Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 325

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye madharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio kujishusha kwa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Haupendi wosia au kependeza kwa Kristo, bali unapenda wale wajeuri wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea, sifa zao, misimamo yao katika mioyo ya mashetani wote, ushawishi wao, na mamlaka yao, ilhali unazidi kuipinga na kuikataa kazi ya Kristo. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni makafiri na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp