Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 59

Ayubu Baada ya Majaribio Yake

Ayubu 42:7-9 Na basi ikawa, kwamba baada ya Yehova kusema maneno haya kwa Ayubu, Yehova akasema kwa Elifazi Mtemani, Ghadhabu yangu inawaka dhidi yako, na dhidi ya hao marafiki zako wawili: kwa sababu nyinyi hamjasema kunihusu kile kilicho sawa, jinsi alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkusema kunihusu kile kilicho sawa, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Hivyo Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi, wakaenda, na kufanya vile Yehova alivyowaamrisha: Yehova pia akamkubali Ayubu.

Ayubu 42:10 Naye Yehova akaubadilisha uteka wa Ayubu, wakati alipowaombea marafiki zake: Yehova pia akampa Ayubu kiasi kilichozidishwa mara mbili kuliko yale aliyokuwa nayo awali.

Ayubu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki Ayubu zaidi baadaye maishani kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Ayubu 42:17 Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku.

Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Duni na Mungu

Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawaje Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uamuzi wowote katika umuhimu wa Mungu ndani ya moyo wa Ayubu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mengi ya Mungu kwa “mtumishi wangu Ayubu” yanaonyesha ni vipi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawaje Mungu hakuongea kuhusu maana ya nyuma ya neno “Mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki cha maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “Ghadhabu yangu inawaka dhidi yako, na dhidi ya hao marafiki zako wawili: kwa sababu nyinyi hamjasema kunihusu kile kilicho sawa, jinsi alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo ya mara ya kwanza kwa Mungu kuambia watu waziwazi kwamba alikuwa amekubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake yeye, na ndiyo mara ya kwanza Alikuwa amethibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu alikuwa amefanya na kusema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwake Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na mabovu, kwa sababu, kama Ayubu wasingeweza kuona mwonekano wa Mungu au kusikia maneno aliyoongea katika maisha yao ilhali Ayubu alikuwa na maarifa sahihi Kumhusu Mungu, huku nao waliweza tu kukisia bila mpango kuhusu Mungu, kukiuka mapenzi ya Mungu na kujaribu uvumilivu wake kwa yote waliyoyafanya. Kwa hivyo, wakati sawa na kukubali yote yalikuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira zake kwa wale wengine, kwani ndani yao Hakuweza tu kuuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, lakini pia Hakusikia chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo Mungu kwa kilichofuata Alisema madai yafuatayo kuwahusu. “Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka zilizoteketezwa ili kusuluhisha makosa yao. Sadaka zilizoteketezwa mara nyingi zinatolewa kwa Mungu, lakini kile kisicho cha kawaida kuhusu sadaka hizi zilizoteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuwa nao ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Rafiki hawa wa Ayubu, nao walifichuliwa katika kipindi kile cha majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanafaa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka zilizoteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea wao ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na wa kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali vitendo vyao lakini Alikubali pakubwa na Alifurahishwa na Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunampandisha daraja binadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu ya hali hii, na anakuwa mdogo na mbaya mbele ya macho ya Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mielekeo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawaje Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, ndani ya macho ya Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuongea moja kwa moja na Mungu na kuwa na mgusano wa moja kwa moja na Mungu, hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko ya wale wengine. Haya ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama Mungu alivyoongea. Ayubu alipewa heshima hii maalum kwa sababu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine kutoitwa watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mielekeo hii miwili tofauti na maalum ya Mungu ndiyo mielekeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani mbele ya macho Yake, huku wale walio wapumbavu hawajamcha Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wadogo mbele ya macho ya Mungu.

Mungu Anamtawaza Ayubu Mamlaka

Ayubu aliwaombea rafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakushughulika nao kama walivyostahili juu ya upumbavu wao—Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na sababu ilikuwa nini? Kwa sababu kulingana na wao maombi yanayohusu mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu naye aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Wakati Mungu anapombariki mtu, Anampa tuzo nyingi, na si tu zile za kidunia: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwaambia kuwa wanastahili kuwaombea wengine, naye Mungu husahau na kusamehe makosa ya hao watu kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu—ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp