Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 529

Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu hapo mwanzo wakiwa watu watakatifu, ni kama kusema, katika bustani ya Edeni, walikuwa watakatifu, wasiokuwa na uchafu. Walikuwa watiifu kwa Yehova, na hawakujua chochote kuhusu kuasi Yehova. Hii ni kwa sababu hawakuwa na kusumbuliwa na ushawishi wa Shetani, hawakuwa na sumu ya Shetani, na walikuwa watu wasafi kati ya binadamu wote. Waliishi katika bustani ya Edeni, bila kutiwa najisi na uchafu wowote, bila kuingiliwa na mwili, na heshima kwa Yehova. Baadaye, walipojaribiwa na Shetani, wakawa na sumu ya nyoka, na tamaa ya kuasi Yehova, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hapo mwanzo, walikuwa watakatifu na wenye kuheshimu sana Yehova; hivyo tu ndivyo walikuwa binadamu. Baadaye, baada ya kujaribiwa na Shetani, wakala tunda la maarifa ya kujua mazuri na mabaya, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Waliendelea kupotoshwa na Shetani, na wakapoteza sura asili ya mwanadamu. Hapo mwanzo, mwanadamu alikuwa na pumzi ya Yehova, na hakuwa muasi hata kidogo, na hakuwa na uovu wowote katika moyo wake. Wakati huo, mwanadamu alikuwa binadamu wa kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu akawa mnyama: Fikra zake zikajawa na uovu na uchafu, bila mazuri ama utakatifu. Je, huyu si Shetani? Umepata kujua mengi kuhusu kazi ya Mungu, ilhali haujabadilika wala kutakaswa. Bado unaishi katika himaya ya Shetani, na bado hujajitoa na kunyenyekea kwa Mungu. Huyu ni mtu ambaye ameshindwa lakini hajafanywa mkamilifu. Na mbona inasemekana kuwa mtu kama huyu hajafanywa mkamilifu? Kwa sababu mtu huyu hafuati maisha ama maarifa ya kazi ya Mungu, na hutamani tu raha za kimwili na starehe ya muda mfupi. Na kwa hivyo hakuna mabadiliko katika tabia zao, na hawajapata sura asili ya mwanadamu ilivyoumbwa na Mungu. Watu hao ni maiti zinazotembea, ni waliokufa na hawana roho! Wale wasiofuata maarifa ya mambo katika Roho, wasiofuata utakatifu, na wasiofuata kuishi kulingana na maisha ya ukweli, wanaotosheka na kushindwa kwa upande wa kanusho, na hawawezi kuishi kulingana na kuonyesha ukweli, na kuwa watu watakatifu—ni watu ambao hawajaokolewa. Kwani, kama hana ukweli, mwanadamu hataweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu; wale watakaoweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu pekee ndio wale ambao wameokolewa. Ninalotaka Mimi ni watu kama Petro, watu wanaofuata kufanywa wakamilifu. Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili upatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwako, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa wanadamu wa halisi. Kama huwezi kuishi kulingana na ukweli, ama kuishi kulingana na aliyefanywa mkamilifu, basi inaweza kusemwa kuwa wewe si binadamu, ila wewe ni mfu anayetembea, mnyama, kwa sababu huna ukweli, ni kusema huna pumzi ya Yehova, na basi wewe ni mtu aliyekufa ambaye hana roho! Ingawa unaweza kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa, unachopata ni wokovu kidogo, na hujakuwa kiumbe chenye roho. Ingawa umepata adabu na hukumu, tabia yako haijafanywa upya ama kubadilishwa kama matokeo; umebaki tu ulivyokuwa, bado wewe ni wa Shetani, na wewe si mtu aliyetakaswa. Wale tu waliofanywa wakamilifu ndio wenye thamani, na watu tu kama hao ndio wamepata maisha ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp