Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 10

Kutomcha Mungu na Kutojiepusha na Maovu ni Kumpinga Mungu

Sasa hivi mnaangaliana uso kwa uso na Mungu, uso kwa macho na neno la Mungu. Maarifa yenu ya Mungu ni mengi zaidi kuliko yale ya Ayubu. Kwa nini Naleta suala hili? Kwa nini Ninaongea hivi? Ningependa kuwaelezea hoja moja, lakini kabla Sijafanya hivyo, Ningependa kuwauliza swali: Ayubu alijua machache sana kumhusu Mungu, ilhali angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo basi kwa nini watu siku hizi wanashindwa kufanya hivyo? (Upotoshaji mkubwa.) “Upotoshaji mkubwa”—hicho ndicho kiini cha swali, lakini Sitawahi kulitazama hivyo. Mara nyingi mnachukua falsafa na barua ambazo mnazungumzia mara kwa mara, kama vile “upotoshaji mkuu,” “kuasi dhidi ya Mungu,” “kutotii Mungu,” “kutotii,” “kutopenda ukweli” na mnatumia vidahizo kama hivi kuelezea kiini halisi cha kila swali. Hii ni njia isiyofaa ya kufanya mazoezi. Kutumia jibu moja kuelezea maswali yaliyo na asili tofauti mara moja huibua shaka ya kuukufuru ukweli na Mungu. Sipendi kusikia aina hii ya jibu. Hebu fikiria! Hakuna yeyote kati yenu amefikiria kuhusu suala hili, lakini kila siku Mimi Ninaliona, na kila siku Mimi Ninalihisi. Hivyo basi, mnafanya, na Mimi Ninatazama. Wakati mnapolifanya, hamwezi kuhisi kiini halisi cha suala hili. Lakini wakati Ninapoliona, Ninaweza kuona kiini halisi chake, na Ninaweza kuhisi kiini chake halisi vilevile. Hivyo basi kiini hiki ni nini basi? Kwa nini watu siku hizi hawamchi Mungu na hawaambai maovu? Majibu yenu yako mbali na kuweza kueleza kiini halisi cha swali hili, na haziwezi kutatua kiini halisi cha swali hili. Hiyo ni kwa sababu kunacho chanzo hapa ambacho nyinyi hamna habari kukihusu. Chanzo hiki ni kipi? Ninajua mnataka kusikia kukihusu, hivyo basi Nitawaambia kuhusu chanzo cha swali hili.

Hapo mwanzo kabisa wa kazi ya Mungu, Alichukulia vipi binadamu? Mungu alimwokoa binadamu; Alimchukulia binadamu kama mmoja wa familia Yake, kama mlengwa wa kazi Yake, kama kile ambacho Alitaka kukishinda, kuokoa, na kile ambacho Alitaka kufanya kuwa kitimilifu. Huu ndio uliokuwa mwelekeo wa Mungu kwa binadamu mwanzoni mwa kazi Yake. Lakini mwelekeo wa binadamu kwa Mungu wakati huo ulikuwa upi? Mungu alikuwa haeleweki kwa binadamu na binadamu alimchukulia Mungu kuwa mgeni. Inaweza kusemwa kwamba mwelekeo wa binadamu kwa Mungu ulikuwa si sahihi, na binadamu hakuwa na uwazi mzuri wa namna ya kumchukua Mungu. Hivyo basi Alimshughulikia alivyopenda yeye, na akafanya kile alichopenda yeye. Je, binadamu alikuwa na mtazamo kuhusu Mungu? Hapo mwanzoni, binadamu hakuwa na mtazamo wowote kuhusu Mungu. Mtazamo wa binadamu kama ulivyojulikana, ulikuwa tu baadhi ya dhana na fikira kumhusu Mungu. Kile ambacho kiliingiliana na dhana za watu kilikubalika; kile ambacho hakikuingiliana kiliitikiwa juujuu, lakini katika mioyo yao watu waligongana pakubwa nacho na wakakipinga. Huu ndio uliokuwa uhusiano wa binadamu na Mungu hapo mwanzoni: Mungu alimwona binadamu kama mwanachama wa familia, ilhali binadamu alimchukulia Mungu kama mgeni. Lakini baada ya kipindi cha kazi ya Mungu, binadamu alielewa hatimaye kile ambacho Mungu alikuwa akijaribu kutimiza. Watu hatimaye walijua kwamba Mungu ndiye aliyekuwa Mungu wa kweli, na hatimaye wakajua kile ambacho binadamu angepokea kutoka kwa Mungu. Binadamu alimchukulia Mungu wakati huu kuwa nini? Binadamu alichukulia Mungu kuwa tegemeo kuu, akitumai kupokea neema, kupokea baraka, kupokea ahadi. Naye Mungu alimchukulia binadamu wakati huu kuwa nini? Mungu alimchukulia binadamu kuwa mlengwa wa ushindi Wake. Mungu alitaka kuyatumia maneno ili kumhukumu binadamu, kumjaribu binadamu, kumpa majaribio binadamu. Lakini kwa wanadamu wakati huu hasa, Mungu alikuwa kifaa ambacho angetumia kutimiza shabaha zake binafsi. Watu waliona kwamba ukweli uliotolewa na Mungu ungeweza kushinda na kuwaokoa, na kwamba walikuwa na fursa ya kupokea vitu walivyotaka kutoka kwa Mungu, hatima ambayo walikuwa wakitaka. Kwa sababu ya haya, chembechembe ya uaminifu kajitunga katika mioyo yao, na walikuwa radhi kumfuata Mungu huyu. Muda ukapita, na watu wakawa na maarifa fulani ya juujuu na ya kifalsafa kuhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba walikuwa wameanza “kuzoeana” zaidi na zaidi na Mungu. Neno likitamkwa na Mungu, mahubiri Yake, ukweli Aliokuwa ameutoa awali, na kazi Yake—watu walikuwa “wamezoea” zaidi na zaidi. Hivyo basi, watu walidhania kimakosa kwamba Mungu hakuwa tena mgeni, na kwamba tayari walikuwa wakitembea njia ya uwiano na Mungu. Tangu hapo mpaka sasa, watu wamesikiliza mahubiri mengi ya ukweli, na wamepitia kazi nyingi ya Mungu. Ilhali kwenye uingiliaji kati na uzuiaji wa mambo mengi tofauti na hali, watu wengi hawawezi kufikia hali ya kutia ukweli katika matendo, na hawawezi kufikia hali ya kumtosheleza Mungu. Watu wanazidi kuwa goigoi, wanazidi kuikosa imani. Wanazidi kuhisi ni kana kwamba matokeo yao binafsi hayajulikani. Hawathubutu kuwa na mawazo yoyote ya kupita kiasi, na hawatafuti kupiga hatua yoyote ya maendeleo; wanafuata tu shingo upande, wakienda mbele hatua kwa hatua. Kuhusiana na hali ya sasa ya binadamu, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu ni upi? Tamanio tu la Mungu ni kuukabidhi ukweli huu kwa binadamu, na kutia moyoni mwa binadamu njia Yake, na kupangilia hali mbalimbali ili kujaribu binadamu katika njia tofauti. Shabaha yake ni kuweza kuchukua maneno haya, ukweli huu, na kazi Yake, na kusababisha matokeo ambapo binadamu anaweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Watu wengi ambao Nimewaona wanalichukua tu neno la Mungu na kuliona kuwa falsafa, kuliona kuwa barua, kuliona kuwa kanuni za kufuatwa. Wanapoendelea na shughuli zao na kuongea au kukabiliwa na majaribio, hawachukulii njia ya Mungu kama njia ambayo wanafaa kuifuata. Hali hii hasa ni kweli wakati watu wanapokabiliwa na majaribio makuu; Sijamwona yeyote ambaye alikuwa anatia katika matendo kwa mwelekeo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu ya hili, mwelekeo wa Mungu kwa binadamu umejaa chuki na chukizo ya kupindukia. Baada ya Mungu kuwapa watu majaribio kadhaa, hata mara mia, bado hawana mwelekeo wazi wa kuonyesha bidii yao—ninataka kumcha Mungu na kujiepusha na maovu! Kwa sababu watu hawana bidii hii, na hawaonyeshi ishara kama hii, mwelekeo wa sasa wa Mungu kwao si kama ule wa hapo nyuma, Alipotoa rehema Yake, akatoa uvumilivu wake, akatoa ustahimilivu na subira yake. Badala yake, Amesikitishwa mno na binadamu. Ni nani aliyesababisha masikitiko haya? Aina hii ya mwelekeo ambao Mungu anao kwa binadamu, unamtegemea nani? Unategemea kila mtu anayemfuata Mungu. Kwenye mkondo wa miaka Yake mingi ya kazi, Mungu ametaja mahitaji mengi kwa binadamu, na kupangilia hali nyingi kwa binadamu. Lakini haijalishi ni vipi binadamu ametenda, na haijalishi ni mwelekeo upi ambao binadamu anao kwa Mungu, binadamu hawezi kutenda kwa njia wazi kulingana na shabaha ya kumcha Mungu na kujiepusha na uovu. Hivyo basi, Nitajumlisha yote haya kwa msemo mmoja, na kuweza kutumia msemo huu kuelezea kila kitu ambacho tumeweza kuzungumzia kuhusiana na ni kwa nini watu hawawezi kutembea kwa njia ya Mungu—mche Mungu na kujiepusha na maovu. Msemo huu ni upi? Msemo huu ni: Mungu humchukulia binadamu kama kifaa cha wokovu Wake, kifaa cha kazi Yake; binadamu humchukulia Mungu kama adui wake, kama tabaini yake. Je, unalielewa suala hili sasa? Kile ambacho ndicho mwelekeo wa binadamu; kile ambacho ndicho mwelekeo wa Mungu; kile ambacho ni uhusiano wa binadamu na Mungu—hivi vyote viko wazi sana sasa. Haijalishi ni kiwango kipi cha mahubiri ambayo mmeyasikiliza, yale mambo ambayo mliyoyatolea muhtasari nyinyi wenyewe—kama vile kuwa mwaminifu kwa Mungu, kumtii Mungu, kutafuta njia ya uwiano na Mungu, kutaka kuishi daima dawamu kwa ajili ya Mungu, kuishi kwa ajili ya Mungu—kwangu Mimi mambo hayo hayajumuishi kutembea kwa njia ya Mungu kwa nadhari, ambako ni kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Badala yake, ni njia mbalimbali kupitia kwazo mnaweza kufikia shabaha fulani. Ili kutimiza shabaha hizi, mnaangalia shingo upande baadhi ya taratibu. Na ni taratibu hizi hasa ambazo huwapeleka watu mbali zaidi kutoka katika njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kumweka Mungu katika upinzani na binadamu kwa mara nyingine.

Swali tunalolizungumzia leo ni zito kidogo, lakini licha ya chochote, bado Natumai kwamba mtakapopitia yale yote yajayo, na kwenye nyakati zijazo, mnaweza kufanya kile ambacho Nimewaambia mfanye. Msipuuze Mungu na kumchukulia Yeye kama hewa tupu, kuhisi kwamba Anakuwepo tu nyakati zile Anapokuwa Mwenye manufaa kwako, lakini wakati ule ambao humhitaji unahisi kwamba Yeye hayupo. Unaposhikilia uelewa huu katika bila ufahamu, tayari umemghadhabisha Mungu. Pengine kunao watu wanaosema: “Mimi sichukulii Mungu kama hewa tupu, mimi siku zote humwomba Mungu, siku zote mimi humtosheleza Mungu, na kila kitu ninachokifanya huwa katika ule upana na kiwango na kanuni zinazohitajika na Mungu. Bila shaka siendelei kulingana na mawazo yangu binafsi.” Ndiyo, namna ambayo unafanya mambo ni sahihi. Lakini unafikiria vipi wakati unakumbana macho kwa macho na suala? Unakuwa na matendo gani unapokabiliwa na suala? Baadhi ya watu huhisi kwamba Mungu yupo wakati wanapomwomba Yeye, na Kumsihi kuwasikiliza. Lakini wakati wanapokabiliwa na suala wanakuja na fikira zao binafsi na wanataka kuzitii. Hapa Mungu huchukuliwa kama hewa tupu. Aina hii ya hali humfanya Mungu kutokuwepo. Watu hufikiria kwamba Mungu anafaa kuwepo wakati wanapomhitaji Yeye, na wakati hawamhitaji Mungu Hafai kuwepo. Watu hufikiria kwamba kufanya mambo kulingana na mawazo yao katika matendo ya maisha ni tosha. Wanasadiki wanaweza kufanya mambo vyovyote vile wapendavyo. Wanafikiria tu kwamba hawahitaji kutafuta njia ya Mungu. Watu ambao kwa sasa wamo katika aina hii ya hali, hali hii ya namna—huoni kwamba karibu wataingia hatarini? Baadhi ya watu husema: “Haijalishi kama karibu nitaingia hatarini au la, nimesadiki kwa miaka mingi sana, na ninasadiki kwamba Mungu hataniacha kwa sababu Asingeweza kustahimili kuniacha mimi.” Watu wengine husema: “Hata tangu nilipokuwa kwenye tumbo la mama yangu, nilimsadiki Bwana, tangu hapo mpaka sasa, jumla ya miaka arubaini au hamsini hivi. Kwa mujibu wa muda, mimi ndimi nimefuzu zaidi kuokolewa na Mungu; mimi ndimi nimefuzu zaidi kuwepo. Kwenye kipindi hiki cha muda cha miongo minne au mitano, niliiacha familia yangu na kazi yangu. Nilijitolea kila kitu nilichokuwa nacho kwa Mungu, kama pesa, ardhi, anasa na muda wa familia; sijala vyakula vingi vitamu; sijafurahia vitu vingi vya kusisimua; sijatembelea sehemu nyingi za kuvutia; nimeweza hata kupitia mateso ambayo hata watu wa kawaida wasingevumilia. Kama Mungu hawezi kuniokoa mimi kwa sababu ya haya yote, basi mimi nashughulikiwa kwa njia isiyo ya haki na siwezi kuamini kwa aina hii ya Mungu.” Je, kunao watu wengi walio na aina hii ya mtazamo? (Kunao wengi sana.) Basi leo Nitawasaidia kuelewa hoja moja: Kila mmoja wa hao anayeshikilia aina hii ya maoni anachukua hatua zitakazomdhuru mwenyewe. Hii ni kwa sababu wanatumia maoni yao binafsi katika kuyafunika macho yao. Ni kufikiria kwao hasa, na hitimisho yao binafsi zinazochukua nafasi ya kiwango cha kile Mungu anahitaji kutoka kwa binadamu, ndizo zinazowashikilia dhidi ya kukubali nia za kweli za Mungu, na kuwafanya kutoweza kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu, na kuwafanya pia kupoteza fursa yao kufanywa kuwa watimilifu na Mungu na kutokuwa na sehemu au mgao katika ahadi ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp