Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 82

Katika muda huu ambao Bwana Yesu alifanya kazi katika mwili, wengi wa wafuasi Wake wasingeweza kuthibitisha kikamilifu utambulisho Wake na mambo Aliyoyasema. Wakati aliposulubishwa msalabani, mwelekeo wa wafuasi Wake ulikuwa ule wa matarajio; aliposulubiwa msalabani na kupitishiwa yale yote aliyopitishiwa hadi alipowekwa katika kaburi, mwelekeo wa watu Kwake yeye ulikuwa wa kutoridhika. Wakati huu, watu walikuwa tayari wameanza kusonga katika mioyo yao kutoka katika kushuku hadi kukataa mambo ambayo Bwana Yesu alikuwa amesema wakati Akiwa mwili. Na Alipotembea nje ya kaburi na kujitokeza kwa watu mmoja baada ya mwengine, wengi wa watu ambao walikuwa wamemwona Yeye kwa macho yao au kusikia habari za kufufuka Kwake, walibadilika kwa utaratibu kutoka katika hali ya kumkataa hadi ile ya nadharia ya kushuku. Kufikia muda ule ambao Bwana Yesu alimfanya Tomaso kuuweka mkono wake katika upande Wake, kufikia wakati ambao Bwana Yesu aliuvunja mkate na kuula mbele ya umati wa watu baada ya kufufuka Kwake na baada yake kula kipade cha samaki aliyechemshwa mbele yao, hapo tu ndipo walipokubali kwa kweli Bwana Yesu ni Kristo katika mwili. Mnaweza kusema kwamba ni kana kwamba mwili huu wa kiroho ulio na nyama na damu uliosimama mbele ya hao watu ulikuwa ukizindua kila mmoja wao kutoka katika ndoto. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Ndiye aliyekuwepo tangu miaka hiyo ya nyuma. Alikuwa na umbo, na mwili, na mifupa, na Alikuwa tayari ameishi na kula na wanadamu kwa muda mrefu…. Wakati huu, watu walihisi kwamba uwepo Wake ulikuwa halisi, wa ajabu sana; wote walichangamka na kufurahi mno, na wakati uo huo walijawa na hisia. Na kuonekana Kwake tena kuliwaruhusu watu waweze kuona kwa kweli unyenyekevu Wake, kuhisi ukaribu Wake na tamanio Lake, uhusiano Wake wa karibu na wanadamu. Kupatana huku kwa kufupi kuliwafanya watu waliomwona Bwana Yesu kuhisi kana kwamba muda mrefu umepita. Mioyo yao iliyopotea, kuchanganyikiwa, yenye woga, yenye wasiwasi, inayotarajia na isiyosikia hisia zozote vyote vilipata utulivu. Hawakuwa na shaka tena au kutoridhika tena kwa sababu walihisi kwamba sasa kulikuwa na tumaini na kitu cha kutegemea. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Angekuwa nao milele, Angekuwa mnara wao dhabiti, kimbilio lao la kila wakati.

Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue yafuatayo: Maisha yao ulimwenguni hawapo pekee. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumwegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumwegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawataishia katika dhambi tena. Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake zilikuwa chache mno lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito.

Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la mwili. Alikuwa mjumbe wa Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Akaipatia nguvu na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema. Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Yeye humaliza kazi Anayoianza. Kunazo hatua na mpango, na umejaa hekima ya Mungu, kudura Yake, na matendo Yake ya ajabu. Umejaa pia upendo na rehema za Mungu. Bila shaka, uzi mkuu unaotiririka katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika aya hizi za Biblia, katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Mpaka sasa hakuna chochote kati ya hivi vyote ambacho kimebadilika—unaweza kukiona? Unapoviona hivi, moyo wako haugeuki bila kusukumwa na kuwa karibu na Mungu? Kama uliishi katika enzi hiyo na Bwana Yesu Akakuonekania baada ya kufufuka Kwake, kwa njia ya kushikika ili wewe uweze kuona, na kama Aliketi mbele yako, Akala mkate na samaki na kukuchambulia wewe maandiko, Akaongea na wewe, basi ungehisi vipi? Ungehisi furaha? Je, ungehisi kuwa mwenye hatia? Kutoelewana kwa awali na kuepuka Mungu kwa awali, migogoro na shaka dhidi ya Mungu—hivi vyote havingetoweka tu? Je, unadhani kwamba uhusiano kati ya binadamu na Mungu ungekuwa bora zaidi?

Kupitia kwa ufasiri wa sura hizi finyu za Biblia, uligundua makosa yoyote katika tabia ya Mungu? Uligundua uchafuzi wowote katika upendo wa Mungu? Uliuona udanganyifu au uovu wowote katika kudura ya Mungu au hekima? Bila shaka la! Sasa unaweza kusema kwa uhakika kwamba Mungu ni mtakatifu? Unaweza kusema kwa uhakika kwamba hisia za Mungu zinafichua kiini Chake na tabia kwa ujumla? Natumai kwamba baada ya kuyasoma maneno haya, kile ambacho umeelewa kutoka katika maneno haya kitakusaidia na kukufaidi katika ufuatiliaji wako wa mabadiliko katika tabia na hali ya kumcha Mungu. Natumai pia kwamba maneno haya yataweza kukuzalia matunda ambayo yatakua kila siku, hivyo basi katika mchakato wa ufuatiliaji huu kukuleta karibu na Mungu zaidi na zaidi, wa kukuleta karibu na karibu zaidi na kiwango ambacho Mungu anahitaji, ili usichoke tena na ufuatiliaji wa ukweli na usihisi tena kwamba ufuataji wa ukweli na ule wa mabadiliko katika tabia ni usumbufu au jambo duni. Ni, kwa kweli, udhihirisho wa tabia ya kweli ya Mungu na kiini kitakatifu cha Mungu ambayo yanakupa motisha kutamani mwangaza, kutamani haki, na kuazimia kufuatilia ukweli, kufuatilia ridhaa ya mapenzi ya Mungu, na kuwa binadamu anayepatwa na Mungu, na kuwa mtu halisi.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp