Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi? | Dondoo 323

Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vyema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni? Ingawa watu wameshuhudia matukio ya kiajabu ya mbinguni wakati huu na wamepata kusikia kuhusu elimu kuu ambayo mwanadamu hajapata kuwa nayo awali, bado wako gizani kuhusu mambo mengi ya kawaida, na ambao ni ukweli ambao haujafikiriwa. Baadhi ya watu wanaweza kusema, “Tumemwamini Mungu kwa miaka mingi. Tutakosaje kujua kufahamu Mungu ni nini? Je, si hili linatudunisha?” Lakini ukweli ni kwamba, ingawa kila mtu ananifuata wakati huu, hakuna yeyote anao ufahamu kuhusu kazi hii yote ya sasa. Hawatilii maanani masuali ya kawaida na rahisi, kando na hili suali tata la “Mungu”. Mnapaswa kujua kwamba hayo maswali ambayo mnayachukulia kuwa ya kawaida na hamjayatambua ndiyo mnayopaswa kuyajua zaidi, kwa maana mnajua tu kuufuata umati, hamyatilii maanani wala kuyajali yale ambayo mnafaa kujihami nayo. Je, mnajua kwa uhakika ni kwa nini mnapaswa kuwa na imani kwa Mungu? Je, mnajua kwa uhakika Mungu ni nini? Je, mnajua kwa uhakika binadamu ni nini? Kama mwanadamu ambaye yuko na imani kwa Mungu, iwapo huelewi mambo haya, je, hupotezi hadhi ya mwumini wa Mungu? Kazi Yangu leo ni hii: kuwafanya watu waelewe umuhimu wao, kuelewa yote Ninayoyafanya, na kufahamu uso wa kweli wa Mungu—hiki ndicho kitendo cha kufunga cha mpango Wangu wa usimamizi, hatua ya mwisho ya kazi Yangu. Ndiyo maana Nawaambia yote kuhusu mafumbo ya maisha mapema, ili nyote muweze kuyakubali kutoka Kwangu. Kwa kuwa hii ndiyo kazi ya nyakati za mwisho, lazima Niwaeleze ukweli wa maisha jinsi ilivyo kwa maana hamjawahi kuyakubali, hata ikiwa huwezi kuyakubali na kuyashika, kwa maana mmepungukiwa sana na hamna matayarisho ya kutosha. Ninataka kumalizia kazi Yangu, kukamilisha kazi yote Ninayopaswa kukamilisha, na kuwafahamisha kikamilifu kuhusu yale Ninayowatuma mfanye, msije mkapotoka tena na kuanguka katika mitego ya mwovu giza linapoingia. Kuna njia nyingi zaidi ya ufahamu wenu, maneno mengi msiyoelewa. Ninyi ni wapumbavu sana. Nazijua hali zenu na upungufu wenu vema. Kwa hivyo, ingawa kuna maneno mengi ambayo hamtaweza kuyaelewa, bado Ninataka kuwaambia ukweli huu wote ambao hamjawahi kuuchukua—kwa kuwa kila mara Ninahofu iwapo, katika hali yenu ya sasa, mtaweza kusimama na kutoa ushuhuda Kwangu. Sio kwamba Nawadhalilisha. Nyote mmekuwa wanyama ambao hawajapitia mafunzo Yangu ya rasmi, na hili ni jambo ambalo linaleta shauku kuhusu kiasi cha utukufu ulio ndani yenu. Ingawa Nimetumia nguvu nyingi kushughulika juu yenu, inaonekana kuwa vipengele vizuri ndani yenu havipo kabisa, ilhali dalili za uovu zinaweza kuhesabika kwa vidole na zinatolewa tu kwa madhumuni ya shuhuda za kumhaibisha Shetani. Takriban kila kitu kingine ndani yenu ni sumu ya Shetani. Mnaonekana Kwangu ni kama ambao mmepita kiwango cha kuokolewa. Kwa hivyo hali ikiwa jinsi ilivyo sasa, Naziangalia baadhi ya tabia zenu na hatimaye Najua vimo vyenu halisi. Hiyo ndiyo maana Nina wasiwasi kwa sababu yenu: Akiachwa kuishi maisha peke yake, je, mwanadamu atapata kuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyo sasa? Je, hamna wasiwasi kuhusu hali zenu za kitoto? Mnaweza hakika kuwa kama watu wateule wa Uyahudi, kuwa waaminifu Kwangu pekee Yangu katika kila hali? Kile mnachodhihirisha sio mchezo wa watoto wanapoondoka mbele ya wazazi wao, bali ni unyama unaoonekana katika wanyama ambao wako mbali na mjeledi wa mchungaji wao. Mnapaswa kujua hali yenu halisi, ambayo pia ni udhaifu mlio nao nyote, ambao ni ugonjwa mlio nao nyote. Kwa hivyo ombi Langu la pekee kwenu ni kwamba muwe na ushahidi Kwangu. Msije katika hali yoyote kuyaruhusu maradhi ya zamani kuchipuka tena. Jambo la muhimu zaidi ni kutoa ushuhuda. Hicho ndicho kiini cha kazi Yangu. Mnafaa kuyakubali maneno Yangu jinsi Maria alivyokubali ufunuo wa Yehova uliomjia kupitia kwenye ndoto, kuamini na kisha kutii. Hili pekee ndilo linakubalika kama kuwa mtakatifu. Kwa maana ni ninyi ndio mnasikia neno Langu zaidi, na ambao wamebarikiwa zaidi na Mimi. Ninawapa mali Yangu yote ya thamani, kuwakabidhi kila Nilicho nacho. Hali yenu na ile ya Wayahudi, hata hivyo, ni tofauti kabisa, ni kama nchi mbili tofauti. Lakini mkilinganishwa nao, mnapokea baraka nyingi zaidi yao. Huku wao wakisubiri kwa hamu ili kujitokeza Kwangu, muda mwingi Nimekuwa na ninyi, kutumia utajiri Wangu kwa pamoja. Kwa ulinganisho, ni nini kinachowapa haki ya kunifokea na kuzozana na Mimi na kudai sehemu za mali Yangu? Hampati vya kutosha? Ninawapa vingi sana, lakini Mnachonipa ni huzuni wa kuvunja moyo na dhiki na chuki isiyokomeshwa na kutoridhika. Mnakuwa wazushi sana, ilhali bado mnaiamsha huruma Yangu. Kwa hivyo sina la kufanya ila kuizima chuki Yangu kwenu na uzushi wakati baada ya mwingine. Katika hii miaka elfu kadhaa ya kazi Yangu, sikuwa Nimewahi kuleta pingamizi kwa mwanadamu awali kwa kuwa Nilikuwa Nimegundua kwamba katika historia ya kukua kwa mwanadamu, wale waongo zaidi miongoni mwenu ndio wanaofahamika zaidi. Wao ni kama urithi wa thamani ambao umeachiwa wewe na “babu” maarufu wa zama za kale. Jinsi gani Ninavyochukia wale nguruwe na mbwa ambao wana upungufu wa ubinadamu. Hamna hisia kabisa! Tabia zenu ni zenye uovu sana! Mioyo yenu ni migumu mno! Iwapo Ningepeleka haya maneno Yangu na hii kazi Yangu Uyahudi, Ningekuwa nimeshapata utukufu muda mrefu uliopita. Lakini sio hivyo miongoni mwenu. Miongoni mwenu kuna tu kutojali kwa kikatili, madharau yenu, na visingizio vyenu. Hamna hisia na hamna thamani yoyote!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana