Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 405

Nimesema hapo awali kuwa “Wale wote wanaotafuta kuona ishara na maajabu watatelekezwa; wao sio wale wataofanywa wakamilifu.” Nimenena maneno mengi sana, ilhali hauna maarifa hata kidogo ya kazi hii, na kuwa umefika katika hatua hii, bado unaulizia ishara na maajabu. Je, kuamini kwako kwa Mungu ni harakati ya kuona ishara na maajabu, au ni kwa sababu ya kupata uzima? Yesu pia Alinena maneno mengi ambayo, leo, bado hayajatimika. Je unaweza kusema kuwa Yesu sio Mungu? Mungu alishuhudia kuwa Yeye ni Kristo na ni Mwana mpendwa wa Mungu. Je unaweza kukataa haya? Leo, Mungu anazungumza tu maneno, na iwapo huna uwezo wa kufahamu kabisa, basi huwezi kusimama kidete. Je unamwamini kwa sababu Yeye ni Mungu, au unamwamini kwa msingi kwamba maneno Yake yatatimika au la? Je unaamini katika ishara na maajabu, au unaamini katika Mungu? Leo, Haonyeshi ishara na maajabu—je Yeye kweli ni Mungu? Iwapo maneno Anayonena hayatimiki, je Yeye kweli ni Mungu? Je dutu ya Mungu inaamuliwa na iwapo maneno Anenayo yatatimika au hapana? Ni kwa nini watu wengine daima hungoja kutimika kwa maneno ya Mungu kabla ya kumwamini? Je hii si maana kwamba hawamjui? Wote walio na dhana za aina hii ni watu wanaomkana Mungu; wanatumia dhana kumpima Mungu; maneno ya Mungu yakitimika wanamwamini Mungu, na yasipotimika hawamwamini Mungu; na kila wakati wanatafuta ishara na maajabu. Je wao si Mafarisayo wa wakati wa sasa? Kama unaweza ama huwezi kusimama imara kunategemea iwapo unamjua ama humjui Mungu wa kweli—hili ni muhimu! Jinsi ulivyo ukuu wa uhalisi wa neno la Mungu ndani Yako, ndivyo ulivyo ukubwa wa maarifa yako kuhusu uhakika wa Mungu, na ndivyo utaweza kusimama kidete katika majaribu. Zaidi unavyotazamia ishara na maajabu, ndivyo utakavyokosa kusimama imara, na utaanguka katika majaribu. Ishara na maajabu sio msingi; uhakika wa Mungu tu ndio uzima. Watu wengine hawajui matokeo yanayotokana na kazi ya Mungu. Wanaishi katika mshangao kila siku, wakikosa kutafuta ufahamu wakazi ya Mungu. Harakati zao ni kumfanya Mungu atimize mapenzi yao, na ni baada tu ya haya ndio wawe makini katika imani yao. Wanasema kuwa watautafuta uzima iwapo maneno ya Mungu yatatimika, lakini iwapo maneno ya Mungu hayatatimika, basi hakuna uwezekano wa wao kuutafuta uzima. Mwanadamu anafikiri kuwa imani kwa Mungu ni kutafuta kuona ishara na maajabu na harakati ya kupanda mbinguni na mbingu ya tatu. Hakuna asemaye kuwa imani yake kwa Mungu ni harakati ya kuingia katika ukweli, kutafuta uzima, na kutafuta kupatwa na Mungu. Harakati ya aina hii ina thamani gani? Wale wasiofuata ufahamu wa Mungu na kuridhika kwa Mungu ni watu ambao hawamwamini Mungu, ni watu ambao hukufuru Mungu!

Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi. Leo, aina hiyo ya utendaji wa kidini lazima itakaswe; kufuata udhihirisho wa miujiza ya Mungu, kufuata uponyaji wa Mungu na kukemea Kwake mapepo, kufuata kupewa amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu, kufuata kupata mandhari na raha ya mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini, sio dhahiri na ni njia dhahania ya imani. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: ni imani katika Mungu ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—hicho ndicho kiasi cha chini zaidi unachopaswa kuwa nacho katika imani yako kwa Mungu. Imani kwa Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha katika mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu, kutoka maisha ya kiasili kwenda kwa maisha katika nafsi ya Mungu, ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii Mungu. Unapomjua tu Mungu ndipo unapoweza kupenda Mungu, na kupatikana kwa lengo hili ndilo lengo la pekee mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp