Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 25

Mungu Awatengenezea Adamu na Hawa Nguo za Ngozi

Mwa 3:20-21 Adamu akampa mke wake jina la Hawa; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mama ya wote wenye uhai. Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha.

Katika picha hii ya “Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha,” ni wajibu gani ambao Mungu anatekeleza anapokuwa na Adamu na Hawa? Na ni katika aina gani ya uajibu ambao Mungu anajitokeza katika ulimwengu akiwa tu na wanadamu wawili? Kutekeleza wajibu wa Mungu? Kaka na dada kutoka Hong Kong, tafadhali jibuni. (Kutekeleza wajibu wa mzazi.) Kaka na dada kutoka Korea Kusini, ni wajibu wa aina gani mnafikiria Mungu anatekeleza hapa? (Kiongozi wa familia.) Kaka na dada kutoka Taiwan, mnafikiria nini? (Wajibu wa mtu katika familia ya Adamu na Hawa, wajibu wa mwanafamilia.) Baadhi yenu mnafikiria kuwa Mungu anajitokeza kama mwanafamilia wa Adamu na Hawa, huku baadhi wakisema kwamba Mungu anajitokeza kama kiongozi wa familia na wengine wanasema kwamba Anajitokeza kama mzazi. Haya yote yanafaa sana. Lakini ni nini hasa Ninachotilia mkazo hapa? Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminifu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu. Hapa, ukweli na unyenyekevu wa Mungu unawezesha zaidi watu kuona namna ambavyo Anapendeka. Kwa kinyume cha mambo, yule Mungu mkubwa sana, Mungu anayependeka na yule Mwenyezi Mungu katika mioyo ya watu ni mdogo sana, asiyevutia, na asiyeweza kuhimiliwa hata mara moja. Unapouona mstari huu na kuisikia hadithi hii, unamkasirikia Mungu kwa sababu Alifanya kitu kama hiki? Baadhi ya watu wanaweza kufanya hivyo, lakini kwa wengine itakuwa ni tofauti kabisa. Watafikiri Mungu ni mkweli na anapendeka, na hasa ni ule ukweli na uzuri wa Mungu ndiyo unaowafurahisha. Kwa kadri wanavyoona ule upande wa kweli wa Mungu, ndipo wanapothamini uwepo wa kweli wa upendo wa Mungu, umuhimu wa Mungu katika mioyo yao, na namna anavyosimama kando yao kila muda.

Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahali, na enzi. Ukweli na uzuri wa Mungu unaweza kwa kweli kuonyeshwa kupitia kufanya jambo ambalo watu wanafikiria si la kipekee na ni dogo, jambo ambalo ni dogo sana kiasi cha kwamba watu hata hawafikirii angeweza kufanya. Mungu si mnafiki. Hakuna kupiga chuku, kufunika ukweli, majivuno au kiburi katika tabia na kiini Chake. Siku zote Hajigambi, lakini badala yake Anapenda, Anaonyesha hali ya kujali, Anaangalia, na kuwaongoza wanadamu Aliowaumba kwa uaminifu na dhati. Haijalishi ni kiwango kipi ambacho watu wanaweza kuthamini, kuhisi, au kuona, Mungu kwa hakika anafanya mambo haya. Je, kujua kwamba Mungu anacho kiini kama hicho kunaweza kuathiri upendo wa watu kwake Yeye? Kutaweza kushawishi namna wanavyomcha Mungu? Ninatumai utakapoelewa upande halisi wa Mungu utaweza kuwa hata karibu zaidi na Yeye na kuweza kuthamini hata zaidi na kwa kweli upendo Wake na utunzaji Wake kwa wanadamu, huku wakati huohuo pia kumpa moyo wako na kutowahi tena kuwa na shaka au wasiwasi wowote kwake Yeye. Mungu anafanya kimyakimya kila kitu kwa ajili ya binadamu, akifanya kimyakimya kupitia ukweli, uaminifu, na upendo Wake. Lakini siku zote Hana hofu au majuto yoyote kwa yale yote Anayofanya, wala hahitaji mtu yeyote kumlipa Yeye kwa njia yoyote au kuwa na nia za kuwahi kupokea kitu kutoka kwa wanadamu. Kusudio tu la kila kitu Alichowahi kufanya ni ili Aweze kupokea imani na upendo wa kweli kutoka kwa wanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp