Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 458

Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hiyo, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia Mungu kazi, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo, kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi ya Mungu, mwanadamu anakuwa na fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zenu katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, hivyo kuwawezesha kuingia kuzuri katika kazi yenu. Kama mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilicho ndani ya mwanadamu, hakuna uwezekano wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisia, maana Roho Mtakatifu huangazia kwa njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili ndani ya mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwake. Hata hivyo, katika uhalisia, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa asili, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia uzoefu ambapo mwanadamu anakabiliana na shida nyingi, kimo halisi cha mwanadamu kinadhihirika katika mazingira kama hayo. Ni wakati huo tu ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio kikubwa sana, na ubinafsi, kujitumainia nafsi, na tamaa za mwanadamu vyote vinaibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao wanatambua kwamba haukuwa uhalisia wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea mwangaza tu. Roho Mtakatifu anapompa nuru mwanadamu ili kuuelewa ukweli, mara nyingi huwa ni kwa namna ya wazi na dhahiri, bila muktadha. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu. … Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa hasa kujikita katika kuingia kwenu wakati huo huo, kuona hasa kazi ya Roho Mtakatifu ni gani na kuingia kwenu ni kupi, na vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa vizuri naye na kuiruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kutenda ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusianao wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku baada ya siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hiyo ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika ambapo kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mlipitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, na vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa heshima na ibada kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (2)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp