Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani

Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli. Uaminifu mnaomiliki unatokana na kuishi kwa sanamu nyingine mioyoni mwenu, na kunihusu Mimi, Mungu anayechukuliwa kama asiye mkubwa wala mdogo ndani ya macho yenu, hamnitambui na chochote ila maneno. Ninaposema juu ya umbali wenu kutoka kwa Mungu, Ninamaanisha jinsi mlivyo mbali na Mungu wa kweli, ilhali Mungu asiye dhahiri Anaonekana kuwa karibu. Nisemapo “asiye mkubwa,” inamaanisha jinsi Mungu mnayemwamini siku ya leo anaonekana tu kuwa mwanadamu asiye na uwezo wa nguvu; mwanadamu asiye bora sana. Na Nisemapo, “asiye mdogo,” inamaanisha kuwa ingawa mwanadamu huyu hawezi kuita upepo na kuamuru mvua, Anaweza kumwita Roho wa Mungu kufanya kazi inayotingisha mbingu na dunia, hivyo kumchanganya mwanadamu. Kwa nje, nyote mnaonekana kuwa watiifu kwa huyu Kristo aliye duniani, lakini kwa kiini hamna imani Kwake wala kumpenda. Ninachomaanisha ni kwamba yule mliye na imani kwake kwa kweli ni yule Mungu asiye dhahiri katika hisia zenu, na yule kweli mnayempenda ni Mungu mnayemtamani usiku na mchana, lakini bado hamjamwona kamwe kibinafsi. Na kwa huyu Kristo, imani yenu ni sehemu tu, na upendo wenu Kwake si kitu. Imani inamaanisha imani na tumaini; upendo unamaanisha kuabudu na kusifu ndani ya mioyo yenu, bila kuondoka. Lakini imani yenu na upendo wenu kwa Kristo wa siku ya leo vimepunguka chini ya hili. Ikujapo kwa imani, mna imani Kwake jinsi gani? Ikujapo kwa upendo, mnampenda jinsi gani? Hamjui chochote kuhusu tabia Yake, wala hata kiini Chake, hivyo ni jinsi gani kwamba mna imani Kwake? Uko wapi ukweli wa imani yenu Kwake? Mnampenda jinsi gani? Uko wapi ukweli wa upendo wenu Kwake?

Wengi wamenifuata bila kusita hadi leo, na kwa miaka hii, nyote mmeteseka sana uchovu mwingi. Nimefahamu vizuri tabia na mazoea ya kila mmoja wenu. Ilikuwa vigumu sana kushirikiana nanyi. Cha huruma ni kwamba ingawa nina maarifa nyingi kuwahusu, hamna ufahamu hata kidogo kunihusu. Sio ajabu wengine wanasema mlidanganywa na mwanadamu katika wakati wa mkanganyiko. Hakika, hamwelewi chochote kuhusu tabia Yangu, na hata chini zaidi hamwezi kufahamu yaliyo akilini Mwangu. Sasa kutoelewana kwenu Kwangu ni kuongeza chumvi kwenye jeraha, na imani yenu Kwangu inabaki ile ya mkanganyiko. Badala ya kusema mna imani na Mimi, ingekuwa bora kusema kwamba nyote mnajaribu kupata neema Yangu na kujipendekeza Kwangu. Nia zenu ni rahisi—yeyote anayeweza kunituza, nitamfuata, na yeyote anayeweza kuniwezesha kutoroka majanga makubwa, nitaamini kwake, awe Mungu ama Mungu fulani yeyote. Hakuna kati ya haya yanayonihusu. Kuna wanadamu wengi kama hao kati yenu, na hali hii ni nzito sana. Ikiwa siku moja, majaribio yatafanywa kuona wangapi kati yenu wanamwamini Mungu kwa sababu mna umaizi kuhusu kiini Chake, basi Nahofia kwamba hakuna mmoja wenu atakuwa Ninavyotamani. Hivyo haitakuwa hoja kwa kila mmoja wenu kuzingatia swali hili: Mungu mliye na imani na Yeye ni tofauti sana na Mimi, hivyo nini basi ni kiini cha imani yenu kwa Mungu? Kadri mnavyoamini katika mnayemwita Mungu wenu, ndivyo mnavyozidi kupotea mbali sana Nami. Nini, basi, ni msingi wa suala hili? Nina uhakika hakuna mmoja wenu amewahi kufikiria suala hili, lakini mmefikiria uzito wake? Mmetoa mawazo kwa matokeo ikiwa mtaendelea na namna hii ya imani?

Sasa, matatizo yaliyowekwa mbele yenu ni mengi, na hakuna mmoja wenu aliye na uhodari wa kuleta ufumbuzi. Iwapo haya yataendelea, basi walio katika hatari ya kupoteza ni nyinyi wenyewe. Nitawasaidia kuyatambua matatizo, lakini itabakia kwenu kupata ufumbuzi.

Nawathamini sana wale wasioweka shaka kuhusu wengine na kuwapenda sana wale wanaokubali ukweli kwa urahisi; kwa aina hizi mbili za wanadamu Ninaonyesha utunzaji mkubwa, kwani machoni Mwangu wao ni waaminifu. Kama una ujanja mwingi, basi utakuwa na moyo uliolindwa na mawazo ya shaka juu ya mambo yote na wanadamu wote. Kwa sababu hii, imani yako Kwangu inajengwa kwa msingi wa shaka. Imani kama hii ni moja ambayo kamwe Sitaitambua. Bila imani ya kweli, basi upendo wenu uko mbali na upendo wa kweli. Na mkiwa hata na shaka na Mungu na kuwa na kisio juu Yake kwa kutaka, basi nyinyi bila shaka ni wanadamu wajanja zaidi. Mnakisia iwapo Mungu anaweza kuwa kama mwanadamu: mwenye dhambi isiyosameheka, mwenye tabia ndogo ndogo, asiye na haki na mantiki, aliyekosa hisia ya wema, anayechukua hatua za ubaya, udanganyifu na ujanja, na pia anayefurahishwa na uovu na giza, na kadhalika. Si sababu ambayo mwanadamu ana mawazo kama haya sababu mwanadamu hana hata ufahamu mdogo wa Mungu? Imani kama hii ni sawa na dhambi! Zaidi ya hayo, kuna hata wale wanaoamini kwamba Sifurahishwi na yeyote isipokuwa wale wanaojirairai na kujipendekeza, na kwamba wale wasiojua chochote kuhusu mambo kama haya watakuwa wasio maarufu na hawataweza kuhifadhi nafasi yao kwa nyumba ya Mungu. Je, haya ndiyo maarifa ambayo mmepata kwa miaka hii yote mingi? Ni haya ndiyo mliyoyapata? Na ufahamu wenu kunihusu ni mbali tu na kutoelewa kama huu; mengi zaidi, kuna kufuru kwenu dhidi ya Roho wa Mungu na kuitukana Mbingu. Hii ndiyo maana Ninasema kwamba imani kama yenu itawasababisha tu kupotea mbali na Mimi na kukuwa na upingamizi mkubwa dhidi Yangu. Kwa miaka mingi ya kazi, mmeona ukweli mwingi, lakini mnajua kile masikio Yangu yamesikia? Ni wangapi kati yenu walio tayari kukubali ukweli? Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na mhalifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa binadamu wa kawaida: bila moyo wa ukarimu na upendo wema. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na yenye huruma, asili ya ukarimu iko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu tu ni lengo tukufu ambalo mwanadamu anaweka matumaini, na umbo la hadithi aliyetungwa na mwanadamu. Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ikujapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ikujapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani. Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni hatolewi kwa hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana nia ya kibinafsi na hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande wa danganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duaniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni. Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa upande wa wasio wema na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Hiyo ni, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa na hivyo kuwa ghaibu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana takwimu wakuu na kuheshimu walio na ufasaha mkubwa. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayewapa kiasi kidogo cha utajiri, na mnakonda tu kwa sababu ya Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, ama hata kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Mmefikiria kuhusu swali hili?

Mnachofanya hakimkosei tu huyu Kristo, lakini muhimu zaidi, kinamkosea Mungu aliye mbinguni. Nadhani kwamba haya siyo madhumuni ya imani yenu kwa Mungu! Mnatamani sana kwa Mungu kufurahishwa nanyi, lakini bado mko mbali sana na Mungu. Tatizo ni nini hapa? Mnakubali tu maneno Yake, sio kushugulika na kupogoa Kwake, na hata mpangilio Wake wote. Zaidi ya hayo, hamwezi kuwa na imani kamilifu Kwake. Tatizo, basi, ni nini hapa? Kimsingi, imani yenu ni kaka tupu la yai lisiloweza kutoa kifaranga. Kwani imani yenu haijawaletea ukweli ama kuwapa maisha, na badala imewaletea hisia danganyifu ya tumaini na msaada. Madhumuni ya imani yenu kwa Mungu ni tumaini hili na msaada huu badala ya ukweli na maisha. Kwa hivyo, Nasema kwamba mwendo wa imani yenu kwa Mungu si mwingine bali ni kujaribu kupata neema ya Mungu kupitia utumwa na kutokuwa na aibu, na haiwezi kwa njia yoyote kuchukuliwa kuwa imani ya kweli. Kifaranga anaweza kujitokezaje kwa imani kama hii? Kwa maneno mengine, ni tunda lipi imani kama hii inaweza kuzalisha? Azma ya imani yenu kwa Mungu ni kutimiza nia zenu kupitia kumtumia Mungu. Huu sio ukweli zaidi unaoonyesha kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu? Mnaamini kuwepo kwa Mungu aliye mbinguni lakini mnakataa yule Mungu aliye duniani. Hata hivyo, Sikubaliani na maoni yenu. Nawapongeza tu wale wanadamu wanaosimama imara na kumtumikia Mungu wa duniani, kamwe sio wale wasiomkiri Kristo aliye duniani. Bila kujali jinsi wanadamu kama hawa walivyo waaminifu kwa Mungu aliye duniani, mwishowe, hawatauepuka mkono Wangu unaoadhibu waovu. Wanadamu kama hawa ni waovu; ni wale waovu wanaompinga Mungu na hawajawahi kumtii Kristo kwa furaha. Bila shaka, idadi yao inajumuisha wale wote wasiomjua na, zaidi, wasiomkiri Kristo. Mnaamini kwamba mnaweza kutenda mtakavyo kwa Kristo iwapo nyinyi ni waaminifu kwa Mungu aliye mbinguni. Si sawa! Kutomjua Kristo ni kutomjua pia Mungu wa mbinguni. Bila kujali uaminifu wenu kwa Mungu aliye mbinguni, ni maneno matupu tu na kujifanya, kwani Mungu aliye duniani si muhimu tu kwa mwanadamu kupokea ukweli na ufahamu mkubwa, lakini hata zaidi ni muhimu kwa lawama ya mwanadamu na baadaye kwa kuushika ukweli kuwaadhibu waovu. Mmeelewa faida na matokeo hapa? Mmepata kuyapitia? Ningependa nyinyi siku moja hivi karibuni muelewe ukweli huu: Kumjua Mungu, mnapaswa kumjua sio tu Mungu wa mbinguni lakini, hata muhimu, Mungu aliye duniani. Msiyachanganye yaliyo kipaumbele ama kuruhusu yaliyo chini kuchukua nafasi ya yaliyo makubwa. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kujenga uhusiano mzuri na Mungu, kuwa karibu na Mungu, na kupeleka moyo wako karibu na Yeye. Kama umekuwa wa imani kwa miaka nyingi na kushirikiana na Mimi kwa muda mrefu, lakini bado unabaki mbali na Mimi, basi Nasema kwamba ni lazima mara nyingi unaikosea tabia ya Mungu, na mwisho wako utakuwa mgumu sana kufikiria. Kama miaka mingi ya ushirikiano na Mimi haijakubadilisha kuwa mwanadamu aliye na ubinadamu na ukweli, na badala yake njia zako za uovu zimekuwa imara ndani ya asili yako, ikiwa wewe si tu mwenye kiburi mara mbili lakini kutonielewa Kwako kunakuwa hata kwa kuhuzunisha zaidi, kiasi kwamba unakuja kunichukulia kuwa rafiki yako wa kando, basi Nasema kwamba mateso yako si ya ngozi ya ndani, lakini yamepenya ndani ya mifupa yako. Na yote unayoweza kufanya ni kusubiri na kuandaa mazishi yako! Huhitaji kunisihi basi Niwe Mungu wako, kwani umetenda dhambi inayostahili kifo, dhambi isiyosameheka. Hata kama Ningeweza kuwa na huruma nawe, Mungu aliye mbinguni Atasisitiza kuchukua maisha yako, kwani kosa lako dhidi ya tabia ya Mungu si shida ya kawaida, lakini moja iliyo kubwa sana kiasili. Wakati utakapokuja, usinilaumu kwa sababu ya kutokujulisha mbeleni. Yote yanarudia haya: Wakati unashirikiana na Kristo—Mungu aliye duniani—kama mwanadamu wa kawaida, hiyo ni, unapoamini kwamba Mungu huyu si chochote ila ni mwanadamu, ni hapo basi ndipo utaangamia. Hili ndilo onyo Langu la pekee kwenu nyinyi nyote.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana