Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 294

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama kufundisha juu ya Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza? Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa mshindo wa tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wanaoamini kwamba wana ufahamu mdogo wa Mungu licha ya uzoefu wao halisi na ufahamu wa vitendo ni wale Anaowapenda zaidi. Ni wanadamu kama hawa ndio walio na ushahidi wa kweli na wanaweza kweli kukamilishwa na Mungu. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya dutu ya maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli mna imani ya kutembea njia hii, basi zidini kuifuata. Iwapo hamwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kuenda zenu kabla hamjachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Hamna uaminifu ama utii hata kidogo, ama mioyo ilio na kiu ya haki na ukweli. Na wala hamna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yenu mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Hamwezi kuweka mnachopaswa wala kusema mnachopaswa. Hamwezi kuweka katika vitendo kile ambacho mnapaswa, na hamwezi kufanya kazi mnayopaswa. Hamna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio mnalopasa. Hamjavumilia mateso mnayopaswa kuwa mmevumilia, na hamna imani mnayopaswa kuwa nayo. Hamna sifa yoyote kabisa; mna heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nawahimiza kwamba mko bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nanyi na kuvumilia mateso kwa ajili yenu. Mnaamini katika Mungu lakini bado hamjui mapenzi Yake; mnakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado hamwezi kukidhi mahitaji Yake. Mnaamini katika Mungu lakini bado hamumjui, na kuishi ingawa hamna lengo la kujaribu kufikia. Hamna maadili na hamna madhumuni. Mnaishi kama wanadamu lakini hamna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Mnafikiriwaje kuwa wanadamu? Mnaamini katika Mungu lakini mnamdanganya. Juu ya hayo, mnachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, hamwonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Hamwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu yasiyo ya maana. Kwa hivyo mnawezaje kufikiriwa kuwa wanadamu? Chakula mnachokula na hewa mnayopumua vimetoka kwa Mungu, mnafurahia neema Yake, na bado mwishowe, hamna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, mmekuwa watu wasio na maana wanaompinga Mungu. Si basi nyinyi ni wanyama wasio bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kuwaliko?

Hao wahubiri na wazee wanaosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu ni wapinzani wa Mungu na wako katika muungano na Shetani; wale kati yenu wasiosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu hawatakuwa hata wapinzani wakubwa zaidi wa Mungu? Juu ya hayo, hamna ushirikiano basi na Shetani? Wale wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu hawajui kuwa na makubaliano na moyo wa Mungu. Bila shaka, haiwezi kuwa ukweli kwa wale wanaoyaelewa madhumuni ya kazi Yake? Kazi ya Mungu kamwe haina makosa; badala yake, ni kufuatilia kwa mwanadamu kuliko na dosari. Wale wabaya wanaompinga Mungu makusudi sio waovu zaidi na mahasidi kuliko hao wahubiri na wazee? Wanaompinga Mungu ni wengi, na miongoni mwa wanadamu hao wengi, kuna aina mbalimbali ya upinzani dhidi ya Mungu. Kwa kuwa kuna kila aina ya waamini, hivyo pia kuna kila aina ya wale wanaompinga Mungu kila tofauti na kingine. Hakuna mmoja kati ya wale wasiotambua wazi madhumuni ya kazi ya Mungu anayeweza kuokolewa. Bila kujali jinsi mwanadamu anaweza kuwa alimpinga Mungu zamani, mwanadamu ajapo kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu na kujitolea juhudi zake ili kumridhisha Mungu, dhambi zake za awali zitafutiliwa mbali na Mungu. Bora tu mwanadamu anatafuta ukweli na kuuweka ukweli katika vitendo, Mungu hataweka akilini kile amefanya. Badala yake, ni kwa msingi wa kutenda ukweli kwa mwandamu ndiyo Mungu anamtetea mwanadamu. Hii ndiyo haki ya Mungu. Kabla ya mwanadamu kumwona Mungu ama kuwa na uzoefu wa kazi Yake, bila kujali jinsi mwanadamu anamtendea Mungu, Haliweki hili akilini. Hata hivyo, mara tu mwanadamu amwonapo Mungu, na kuwa na uzoefu wa kazi Yake, matendo yote na vitendo vyote vya mwanadamu vinaandikwa chini ndani ya “rekodi” na Mungu, kwani mwanadamu amemwona Mungu na kuishi ndani ya kazi Yake.

Wakati mwanadamu ameona kwa kweli kile Mungu alicho nacho na kile Alicho, aonapo ukuu Wake, na kweli kuja kujua kazi ya Mungu, na zaidi ya hayo, tabia ya awali ya mwanadamu inabadilika, basi mwanadamu atakuwa ameitupilia mbali kabisa tabia yake ya uasi inayompinga Mungu. Inaweza kusemwa kwamba kila mwanadamu amempinga Mungu wakati mmoja na kila mwanadamu ameasi dhidi ya Mungu. Hata hivyo, kama unamtii Mungu mwenye mwili kwa makusudi, na kwa hivyo kuuridhisha moyo wa Mungu kwa uaminifu wako, unaweka katika vitendo ukweli unaopaswa, kutekeleza jukumu lako unavyopaswa, na kufuata kanuni unavyopaswa, basi wewe ni mmoja aliye tayari kutupilia mbali uasi wake kumridhisha Mungu na mmoja anayeweza kukamilishwa na Mungu. Iwapo utakataa kutambua makosa yako na huna moyo wa kutubu; ukiendelea katika njia yako ya uasi na huna kabisa moyo wa kufanya kazi na Mungu na kumridhisha Mungu, basi mjinga mkaidi kama wewe kwa hakika ataadhibiwa na hatawahi kuwa mmoja wa kukamilishwa na Mungu. Iwapo hivyo, wewe ni adui wa Mungu leo na kesho, na hivyo pia utabaki adui wa Mungu siku ifuatayo; utakuwa milele mpinzani wa Mungu na adui wa Mungu. Mungu atakuachaje? Ni asili ya mwanadamu kumpinga Mungu, lakini mwanadamu hawezi kwa makusudi kutafuta “siri” za kumpinga Mungu kwa sababu kubadili asili yake ni kazi isiyoshindika. Kama hali ni hiyo, basi ni bora uende zako kabla hujachelewa, isiwe kurudi kwako wakati ujao kukawa kali zaidi, na isiwe asili yako kama ya mnyama ikaibuka na kuwa isiyotawalika mpaka mwili wako unaondolewa na Mungu mwishowe. Unaamini katika Mungu ili ubarikiwe; ikiwa mwishowe, balaa tu ndiyo itakayokupata, hiyo haitakuwa na thamani. Nawahimiza kuunda mpango mwingine; zoezi jingine litakuwa bora kuliko imani yenu kwa Mungu. Hakika kuna mengi kuliko njia hii moja? Hamngeweza kuendelea kuishi vile vile bila kutafuta ukweli? Mbona kuishi katika kutopatana na Mungu kwa namna hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp