Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 36

Mungu Lazima Aangamize Sodoma

Mwa 18:26 Na Yehova akasema, Nikipata katika Sodoma watu hamsini wenye haki ndani ya mji huo, basi nitaacha pahali pote kwa sababu yao.

Mwa 18:29 Na akanena tena na yeye, na kusema, Iwapo watu arobaini wakapatikana humo. Naye akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:30 Na akamwambia, Iwapo watapatikana huko watu thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:31 Na akasema, Iwapo watapatikana huko watu ishirini. Naye akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Mwa 18:32 Na akasema, Iwapo watapatikana huko watu kumi. Naye akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake

Vifungu hivi vilivyotajwa hapo juu vinayo maneno msingi mbalimbali: nambari. Kwanza, Yehova alisema kwamba kama Angewapata wenye haki hamsini ndani ya Jiji, basi Angepanusurisha mahali hapo, hii ni kusema, Asingeangamiza jiji hilo. Hivyo walikuwepo, kwa hakika, watakatifu hamsini ndani ya Sodoma? Hawakuwemo. Muda mfupi baadaye, Ibrahimu alimwambia nini Mungu? Alisema, labda kutakuwemo arubaini waliopatikana humo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Kisha, Ibrahimu akasema huenda wakawepo thelathini watakaopatikana hapo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Na labda ishirini? Sitafanya hivyo. Kumi? Sitafanya hivyo. Kulikuwemo, kwa hakika, wenye haki kumi ndani ya jiji? Hapakuwa kumi—lakini kulikuwemo na mmoja. Na huyu mmoja alikuwa nani? Alikuwa Loti. Wakati huo, kulikuwepo tu na mwenye haki mmoja kwenye eneo la Sodoma, lakini Mungu alikuwa mmakinifu sana au mkali kuhusiana na nambari hii? La, hakuwa hivyo! Na wakati binadamu aliendelea kuulizia, “Na je wale arubaini?” “Na je wale thelathini?” mpaka pale alipofika katika sehemu ile ya “Na je wale kumi?” Mungu alisema, “Hata kama wangalikuwemo kumi, Singeangamiza jiji hilo; Ningelinusurisha, na kuwasamehe wale watu wengine mbali na wale kumi.” Idadi ya watu kumi ingekuwa ya kuhurumiwa vya kutosha, lakini ilitokea kwamba, kwa hakika, hakukuwemo na hata ile idadi inayohitajika ya watu wenye haki kule Sodoma. Unaona, basi, kwamba katika macho ya Mungu dhambi na maovu ya watu wa jiji ilikuwa kwa kiasi kwamba Mungu hakuwa na chaguo lolote ila kuwaangamiza. Mungu alimaanisha nini Aliposema kwamba Asingeliharibu jiji kama kungekuwemo na wenye haki hamsini? Nambari hizi hazikuwa muhimu kwa Mungu. Kile kilichokuwa muhimu kilikuwa kama jiji lilikuwa na wenye haki Aliotaka au la. Kama jiji lisingekuwa na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja, Mungu asingeruhusu madhara kuwepo kutokana na Yeye kuangamiza jiji hilo. Kile ambacho haya yote yanamaanisha ni kwamba, haijalishi kama Mungu angeliangamiza jiji au la, na haijalishi idadi ya wenye haki waliokuwa ndani ya jiji hilo, kwake Mungu jiji hili lenye dhambi lilikuwa limelaaniwa na lilikuwa limejaa maovu, na hivyo lilifaa kuangamizwa, na kutoweka kwenye macho ya Mungu huku nao wenye haki wakisali. Haikulijalisha enzi husika, haikujalisha awamu ya maendeleo ya wanadamu, mwelekeo wa Mungu haubadiliki: Anachukia maovu, na Anawajali wenye haki mbele ya macho Yake. Mwelekeo huu wazi wa Mungu ndiyo pia ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Kwa sababu hakukuwepo na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja ndani ya jiji, Mungu hakusita tena. Matokeo yake ni kwamba Sodoma ingeangamizwa bila kusita. Mnaona nini katika haya? Katika enzi hiyo, Mungu asingeangamiza jiji kama wamo wenye haki hamsini ndani yake, wala kama kulikuwemo kumi, kumaanisha kwamba Mungu angeamua kusamehe na kumvumilia wanadamu, au angefanya kazi ya kuongoza, kwa sababu ya watu wachache ambao waliweza kumstahi na kumwabudu Yeye. Mungu hutilia maanani haki ya binadamu, Hutilia maanani sana kwa wale wanaoweza kumwabudu Yeye, na Anatilia maanani sana wale wanaoweza kufanya matendo mema mbele yake.

Kutoka nyakati za mapema sana hadi leo, umewahi kusoma ndani ya Biblia kuhusu Mungu kuuwasilisha ukweli, au kuzungumzia kuhusu njia ya Mungu, kwa mtu yeyote? La, hujawahi. Maneno ya Mungu kwa binadamu tunayoyasoma yaliwaambia watu tu cha kufanya. Baadhi walienda na wakayafanya, baadhi hawakuyafanya; baadhi walisadiki, na baadhi hawakusadiki. Hivyo ndivyo ilivyokuwa tu. Hivyo, wenye haki wa enzi hiyo—wale waliokuwa wenye haki mbele ya macho ya Mungu—walikuwa wale tu ambao wangeweza kuyasikia maneno ya Mungu na kufuata amri za Mungu. Walikuwa watumishi waliotekeleza maneno ya Mungu miongoni mwa binadamu. Je, watu kama hao wangeweza kuitwa wale wanaomjua Mungu? Wangeweza kuitwa watu waliofanywa kuwa watimilifu na Mungu? La, wasingeweza kuitwa hivyo. Na hivyo, licha ya idadi yao, kwenye macho ya Mungu hawa wenye haki walistahili kuitwa wandani wa Mungu? Wangeweza kuitwa mashahidi wa Mungu? Bila shaka la! Hawakustahili kamwe kuitwa wandani na mashahidi wa Mungu. Na hivyo Mungu aliwaita watu kama hawa vipi? Kwenye Biblia, hadi kufikia kwenye vifungu vya maandiko ambavyo tumetoka kusoma hivi punde, kulikuwa na matukio mengi ya Mungu kuwaita “Mtumishi wangu.” Hivi ni kusema, kwa wakati huo kwenye macho ya Mungu watu hawa wenye haki walikuwa watumishi wa Mungu, walikuwa watu waliomhudumia Yeye duniani. Naye Mungu alifikiria vipi kuhusu jina hilo? Kwa nini Akawaita hivyo? Je, Mungu anavyo viwango ambavyo Anatumia katika Kuwaita watu ndani ya moyo Wake? Bila shaka anavyo. Mungu anavyo viwango, haijalishi kama Anawaita watu wenye haki, watimilifu, wanyofu, au watumishi. Anapomwita mtu mtumishi Wake, Anayo imani thabiti kwamba mtu huyu anaweza kuwapokea wajumbe Wake, na anaweza kufuata amri Zake, na anaweza kutekeleza kile ambacho ameamrishwa kufanya na wale wajumbe. Na mtu huyu anatekeleza nini? Kile ambacho Mungu anamwamuru binadamu kufanya na kutekeleza duniani. Wakati huo, kile ambacho Mungu alimwomba binadamu kufanya na kutekeleza duniani kingeweza kuitwa njia ya Mungu? La, kisingeweza. Kwani wakati huo, Mungu alimwomba tu binadamu kufanya mambo machache rahisi; Alitamka amri chache rahisi, Akimwambia binadamu kufanya hiki au kile, na si zaidi ya hayo. Mungu alikuwa akifanya kazi kulingana na mpango Wake. Kwa sababu, wakati huo, masharti mengi hayakuwepo, muda ulikuwa haujatimia, na ilikuwa vigumu kwake wanadamu kuvumilia njia ya Mungu, hivyo basi njia ya Mungu ilikuwa bado haijaanza kuwasilishwa mbele kutoka kwenye moyo wa Mungu. Katika haya, tunaona kwamba haijalishi kama kulikuwa thelathini au ishirini ya wale wenye haki aliozungumzia Mungu, mbele ya macho Yake wote walikuwa watumishi Wake. Wakati wajumbe wa Mungu walipowajia watumishi hawa, wangeweza kuwapokea, na kufuata amri zao, na kutenda kulingana na maneno yao. Haya ndiyo hasa yaliyofaa kufanywa, na kutimizwa, na watumishi mbele ya macho ya Mungu. Mungu ni mwenye busara katika majina Yake kwa watu. Si kwa sababu walikuwa vile mlivyo sasa ndiyo Aliwaita watumishi Wake—kwa sababu walikuwa wamesikia mahubiri mengi, walijua kile ambacho Mungu alifaa kufanya, walielewa mengi kuhusu mapenzi ya Mungu na walifahamu mpango Wake wa usimamizi—lakini kwa sababu ubinadamu wao ulikuwa wenye uaminifu na waliweza kutii maneno ya Mungu; wakati Mungu alipowaamuru, waliweza kuweka pembeni kile walichokuwa wakifanya na kutekeleza kile ambacho Mungu aliwaamuru kufanya. Na hivyo, kwake Mungu safu ile nyingine ya maana kwenye cheo cha mtumishi ni kwamba walishirikiana na kazi Yake duniani na ingawaje hawakuwa wajumbe wa Mungu, hao ndio waliokuwa watekelezaji na wafuatiliaji wa maneno ya Mungu duniani. Unaona, basi, watumishi hawa au wenye haki hawa walikuwa na umuhimu mkubwa katika moyo wa Mungu. Kazi ile ambayo Mungu alifaa kuishughulikia duniani isingeweza kufanyika bila ya watu wa kushirikiana na Yeye, na wajibu uliotekelezwa na watumishi wa Mungu usingeweza kufanywa na wajumbe wa Mungu. Kila kazi ambayo Mungu alitoa amri kwa watumishi hawa ilikuwa yenye umuhimu mkubwa Kwake, na hivyo basi Asingeweza kuwapoteza. Bila ya ushirikiano wa watumishi hawa na Mungu, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingefikia kikomo, na matokeo yake ni kwamba mpango wa usimamizi wa Mungu na matumaini ya Mungu vyote visingewezekana.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp