuata maneno Yake na mahitaji, fuata kile Anachosema kabisa, na ufanikishe kile Anachotaka, kisha utapatwa na Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana