Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 509

Kadiri usafishaji wa Mungu ulivyo mkubwa, ndivyo mioyo ya watu inaweza kumpenda Mungu zaidi. Mateso ndani ya mioyo yao ni ya manufaa kwa maisha yao, wanaweza zaidi kuwa na amani mbele ya Mungu, uhusiano wao na Mungu ni wa karibu zaidi, na wanaweza kuona vizuri zaidi upendo wa juu kabisa wa Mungu na wokovu Wake wa juu kabisa. Petro alipitia usafishaji mamia ya mara, na Ayubu alipitia majaribio kadhaa. Ikiwa mngependa kufanywa kamili na Mungu, nyinyi pia sharti mpitie usafishaji mamia ya mara; ni ikiwa tu mtapitia mchakato huu, na mtegemee hatua hii, ndiyo mnaweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, na kufanywa kamili na Mungu. Usafishaji ndio njia bora zaidi ambayo Mungu hutumia kuwafanya watu kamili; usafishaji na majaribio makali pekee ndiyo yanaweza kusababisha kuonekana upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo ya watu. Bila taabu, watu hukosa upendo wa kweli kwa Mungu; ikiwa hawajaribiwi ndani, na hawapitii usafishaji kwa kweli, basi mioyo yao daima itakuwa ikielea kwa nje. Baada ya kusafishwa hadi kiwango fulani, utayaona mapungufu na matatizo yako mwenyewe, utaona kiasi ambacho unakosa na kwamba huwezi kuzishinda zile shida nyingi unazokabiliwa nazo, na utaona jinsi kutotii kwako kulivyo kukubwa. Ni katika majaribu pekee ndipo watu wataweza kujua kwa kweli hali zao halisi, na majaribu huwafanya watu waweze kufanywa kamili vyema.

Katika maisha yake, Petro alipitia usafishaji mamia ya mara na alipitia majaribu mengi ya uchungu. Usafishaji huu ukawa msingi wa upendo wake mkubwa kabisa kwa Mungu na ukawa uzoefu muhimu zaidi katika maisha yake yote. Kwamba aliweza kuwa na upendo mkubwa kabisa wa Mungu ilikuwa, kwa namna moja, kwa sababu ya uamuzi wake kumpenda Mungu; la muhimu zaidi, hata hivyo, ilikuwa kwa sababu ya usafishaji na mateso aliyopitia. Mateso haya yakawa mwongozo wake katika njia ya kumpenda Mungu, na yakawa jambo lililokumbukwa zaidi kwake. Ikiwa watu hawapitii uchungu wa usafishaji wanapompenda Mungu, basi upendo wao umejaa uchafu na mapendeleo yao wenyewe; upendo kama huu umejaa mawazo ya Shetani, na hauwezi hata kabisa kuridhisha mapenzi ya Mungu. Kuwa na azimio la kumpenda Mungu sio sawa na kumpenda Mungu kwa kweli. Hata ingawa yote wanayofikiria mioyoni mwao ni kwa ajili ya kumpenda Mungu, na kumridhisha Mungu, kana kwamba fikira zao hazina mawazo yoyote ya kibinadamu, kana kwamba zote ni kwa ajili ya Mungu, fikira zao zinapoletwa mbele ya Mungu, fikira kama hizi hazisifiwi wala kubarikiwa na Mungu. Hata wakati watu wameelewa kikamilifu ukweli wote—wakati wamekuja kuujua wote—hili haliwezi kusemwa kuwa ishara ya kumpenda Mungu, haiwezi kusemwa kwamba watu hawa hakika wanampenda Mungu. Licha ya kuelewa ukweli mwingi bila kupitia usafishaji, watu hawana uwezo wa kutia ukweli huu katika vitendo; ni wakati wa usafishaji tu ndipo watu wanaweza kuelewa maana halisi ya ukweli huu, hapo tu ndipo watu wanaweza kufahamu kwa kweli maana yao ya ndani. Wakati huo, wanapojaribu tena, wanaweza kutia ukweli katika vitendo kwa njia ya kufaa, na kulingana na mapenzi ya Mungu; wakati huo, mawazo yao ya kibinadamu yanapunguzwa, upotovu wao wa kibinadamu unapunguzwa, na hisia zao za kibinadamu zinapunguzwa; ni wakati huo tu ndipo utendaji wao ni onyesho la ukweli la upendo wa Mungu. Athari ya ukweli wa upendo wa Mungu haitimizwi kupitia ufahamu wa kusemwa au kuwa tayari kiakili, wala haiwezi kutimizwa kwa kueleweka tu. Inahitaji kwamba watu walipe gharama, na kwamba wapitie uchungu mwingi wakati wa usafishaji, na hapo tu ndipo upendo wao utakuwa safi, na wa kuupendeza moyo wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni kwa Kupitia Usafishaji tu Ndiyo Mwanadamu Anaweza Kuwa na Upendo wa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp