Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Hatima na Matokeo | Dondoo 599

Wanaopeleka watoto na jamaa zao wasioamini kabisa kanisani ni wachoyo sana na wanaonyesha ukarimu wao. Watu hawa wanasisitiza tu upendo, bila kujali iwapo wanaamini ama iwapo ni matakwa ya Mungu. Wengine wanaleta wake zao mbele ya Mungu, ama kuleta wazazi wao mbele ya Mungu, na bila kujali iwapo Roho Mtakatifu anakubali ama anafanya kazi Yake, kwa upofu “wanawachukua watu wenye vipaji” kwa ajili ya Mungu. Kuna faida gani inayoweza kupatikana kutokana na kueneza ukarimu huu kwa watu hawa wasioamini? Hata kama hawa wasioamini wasio na uwepo wa Roho Mtakatifu wanapambana kumfuata Mungu, bado hawawezi kuokolewa kama mtu anavyodhani wanaweza. Wanaopokea wokovu kwa kweli si rahisi hivyo kuwapata. Wale ambao hawajapitia kazi ya Roho Mtakatifu na majaribio na hawajakamilishwa na Mungu aliyepata mwili hawawezi kukamilika kabisa. Kwa hivyo, watu hawa hawana uwepo wa Roho Mtakatifu kutoka wakati wanaanza kumfuata Mungu kwa jina. Kulingana na hali yao halisi, hawawezi tu kufanywa kamili. Hivyo, Roho Mtakatifu Haamui kutumia nguvu nyingi kwao, wala Hawapatii nuru yoyote ama kuwaongoza kwa njia yoyote; Anawaruhusu tu kufuata na hatimaye kufichua matokeo yao—haya yametosha. Shauku na nia za mwanadamu zinatoka kwa Shetani, na hakuna vile zinaweza kukamilisha kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali mtu ni mtu wa aina gani, mtu lazima awe na kazi ya Roho Mtakatifu—je, mtu anaweza kumkamilisha mtu? Mbona mume anampenda mke wake? Na mbona mke anampenda mume wake? Mbona watoto ni watiifu kwa wazazi wao? Na mbona wazazi wanawapenda sana watoto wao? Watu kweli wana nia za aina gani? Je, si kuweza kukidhi mipango na tamaa zao za ubinafsi? Kweli ni ya mpango wa usimamizi wa Mungu? Ni ya kazi ya Mungu? Ni ya kutimiza wajibu wa kiumbe? Waliomwamini Mungu kwanza na hawangepata uwepo wa Roho Mtakatifu hawawezi kupata kazi ya Roho Mtakatifu; imeamuliwa kwamba watu hawa wataangamizwa. Bila kujali kiasi cha upendo ambao mtu anao kwao, hauwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Roho Mtakatifu. Shauku na upendo wa mwanadamu unawakilisha nia za mwanadamu, lakini haviwezi kuwakilisha nia za Mungu na haviwezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Hata mtu akieneza kiasi kikubwa zaidi cha upendo ama huruma kwa hao watu wanaomwamini Mungu kwa jina na kujifanya kumfuata Yeye lakini hawajui ni nini maana ya kumwamini Mungu, bado hawatapata huruma ya Mungu ama kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hata kama watu wanaomfuata Mungu kwa dhati ni wenye akili ndogo na hawawezi kuelewa kweli nyingi, bado wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu mara kwa mara, lakini wale walio wa akili nzuri kidogo, lakini hawaamini kwa dhati hawawezi kabisa kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Hakuna kabisa uwezekano wowote wa wokovu na watu hawa. Hata wakisoma na kusikiza ujumbe mara kwa mara ama kuimba sifa kwa Mungu, mwishowe hawataweza kubaki mpaka wakati wa pumziko. Iwapo mtu anatafuta kwa dhati hakuamuliwi na jinsi wengine wanamhukumu ama jinsi wengine karibu wanamwona, lakini kunaamuliwa na iwapo Roho Mtakatifu anamfanyia kazi na iwapo ana uwepo wa Roho Mtakatifu, na kunaamuliwa zaidi na iwapo tabia yake inabadilika na iwapo ana maarifa ya Mungu baada ya kupitia kazi ya Roho Mtakatifu kwa muda fulani; ikiwa Roho Mtakatifu anamfanyia mtu kazi, tabia ya mtu huyu itabadilika polepole, na mtazamo wake wa kumwamini Mungu utakua safi polepole. Bila kujali muda gani mtu anamfuata Mungu, kama wamebadilika, hii inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kwake. Kama hawajabadilika, inamaanisha kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwake. Hata kama hawa watu wanatoa huduma fulani, wanachochewa na nia zao za kupata bahati nzuri. Huduma ya mara kwa mara haiwezi kuchukua nafasi ya mabadiliko katika tabia yao. Hatimaye, bado wataangamizwa, kwani hakuna haja ya wale wanaotoa Huduma ndani ya ufalme, wala hakuna haja ya yeyote ambaye tabia yake haijabadilika kuwahudumia wale watu ambao wamekamilishwa na walio waaminifu kwa Mungu. Hayo maneno kutoka zamani, “Wakati mtu anamwamini Bwana, bahati inatabasamu kwa familia yake nzima,” yanafaa kwa Enzi ya Neema lakini hayana uhusiano na hatima ya mwanadamu. Yalifaa tu kwa hatua ya wakati wa Enzi ya Neema. Maana iliyokusudiwa ya maneno haya inaelekezwa kwa amani na baraka yakinifu ambazo watu wanafurahia; hayamaanishi kwamba familia nzima ya anayemwamini Bwana itaokolewa, wala hayamaanishi kwamba wakati mtu anapata bahati nzuri, familia yake nzima pia itaingia rahani. Iwapo mtu anapokea baraka ama kupata bahati mbaya inaamuliwa kulingana na kiini cha mtu, na haiamuliwi kulingana na asili ya kawaida ambayo mtu anashiriki na wengine. Ufalme hauna kabisa usemi kama huu ama kanuni kama hii. Kama mtu anaweza kusalimika hatimaye, ni kwa sababu amefikia mahitaji ya Mungu, na kama mtu hawezi hatimaye kubaki katika kipindi cha pumziko, ni kwa sababu mtu huyu hamtii Mungu na hajakidhi mahitaji ya Mungu. Kila mtu ana hatima inayofaa. Hatima hizi zinaamuliwa kulingana na asili ya kila mtu na hazihusiani kabisa. Mwenendo ovu wa mtoto hauwezi kuhamishwa kwa wazazi wake, na haki ya mtoto haiwezi kushirikishwa wazazi wake. Mwenendo ovu wa mzazi huwezi kuhamishwa kwa watoto wake, na haki ya mzazi haiwezi kushirikishwa watoto wake. Kila mtu anabeba dhambi zake husika, na kila mtu anafurahia bahati yake husika. Hakuna anayeweza kuchukua ya mwengine. Hii ni haki. Kwa mtazamo wa mwanadamu, iwapo wazazi wanapata bahati nzuri, watoto wao pia wanaweza, na watoto wakifanya maovu, wazazi wao lazima walipie dhambi zao. Huu ni mtazamo wa mwanadamu na njia ya mwanadamu ya kufanya vitu. Si mtazamo wa Mungu. Matokeo ya kila mtu yanaamuliwa kulingana na asili inayotoka kwa mwenendo wao, na daima yanaamuliwa inavyofaa. Hakuna awezaye kubeba dhambi za mwengine; hata zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kupokea adhabu badala ya mwengine. Hii ni thabiti. Malezi ya upendo ya mzazi kwa watoto wake hayamaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya watoto wake, wala upendo wenye utiifu wa mtoto kwa wazazi wake haumaanishi kwamba anaweza kufanya matendo ya haki badala ya wazazi wake. Hiyo ndiyo maana ya kweli ya maneno haya, “Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga katika kisiagi; mmoja atachukuliwa, na mwingine kuachwa.” Hakuna anayeweza kuwaingiza watoto wake watenda maovu rahani kwa msingi wa upendo wao wa kina kwa watoto wao, wala hakuna anayeweza kumwingiza mke wake (ama mume) rahani kwa sababu ya mwenendo wao wa haki. Hii ni kanuni ya utawala; hakuwezi kuwa na ubaguzi kwa mtu yeyote. Wanaotenda haki ni wanaotenda haki, na watenda maovu ni watenda maovu. Watenda haki watasalimika, na watenda maovu wataangamizwa. Watakatifu ni watakatifu; wao si wachafu. Wachafu ni wachafu, na hawana sehemu yoyote takatifu. Watu wote waovu wataangamizwa, na watu wote wa haki watasalimika, hata kama watoto wa watenda maovu wanafanya matendo ya haki, na hata kama wazazi wa mtu wa haki wanafanya matendo ya haki. Hakuna uhusiano kati ya mume anayeamini na mke asiyeamini, na hakuna uhusiano kati ya watoto wanaoamini na wazazi wasioamini. Ni aina mbili zisizolingana. Kabla ya kuingia rahani, mtu ana jamaa wa kimwili, lakini baada ya mtu kuingia rahani, mtu hana jamaa wa kimwili tena wa kuzungumzia. Wanaofanya wajibu wao na wasiofanya ni adui, wanaompenda Mungu na wanaomchukia Mungu ni wapinzani. Wanaoingia rahani na wale ambao wameangamizwa ni aina mbili ya viumbe wasiolingana. Viumbe wanaotimiza wajibu wao watasalimika, na viumbe wasiotimiza wajibu wao wataangamizwa; zaidi ya hayo, hii itadumu milele. Je, unampenda mume wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, unampenda mke wako ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Je, wewe ni mtiifu kwa wazazi wako wasioamini ili kutimiza wajibu wako kama kiumbe? Mtazamo wa mwanadamu wa kumwamini Mungu ni sahihi ama la? Mbona unamwamini Mungu? Unataka kupata nini? Unampenda Mungu jinsi gani? Wasioweza kutimiza wajibu wao kama viumbe na hawawezi kufanya juhudi nzima wataangamizwa. Watu leo wana mahusiano ya kimwili miongoni mwao, na pia ushirikiano wa damu, lakini baadaye hii yote itavunjwa. Waumini na wasioamini hawalingani ila wanapingana. Walio rahani wanaamini kwamba kuna Mungu na wanamtii Mungu. Wasiomtii Mungu wote watakuwa wameangamizwa. Familia hazitakuwa tena duniani; kunawezaje kuwa na wazazi na watoto ama mahusiano kati ya waume na wake? Kutoambatana kati ya imani na kutoamini kutakuwa kumevunja haya mahusiano ya kimwili!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp