Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 318

Imani yako kwa Mungu, utafutiliaji wako wa ukweli, na vile unavyofanya mambo yote yanapaswa kujikita katika ukweli: Kila kitu unachokifanya kinapaswa kiwe kinatekelezeka, na hupaswi kutafuta vitu vile ambavyo ni vya kinjozi tu. Hakuna maana yoyote katika kufanya vitu namna hii, na, adiha, maisha kama hayo hayana maana. Kwa sababu njia yako na maisha havijengwi katika kitu chochote kile isipokuwa uongo na ulaghai, na hufuati vitu ambavyo vina thamani na maana, kitu pekee unachopata ni fikra za kipuuzi tu na mafundisho ambayo hayana ukweli. Vitu kama hivyo havina uhusiano na maana na thamani ya uwepo wako, na vinaweza visikupeleke mahali popote. Kwa namna hii, maisha yako yote yatakuwa hayana maana au thamani—na kama huishi maisha yenye maana, basi unaweza kuishi mamia ya miaka na yote hiyo inaweza kuwa haina maana yoyote. Hayo yanawezaje kuitwa maisha ya mwanadamu? Haya si ni maisha ya mnyama? Kwa namna hiyo hiyo, kama utajaribu kufuata njia ya imani kwa Mungu, na wala hujaribu kumfuata Mungu anayeweza kuonekana, na badala yake unamwabudu Mungu asiyeonekana na asiyeshikika, halafu si kufuatilia huko ni bure? Mwisho wake, ufuatiliaji wako kutakuwa ni anguko kubwa. Kutafuta kwa aina hiyo kuna manufaa gani kwako? Tatizo kubwa zaidi la mwanadamu ni kwamba anaweza kupenda tu vitu ambavyo hawezi kuviona au kuvigusa, vitu ambavyo ni vya siri kubwa na vya kushangaza, na kwamba haviwezi kufikiriwa na mwanadamu na haviwezi kufikiwa na mwanadamu. Kadiri vitu hivi vinavyokuwa si halisi, kadiri vinavyochambuliwa na mwanadamu, ambaye anavifuata bila kujali kitu chochote, na anajidanganya mwenyewe kwamba anaweza kuvipata. Kadiri vinavyokuwa si halisi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvichunguza na kuvichambua zaidi, hata kwenda mbali zaidi na kufanya mawazo yake ya kina kuyahusu. Kwa kinyume chake, jinsi vitu vinavyokuwa halisi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kuvipuuza; huviangalia kwa dharau, na hata huvitweza. Huu si mtazamo wako sahihi juu ya kazi halisi Ninayoifanya leo? Kadiri mambo hayo yanavyokuwa halisi, ndivyo unavyozidi kuyadharau. Wala hutengi muda kwa ajili ya kuyachunguza, bali unayapuuzia; unayadharau mambo haya halisia, yenye matakwa ya moja kwa moja, na hata unakuwa na dhana nyingi kuhusu Mungu huyu ambaye ni halisi sana, na huwezi kuukubali uhalisi Wake na ukawaida wake. Kwa njia hii, huamini katika hali isiyo dhahiri? Una imani thabiti juu ya Mungu asiye dhahiri wa wakati uliopita, na wala hupendi kumjua Mungu wa kweli wa leo. Hii si kwa sababu Mungu wa jana na Mungu wa leo wanatoka katika enzi tofauti? Si pia kwa sababu Mungu wa jana ni Mungu wa mbinguni aliyeinuliwa, wakati Mungu wa leo ni mwandamu mdogo wa duniani? Aidha, si pia kwa sababu Mungu anayeabudiwa na mwanadamu ni yule aliyetokana na dhana zake, wakati Mungu wa leo ni mwili halisi aliyetokana na dunia? Yote yanaposemwa na kufanyika, si kwa sababu Mungu wa leo ni halisi sana kiasi kwamba mwanadamu hamfuati? Maana kile ambacho Mungu wa leo anamtaka mwanadamu afanye ni kile ambacho mwanadamu hayupo radhi kabisa kukifanya, na ambacho kinamfanya ajisikie aibu. Hii haifanyi mambo kuwa magumu kwa mwanadamu? Je, hii haionyeshi makovu yake hapa? Kwa namna hii, wengi wao ambao hawafuati uhalisia wanakuwa maadui wa Mungu katika mwili, wanakuwa wapinga Kristo. Huu si ukweli dhahiri? Kipindi cha nyuma, wakati Mungu alikuwa hajawa mwili, inawezekana ulikuwa mtu wa dini, au msahilina. Baada ya Mungu kuwa mwili, wasahilina wengi kama hao waligeuka bila kujua na kuwa wapinga Kristo. Unajua ni nini kinachoendelea hapa? Katika imani yako kwa Mungu, hujikiti katika uhalisia au kuufuatilia ukweli, bali unafuata mafundisho ya uongo—je, si hiki ndicho chanzo wazi cha uadui wako na Mungu katika mwili? Mungu mwenye mwili anaitwa Kristo, hivyo sio kwamba wote ambao hawamwamini Mungu katika mwili ni wapinga Kristo? Je, yule unayemwamini na kumpenda ni huyu Mungu katika mwili kweli? Je, kweli ni huyu Mungu aliye hai ambaye ni wa halisia zaidi na ambaye ni wa kawaida kabisa? Malengo ya ufuatiliaji wako, zako ni yapi hasa? Ni ya mbinguni au duniani? Je, ni dhana au ni ukweli? Je, ni Mungu au ni kiumbe fulani asiyekuwa wa kawaida? Kwa kweli, ukweli ndiohalisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa “methali ya maisha.” Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa “ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.” Mwanadamu kufuatilia uwekaji wa ukweli katika matendo ni kufanya wajibu wake, yaani, ufuatiliaji wa kukidhi matakwa ya Mungu. Asili ya matakwa haya ni ukweli halisi, badala ya mafundisho yasiyokuwa na maana ambayo hayafikiwi na mwanadamu yeyote. Kama kutafuta kwako ni mafundisho tu na bila uhalisia wowote, huoni unaasi dhidi ya ukweli? Wewe si mtu anayeushambulia ukweli? Mtu wa namna hiyo anawezaje kutafuta kumpenda Mungu? Watu ambao hawana uhalisia ni wale ambao wanausaliti ukweli, na wote kwa asili ni waasi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp