Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 536

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu la ubinadamu, na hutuacha tukiwa tumejawa na huzuni na hofu. Yeye hufichua fikra zetu, hufichua mawazo yetu, na hufichua tabia zetu potovu. Kupitia kwa yale yote sisi husema na kuyatenda, na kila wazo na fikra zetu, asili na kiini zinafichuliwa kwa neno Lake, na kutuacha na fedheha, tukitetemeka kwa hofu. Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, na hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa hadharani kabisa, na hata zaidi kuhisi tumeshawishika vikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba hatuna thamani machoni Pake, na kuwa sisi ni Shetani aishiye. Matumaini yetu yanavunjika, na kamwe hatuthubutu kumpa madai yoyote yasiyo na msingi au kumjaribu, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Kwa muda, akili zetu hukosa msimamo, na hatujui tutakavyoendelea kwa njia iliyo mbele wala hatujui jinsi ambavyo tutaendelea katika imani zetu. Inaonekana kama imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na ya kuwa hatujawahi kukutana na kufahamiana na Bwana Yesu. Kila kitu machoni petu hutushangaza, na kutufanya tuhisi ni kama tumetupwa mbali. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna hasira ambayo haiwezi kufichika na pia kuna aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, hali kadhalika, sisi hujaribu kuendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, na kujieleza kwa dhati mbele Yake. Ingawa kuna wakati mwingine ambao hatuna kiburi wala unyenyekevu kwa kutazamwa kwa nje, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, ndani yetu tunavumilia bahari ya mateso inayopanda na kushuka. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, na kutuacha bila tamaa zetu kuu na kutokuwa tayari kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kubwa kati yetu na Yeye na hakuna aliye tayari hata kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tunateseka kwa kupata pingamizi kubwa hivi na udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo. Hukumu na kuadibu Kwake zimetuwezesha kwa kweli kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake makosa ya binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni watu wa hadhi ya chini na najisi sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu kama hiyo, na zimetufanya tutamani kuacha asili kama hiyo na kiini kama hicho haraka iwezekanavyo, na kutochukiwa tena Naye wala tusimchafue moyo. Hukumu na kuadibu kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na hatumo tayari tena kwenda kinyume na matayarisho na mipangilio Yake. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kutafuta uzima, na zimetuwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu…. Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, tumetoka kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti…. Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake zote!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp