Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 170
Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi...
Tunawakaribisha watafutaji wote wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu!
Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu; mwanadamu anatafuta kitu fulani duniani, anaonekana akichakura, anayo nia, inaonekana, ya kusubiri kurudi Kwangu—ilhali yeye hajui siku Yangu, na anaweza tu kutegemea mara kwa mara mwanga unaong’aa mashariki. Miongoni mwa watu wote, Ninatafuta wale wanaoupendeza moyo Wangu kwa kweli. Natembea miongoni mwa watu wote, na kuishi miongoni mwa watu wote, lakini mwanadamu yuko salama salmini duniani, na kwa hivyo hakuna wanaopendeza nafsi Yangu kwa kweli. Watu hawajui jinsi ya kuyajali mapenzi Yangu, hawawezi kuona matendo Yangu, na hawawezi kutembea katika mwanga na kumulikwa na mwanga huo. Hata ingawa mwanadamu daima anayathamini maneno Yangu, yeye hana uwezo wa kuona katika mikakati ya udanganyifu ya Shetani; kwa kuwa kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kufanya vile ambavyo moyo wake unatamani. Mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ninapompandisha, yeye hujiona asiyefaa, lakini hili halimfanyi awe na ari ya kuniridhisha. Yeye hushikilia tu kituo Nilichompa mikononi mwake na kukichunguza; bila hisia yoyote kwa uzuri Wangu, yeye anasisitiza badala yake kujijaza na baraka za kituo chake. Je, huu sio upungufu wa mwanadamu? Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma tu kabla ya kufikia kituo chako? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo chako? Wakati mmoja Nilikuwa mwenye huruma kwa mwanadamu, mara kwa mara—ilhali hakuna anayependa kwa dhati wala kuthamini haya, waliyasikiliza tu kama hadithi, au waliisoma tu kama tamthilia. Je, maneno Yangu hayauguzi moyo wa mwanadamu? Je, matamshi Yangu kwa kweli hayaleti mabadaliko yoyote? Inawezekana kuwa hakuna anayeamini katika kuwepo Kwangu? Mwanadamu hajipendi mwenyewe; badala yake, anaungana na Shetani ili kunivamia Mimi, na kumtumia Shetani kama “chombo” cha kunitumikia Mimi. Nitapenyeza katika mipango yote ya Shetani, na kuwazuia watu wote wa duniani dhidi ya kukubali uongo wa Shetani, ili wasije wakaniasi Mimi kwa ajili ya kuwepo kwa Shetani.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Tabia yote ya Mungu imefichuliwa katika mpango wote wa uongozi wa miaka elfu sita. Haikufichuliwa tu katika Enzi ya Neema, ni katika Enzi...
5. Bubujiko la Hewa Kitu cha tano ni kipi? Kitu hiki kinahusiana sana na maisha ya kila siku ya mwanadamu, na uhusiano huu thabiti. Ni kitu...
Hadithi ya 2. Mlima Mkubwa, Kijito Kidogo, Upepo Mkali, na Wimbi Kubwa Kulikuwa na kijito kidogo kilichotiririka kwa kuzungukazunguka,...
Nimewapa maonyo mengi na kuwapa ukweli mwingi ili kuwashinda. Leo mnajihisi kustawishwa zaidi kuliko mlivyohisi hapo zamani, kuelewa kanuni...
Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Upotovu wa Wanadamu | Dondoo 370