Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 402

Mtu hawezi kuwa na haraka kutimiza ufanisi wakati anapotafuta uzima; ukuzi katika maisha haufanyiki tu kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni kawaida na ya matendo, na lazima ipitie mchakato unaohitajika. Ilimchukua Yesu aliyekuwa mwili mchakato wa miaka 33.5 ili kukamilisha kazi Yake ya kusulubishwa, bila kutaja maisha ya binadamu! Si kazi rahisi pia kumuumba binadamu wa kawaida anayemdhihirisha Mungu. Hali hasa iko hivi kwa watu wa taifa la joka kuu jekundu. Ni wa kundi la watu fukara na wanahitaji kipindi kirefu cha neno na kazi ya Mungu. Hivyo basi usiwe na haraka kuyaona matokeo. Lazima ushughulike katika kula na kunywa neno la Mungu, na kutia jitihada katika maneno ya Mungu. Baada ya kuyasoma maneno Yake, lazima uweze kuyatia katika matendo kwa uhalisia, na katika maneno ya Mungu, uweze kupata maarifa, maono, utambuzi, na hekima. Kupitia haya, utabadilika bila kutambua. Kama unaweza kuchukua kama kanuni zako kula na kunywa na neno la Mungu, kulisoma neno Lake, kulijua kwa undani, kulipitia, na kulitia katika matendo, basi utakua bila kutambua. Baadhi husema kwamba hawawezi kulitia neno la Mungu katika matendo hata baada ya kulisoma! Haraka yako ni ya nini? Unapofikia kimo fulani, utaweza kulitia katika matendo neno Lake. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusemaje kwamba hawezi kuwapa msaada au kuwaheshimu wazazi wake? Unafaa kujua sasa kimo chako ni kipi, tia katika matendo kile unachoweza, na usiwe kwamba wewe ndiwe unayekatiza usimamizi wa Mungu. Wewe kula na kunywa tu na maneno ya Mungu na tukisonga mbele, chukulia suala hilo kama kanuni yako. Usiwe na wasiwasi bado kuhusu kama Mungu anaweza kukufanya kuwa kamili. Usiingilie jambo hilo kwa sasa. Wewe kula na kunywa tu na maneno ya Mungu punde unapokutana nayo, na unahakikishiwa kwamba Mungu ataweza kukufanya kuwa kamili. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ukule na kunywa neno Lake. Usifanye hivyo bila mpango. Badala yake, tafuta maneno unayofaa kujua, yaani, yale yanayohusiana na maono. Mwelekeo mwingine ambao lazima utafute ni ule wa matendo halisi, yaani, mwelekeo ule unaohusu kile unachofaa kuingia kwacho. Mwelekeo mmoja ni kuhusu maarifa, na mwingine unahusiana na kuingia. Punde utakapopata mielekeo hii yote, yaani, utakapong’amua kile unachofaa kujua na kutenda, basi utajua namna ya kula na kunywa neno la Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp