Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 196
Mungu amekosa usingizi kwa siku nyingi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine. Kazi hii yote inatendeka kati yenu na kuonekana tu kwenu; hakuna yeyote asiyeamini anayefahamu haya, kwani muda haujafika. Wanadamu hao wako karibu kufanywa wakamilifu baada ya kuvumilia adibu, lakini wale walio nje hawajui lolote juu yake. Kazi hii imefichwa sana! Kwao, Mungu mwenye mwili ni siri, lakini kwa wale walio katika mkondo, Anaweza kuchukuliwa kuwa wazi. Ingawa kwa Mungu yote ni wazi, yote yanakuwa wazi na yote yanaachiliwa, haya tu ni ya ukweli kwa wale wanaomwamini, na hakuna kitu kinachofanywa kujulikana kwa wale wasioamini Kazi inayofanywa hapa imetengwa kwa ushurutisho ili kuwazuia wasijue. Wakipata kujua, kinachowangojea ni shutuma na mateso. Hawataamini. Kufanya kazi katika taifa la joka kuu jekundu, mahali palipo nyuma zaidi, sio kazi rahisi. Kama kazi hii ingewekwa wazi na kujulikana, basi ingekuwa vigumu kuendelea. Hatua hii ya kazi haiwezi kuendelea katika sehemu hii. Wangestahimili vipi kama kazi hii ingeendelezwa kwa uwazi? Hii haingeleta hata hatari kubwa zaidi? Kama kazi hii haingefichwa, na badala Yake kuendelea kama wakati wa Yesu Alivyowaponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa njia ya kustaajabisha, basi si ingekuwa tayari “imeshanyakuliwa” na ibilisi? Je, wangestahimili uwepo wa Mungu? Kama sasa ningeingia kwenye kumbi kuwahadhiria wanadamu, je, si ningekuwa nimeshapasuliwa katika vipande kitambo? Na ikiwa hivyo, kazi Yangu itawezaje kuendelea kufanyika? Sababu ambayo ishara na miujiza haitendeki wazi wazi ni kwa ajili ya kujificha. Kwa hivyo kazi Yangu haiwezi kuonekana, kujulikana wala kugunduliwa na wasioamini. Iwapo hatua hii ya Kazi ingefanyika kwa njia sawa na kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, haingekuwa thabiti sana. Kwa hivyo, kazi hii kufichwa namna hii ni ya manufaa kwenu na kwa kazi yote. Wakati kazi ya Mungu duniani inafika kikomo, kumaanisha, wakati kazi hii katika siri inakamilika, hatua hii ya kazi italipuka na kuwa wazi. Watu wote watajua kwamba kuna kundi la washindi ndani ya taifa la Uchina; kila mwanadamu atafahamu kuwa Mungu katika mwili yuko Uchina na kwamba kazi Yake imefika kikomo. Hapo tu ndipo kutampambazukia mwanadamu: Ni kwa nini taifa la Uchina halijaonyesha kudhoofika wala kuporomoka? Inaonekana kuwa Mungu anaendeleza kazi Yake binafsi katika taifa la China na amefanya kuwa kamilifu kundi la watu na kuwafanya washindi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (2)
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Mungu amekosa usingizi kwa siku nyingi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu...
Mungu Hutumia Maneno ili Kuumba Viumbe Vyote Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa...
Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani...
Mpango wa miaka elfu sita umegawawa katika hatua tatu za kazi. Hakuna hatua moja pekee itakayowakilisha kazi ya enzi hizo tatu ila inaweza...