Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 64

Kama tunataka kuelewa bora zaidi kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa sehemu mpya ya kuanzia. Sehemu hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea awali ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote. Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa watu wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu aligeuka kuwa binadamu, mara ya kwanza Alianza kazi mpya kwa umbo la binadamu, Akiwa na utambulisho wa mwanamume. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote chini ya sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfano wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na sehemu mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza binadamu hadi katika enzi inayofuata.

Kama hii ilikuwa habari ya shangwe au ya kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana. Kwani tangu kuwepo na binadamu, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu kuonekana na kuishi miongoni mwa wanadamu katika umbo ambalo halikuwa Roho; badala yake, Alizaliwa na mwanadamu na kuishi miongoni mwa watu kama Mwana wa Adamu, na kufanya kazi katikati yao. Hii “mara ya kwanza” ilizivunja dhana za watu na pia ilikuwa zaidi ya kufikiria kote. Aidha, wafuasi wote wa Mungu walipata manufaa ya kushikika na kuonekana. Mungu hakuikomesha tu enzi nzee, lakini pia Alikomesha mbinu Zake za kale za kufanya kazi pamoja na mitindo ya kufanya kazi. Hakuruhusu tena wajumbe Wake kuwasilisha mapenzi Yake, na hakufichika tena katika mawingu na hakuonekana tena au kuongea kwa binadamu kupitia kwa ishara za amri kwa radi. Tofauti na chochote kile cha awali, kupitia kwa mbinu ambayo haikufirika kwa binadamu ambayo pia ilikuwa ngumu kwa wao kuelewa na kukubali—kupata mwili—Aligeuka na kuwa Mwana wa Adamu ili kuendeleza kazi ya enzi hiyo. Hatua hii iliwashangaza binadamu, na ikawa pia isiyo na utulivu kwao, kwa sababu Mungu kwa mara nyingine alikuwa ameanza kazi mpya ambayo Hakuwahi kufanya tena.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp