Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 366

Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe. Wakati maji yanameza wanadamu, Nawaokoa kutokana na maji yaliyotuama na kuwapa nafasi ya kuishi upya. Wanadamu wanapopoteza imani yao ya kuishi, Nawavuta juu kutoka ukingo wa kifo, na kuwapa ujasiri wa kuishi, ili kwamba wananichukua kama msingi wa kuwepo kwao. Wanadamu wanaponiasi, Nawafanya Kunijua kwa kuasi kwao. Kutokana na asili ya zamani ya binadamu na kutokana na huruma Yangu, badala ya kuwaua binadamu, Nawaruhusu kutubu na kuanza upya. Wakati wanadamu wanateseka na kiangazi, Nawatoa kifoni kama bado wamesalia na pumzi moja, kuwazuia kudanganywa na Shetani. Watu wameona mikono Yangu mara ngapi; watu wameona uso Wangu karimu mara ngapi, kuuona uso Wangu wa tabasamu; na wameona adhama Yangu mara ngapi, kuona ghadhabu Yangu. Ingawa binadamu haujawahi kunijua, Siwakamati juu ya udhaifu wao kufanya matata yasiyohitajika. Kupitia ugumu wa binadamu, Nina huruma na udhaifu wake. Ni kwa sababu ya kuasi kwa wanadamu, kutokuwa na shukrani kwao, ndiko Nawaadibu kwa viwango tofauti.

Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati familia yao ya karibu ina furaha na iko sawa, wanadamu tayari wananiweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, na hivyo kufurahia furaha heri ya familia. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na anayegusika kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?

Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya binadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Kila mtu, inaonekana, anajaribu kunidanganya, kunipofusha, ili aweze kuingia na kupata shukrani Yangu. Sipendi wala kutia maanani udanganyifu wa watu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuupa binadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kama kitu kimoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Binadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wenu, mtachukiwa na kukataliwa na Mimi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 14

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp