Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 134

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, wakati ule ule, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu wa vitendo hufanya kazi miongoni mwa ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa jumla, Roho anatawala katika pande zote mbili. Hata iwe ni roho gani ndani ya watu, hivyo ndivyo huwa maonyesho yao ya nje. Roho anafanya kazi kawaida, lakini kuna pande mbili za uelekezaji Wake kwa Roho: Upande mmoja ni kazi Yake kwa ubinadamu, na upande mwingine ni kupitia uungu. Unafaa kujua haya wazi wazi. Kazi ya Roho hubadilika kulingana na matukio: Wakati kazi Yake ya binadamu inahitajika, Roho anaielekeza kazi hii ya binadamu, na wakati kazi ya uungu inahitajika, uungu hujitokeza moja kwa moja kuifanya. Kwa sababu Mungu hufanya kazi katika mwili na kujionyesha katika mwili, Anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kazi Yake katika ubinadamu inaongozwa na Roho, na ili kuyaridhisha mahitaji ya kimwili ya watu, kuwezesha ushirikiano wao Naye, kuwafanya waone uhalisi na ukawaida wa Mungu, na kuwafanya waone kuwa Roho amekuja katika Mwili, na Yuko miongoni mwa wanadamu, Anaishi pamoja na wanadamu, na Hushirikiana na wanadamu. Kazi Yake ya uungu ni kwa ajili ya kuwapa watu uzima, na kuwaelekeza watu katika kila kitu kwa upande mzuri, na kubadili tabia za watu na kuwafanya waone kwa kweli kuonekana kwa Roho katika mwili. Kwa kiwango kikubwa, ukuaji katika maisha ya mwanadamu unapatikana moja kwa moja kupitia kazi ya Mungu na maneno katika uungu. Ikiwa tu watu wataikubali kazi ya Mungu ya uungu wataweza kubadili tabia zao, hapo tu ndipo wataweza kushibishwa katika roho zao; ikiwa tu kuna ongezeko la kazi kwa ubinadamu katika mambo hayo—uchungaji wa Mungu, usaidizi, na riziki kwa ubinadamu—ndipo watu wataweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Mungu wa vitendo Mwenyewe ambaye Anazungumziwa leo hufanya Kazi katika uungu na ubinadamu. Kupitia kwa kujitokeza kwa Mungu wa vitendo, kazi Yake ya kawaida ya binadamu na maisha na kazi Yake kamilifu ya uungu vinapatikana. Ubinadamu na uungu wake vimeungwa kuwa kitu kimoja, na kazi ya pande zote mbili inakamilishwa kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Ananena maneno. Mungu anapofanya Kazi katika ubinadamu, Anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kushiriki na kuelewa. Maneno Yake yanasemwa waziwazi, na ni rahisi kueleweka, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila ya kujali kuwa hawa watu wana ufahamu au hawajasoma vyema, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu vilevile inaweza kufanywa kupitia maneno, lakini imejawa na riziki, imejawa na uzima, haijatiwa dosari na mawazo ya mwanadamu, haihusishi mapenzi ya mwanadamu, na haina mipaka ya binadamu, iko nje ya mipaka ya ubinadamu wowote wa kawaida; vilevile, inafanywa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Kama watu wanaikubali kazi ya Mungu katika ubinadamu tu, basi watajiwekea mipaka katika upeo fulani, na hivyo milele watahitaji kushughulikiwa, kupogolewa, na kufundishwa nidhamu ili kwamba pawepo na mabadiliko kidogo ndani yao. Bila ya Kazi au uwepo wa Roho Mtakatifu, ingawa, watairudia mienendo yao ya awali; ni kupitia kazi ya uungu tu ndio haya maradhi na upungufu vitaweza kurekebishwa, hapo ndipo watu wanafanywa kuwa wakamilifu. Badala ya kushughulikia na kupogoa mara kwa mara, kinachohitajika ni matokeo mazuri, kwa kutumia maneno kufidia upungufu wote, kutumia maneno ili kufichua hali zote za watu, kutumia maneno kuyaelekeza maisha yao, kila matamshi yao, kila tendo lao, ili kuziweka wazi nia na motisha yao; hii ni kazi halisi ya Mungu wa vitendo. Na kwa hivyo, katika mwelekeo wako kwa Mungu wa vitendo unafaa kunyenyekea mbele ya ubinadamu Wake, ukimkubali na kumtambua, na zaidi, unapaswa kukubali na kutii kazi ya uungu na maneno. Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu hasa wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.

Roho wa kazi ya Mungu katika ubinadamu ana awamu za mpito. Kwa kuwafanya ubinadamu wakamilifu, Anawawezesha ubinadamu Wake kupokea mwelekeo wa Roho, ambapo baadaye ubinadamu Wake unaweza kuyakimu na kuyaongoza makanisa. Hii ni aina moja ya maonyesho ya kazi ya kawaida ya Mungu. Hivyo, ukiweza kuona wazi kanuni za kazi ya Mungu katika ubinadamu, basi itakuwa vigumu kwako kuwa na dhana kuhusu kazi ya Mungu katika ubinadamu. Bila kujali kitu kingine chochote, Roho wa Mungu hawezi kukosea. Yuko sahihi, na Hana dosari; Hawezi kufanya kitu chochote kimakosa. Kazi ya uungu ni maonyesho ya moja kwa moja ya mapenzi ya Mungu, bila maingilio ya ubinadamu. Haipitii ukamilifu, ila inatoka moja kwa moja kwa Roho. Na bado, kufanya Kwake kazi katika uungu ni kwa sababu ya ubinadamu Wake wa kawaida; si miujiza, na kazi inaonekana kana kwamba imefanywa na mwanadamu wa kawaida; Kimsingi Mungu alitoka mbinguni kuja duniani ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili, kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa kutumia mwili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp