Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 336

Unasema kwamba unatambua Mungu mwenye mwili na unatambua kuwa Neno laonekana katika mwili, na bado unafanya mambo fulani kinyume, na hutendi jinsi Anataka utende, na humwogopi. Je, huku ni kumtambua Mungu? Unatambua Anachokisema ila unakataa kuyaweka katika vitendo hata yale mambo unayoweza kufanya na huzifuati njia zake. Je, huku ni kumtambua? Unamtambua ila mawazo yako ni kujikinga dhidi Yake, kutomcha kamwe. Ikiwa umeona na kuitambua kazi Yake na unafahamu kuwa Yeye ni Mungu, na bado unaendelea kuwa vuguvugu na bado hujabadilika hata kidogo, basi bado hujapata ushindi. Mtu aliyeshindwa hufanya chochote awezacho; anataka kuingia na kuufikia ukweli wa juu hata kama bado hana uwezo. Ni kwamba tu ana mipaka katika yale anayoweza kufanya, yaani, vitendo vyake vimefungiwa na kuwekewa mipaka. Lakini angalau anapaswa kufanya chochote katika uwezo wake. Ukifanya haya mambo, itakuwa ni kwa sababu ya kazi ya kushinda. Hata ukisema, “Kwa sababu Anaweza kunena maneno mengi ambayo mwanadamu hawezi, ikiwa si Mungu, ni nani?” Kuwa na mawazo kama haya hakumaanishi unamtambua Mungu. Ikiwa unamtambua Mungu unapaswa kuthibitisha kwa matendo. Ukiongoza kanisa lakini usiweze kutenda haki, na kutamani pesa na kufuja pesa za kanisa kisiri kwa faida yako—je, huku ni kutambua kuwa kuna Mungu? Mungu ni mwenye Uweza na wa kumcha. Unawezaje kukosa kuogopa kama kweli unatambua kuwa kuna Mungu? Unawezaje kuwa ulifanya kitu cha kuchukiza namna hiyo? Je, huko kunaweza kuitwa kuamini? Je, kweli wamtambua Mungu? Je, unamwamini Mungu? Unayemwamini ni Mungu asiye yakini; ndiyo maana huogopi! Wale wote wanaomtambua Mungu kweli na kumfahamu wanamcha na wanaogopa kufanya chochote kinachompinga na chochote kinachoenda kinyume na dhamiri yao; hususan wanaogopa kufanya chochote kinachoenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hili tu ndilo laweza kuwa ni kumtambua Mungu. Utafanya nini wazazi wako wakikuzuia kumwamini Mungu? Utampenda vipi Mungu ikiwa mume wako asiye muumini anakutendea mema? Aidha utampendaje Mungu ikiwa ndugu na dada zako wanakuchukia? Ikiwa unamtambua, basi utatenda ipasavyo na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi katika hali hizi zote. Ukikosa kutenda wazi na kusema tu kwamba unatambua uwepo wa Mungu, basi wewe ni msemaji tu. Unasema unamwamini na kumtambua. Je, unamtambua kwa njia gani? Unamwamini kwa njia gani? Je, unamwogopa? Unamcha? Unampenda moyoni mwako? Unapokuwa na huzuni bila yeyote wa kuegemea, unahisi Mungu ni wa kupendwa, halafu baadaye unasahau. Huku si kumpenda au kumwamini Mungu! Je, Mungu anataka mwanadamu apate nini mwishoni? Hali zote Nilizozitaja, kama vile: kufikiri kuwa wewe ni mtu mkubwa, kwamba unaelewa mambo upesi, kuwadhibiti wengine, kuwadharau wengine, kuwahukumu watu kwa misingi ya sura zao, kuwadhulumu watu waaminifu, kutamani pesa za kanisa, na kadhalika—kuondokewa na sehemu ya tabia mbovu za kishetani kama hizo ndiko kunakotakiwa kuonekana ndani yako baada ya wewe kushindwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp