Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 62

Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza kisha kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya ambapo hakukuwa na binadamu …

Wakati Mungu aliinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisi, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza, Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi aliyefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—aliposimama mbele ya Mungu, aliyeumbwa kwa nyama na damu, aliye na mwili na umbo, na aliyeweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe huyu hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia lilimgusa na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe huyu hai aliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambayo Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, moyoni Mwake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.

Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.

Kisha, si kipindi kirefu baada ya Mungu kuwaumba binadamu, tunaona kutoka katika Biblia ya kwamba kulikuwa na gharika kubwa kote ulimwenguni. Nuhu anatajwa kwenye rekodi ya gharika, na inaweza kusemekana kwamba Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupokea mwito wa Mungu ili afanye kazi na Yeye ili kukamilisha kazi ya Mungu. Bila shaka, wakati huo ndio uliokuwa pia wa kwanza kwa Mungu kumwita mtu ulimwenguni kufanya kitu kulingana na amri Yake. Mara tu Nuhu alipokamilisha kuijenga safina, Mungu alileta gharika katika nchi kwa mara ya kwanza. Mungu alipoiharibu nchi kwa gharika, ndiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu kuviumba viumbe ambapo Alihisi kuzidiwa na maudhi kwa binadamu; hili ndilo lililomlazimu Mungu kufanya uamuzi wa uchungu wa kuharibu kizazi hiki cha binadamu kupitia kwa gharika. Baada ya gharika kuiharibu dunia, Mungu alifanya agano Lake la kwanza na binadamu kwamba Hatawahi kufanya hivi tena. Ishara ya agano hili ilikuwa upinde wa mvua. Hili ndilo lililokuwa agano la kwanza la Mungu na binadamu, hivyo basi upinde wa mvua ndio uliokuwa ishara ya kwanza ya agano lililotolewa na Mungu; upinde huu wa mvua ni jambo halisi lililopo. Ni kule kuwepo kabisa kwa upinde huu wa mvua ambako humfanya Mungu mara nyingi ahisi huzuni kutokana na kizazi cha binadamu cha awali ambacho Amepoteza, na huwa ni kumbusho la kila mara Kwake kuhusiana na kile kilichowafanyikia…. Mungu asingepunguza mwendo Wake—Asingesubiri kuchukua hatua ya kufuata katika usimamizi Wake. Hivyo basi, Mungu alimchagua Ibrahimu kama chaguo Lake la kwanza kwa kazi Yake kotekote Israeli. Hii ndiyo iliyokuwa pia mara ya kwanza kwa Mungu kumchagua mteuliwa kama huyo. Mungu aliamua kuanza kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa binadamu kupitia kwa mtu huyu, na kuendeleza kazi Yake miongoni mwa vizazi vya mtu huyu. Tunaweza kuona katika Biblia kwamba hivi ndivyo Mungu alivyomfanyia Ibrahimu. Basi Mungu akaifanya Israeli kuwa nchi ya kwanza iliyochaguliwa, na Akaianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria kupitia kwa watu Wake waliochaguliwa, Waisraeli. Tena kwa mara ya kwanza, Mungu aliwapa Waisraeli sheria na kanuni za moja kwa moja ambazo mwanadamu anafaa kufuata, na Akazieleza kwa kina. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpatia binadamu sheria kama hizo mahususi na wastani kuhusu namna wanavyofaa kutoa kafara, namna wanavyofaa kuishi, kile wanachofaa kufanya na kutofanya, ni sherehe na siku gani wanazofaa kutilia maanani, na kanuni za kufuata katika kila kitu walichofanya. Hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpa binadamu taratibu na kanuni hizo zenye maelezo na uwastani kwa ajili ya maisha yao.

Ninaposema “mara ya kwanza,” inamaanisha Mungu hakuwa Amewahi kukamilisha kazi kama hiyo tena. Ni kitu ambacho hakikuwepo awali, na hata ingawa Mungu alikuwa Amemuumba binadamu na Alikuwa ameumba aina zote za viumbe na vitu vyenye uhai, Hakuwa amewahi kukamilisha kazi ya aina hiyo. Usimamizi wa Mungu kwa binadamu; yote ilihusu binadamu na wokovu Wake na usimamizi wa binadamu. Baada ya Ibrahimu, Mungu alifanya chaguo tena kwa mara ya kwanza—Alimchagua Ayubu kuwa ndiye chini ya sheria ndiye ambaye angestahimili majaribio ya Shetani huku akiendelea kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na kuweza kumtolea Yeye ushuhuda. Hii pia ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kuruhusu Shetani kumjaribu mtu na mara ya kwanza Alipoweka dau na Shetani. Mwishowe, kwa mara ya kwanza, Mungu alimpata mtu aliyekuwa na uwezo wa kusimama kama shahidi Wake huku akiwa amemkabili Shetani—mtu ambaye angeweza kumshuhudia Yeye na kumwaibisha kabisa Shetani. Tangu Mungu alipomuumba mwanadamu, huyu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza, aliyempata ambaye aliweza kumshuhudia Yeye. Punde alipokuwa amempata mtu huyu, Mungu alikuwa na hata hamu zaidi ya kuendeleza usimamizi Wake na kuchukua hatua inayofuata katika kazi Yake, Akitayarisha chaguo Lake lifuatalo na mahali Pake pa kazi.

Baada ya kushiriki kuhusu haya yote, je, mnao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa binadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …

Baada ya kusikia haya yote leo, mnaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kawaida sana. Yaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani katikati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwasiliana na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa wazi moyoni mwake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira na mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja awali ni taarifa fulani tu kwa watu sasa na yaonekana kwamba hayana umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika mkondo wa kile ambacho utapitia kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kwa kadri maisha yako yanavyoendelea na pale ambapo pana msimamo kidogo wa Mungu katika moyo wako, au unapokuja kuelewa waziwazi na kwa kina mapenzi Yake, utaweza kuelewa kwa kweli umuhimu na haja ya kile Ninachozungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya na mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na makusudio Yake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Makusudio na fikira hizi vinawakilisha tabia ya Mungu, na vinaonyesha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Punde mtu anapoelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivi ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu ni vitu viwili visivyoteganishwa.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp