Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 84

Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana

“Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo” (Mwa 1:6-7). Ni mabadiliko gani yaliyofanyika baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji”? Maandiko yanasema: “Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu.” Ni nini kilichokuwa matokeo baada ya Mungu kutamka hivi na kufanya hivyo? Jibu linapatikana kwenye sehemu ya mwisho ya fungu hili: “na kukawa vivyo hivyo.”

Sentensi hizi fupi mbili zinarekodi tukio la kupendeza, na zinafafanua mazingira mazuri—utekelezaji wa kipekee ambapo Mungu aliyatawala maji, na kuunda anga ambayo binadamu angeishi…

Katika picha hii, maji na anga vinaonekana mbele ya macho ya Mungu papo hapo, na vyote vinagawanywa kwa mamlaka ya matamshi ya Mungu, na kugawanywa kwa sehemu ya juu na ya chini kwa njia ambayo iliteuliwa na Mungu. Hivi ni kusema, anga iliyoumbwa na Mungu haikufunika tu maji yaliyo chini, lakini pia ilishikilia maji yaliyo juu… Katika haya, binadamu hawezi kufanya chochote ila kukodoa macho, kushangaa, na kutweta kwa kuvutiwa na maajabu ya onyesho hilo ambalo Muumba aliyahamisha maji, na kuyaamuru maji, na kuumba anga, na yote haya Alifanya kupitia kwa nguvu za mamlaka Yake. Kupitia kwa matamshi ya Mungu, na nguvu za Mungu, na mamlaka ya Mungu, Mungu aliweza kutimiza tendo jingine kubwa. Je, hizi si nguvu za mamlaka ya Muumba? Hebu na tutumie maandiko haya katika kufafanua vitendo vya Mungu: Mungu aliyatamka matamshi Yake na kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu kulikuwa na anga katikati ya maji. Wakati uo huo, badiliko la ajabu lilitokea kwenye nafasi hii kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu, na halikuwa badiliko katika hali ya kawaida, lakini aina fulani ya kibadala ambapo kitu kisichokuwepo kiligeuka na kuwa kitu kilichopo. Yote haya yalizaliwa kwenye fikira za Muumba, na yakawa kitu kilichopo kutoka kwenye kitu kisichokuwepo kwa sababu ya matamshi yaliyotamkwa na Muumba, na, vilevile, kuanzia sasa kwenda mbele yangekuwepo na kuwa imara, kwa minajili ya Muumba, na yangesonga, kubadilika, na kupata nguvu kulingana na fikira za Muumba. Ufahamu huu unafafanua kitendo cha pili cha Muumba katika viumbe Vyake vya ulimwengu mzima. Yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka na nguvu za Muumba, na ulikuwa utekelezaji mwingine anzilishi uliofanywa na Muumba. Siku hii ndiyo iliyokuwa siku ya pili ambayo Muumba alikuwa amepitisha tangu kuwekwa msingi kwa ulimwengu, na ilikuwa siku nyingine nzuri Kwake: Alitembea miongoni mwa nuru, Aliileta anga, Aliyapangilia na kuyatawala maji, na vitendo Vyake, mamlaka Yake, na nguvu Zake vyote viliweza kuanza kazi kwenye siku hiyo mpya…

Je, kulikuwepo na anga katikati ya maji kabla ya Mungu kutamka matamshi Yake? Bila shaka la! Na je, baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji”? Viumbe vilivyonuiwa na Mungu vilionekana; kulikuwa na anga katikati ya maji, na maji yaligawanywa kwa sababu Mungu alisema hivyo “na uigawanye maji kutoka kwa maji.” Kwa njia hii, kufuatia maneno ya Mungu, viumbe vipya viwili, viumbe viwili vilivyozaliwa na vilivyokuwa vipya vilionekana miongoni mwa viumbe vyote kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Na unahisi vipi kuhusu kujitokeza kwa viumbe hivi viwili vipya? Je, unahisi ukubwa wa nguvu za Muumba? Unahisi ile nguvu ya kipekee na isiyo ya kawaida ya Muumba? Ukubwa wa msukumo na nguvu kama hizo unatokana na mamlaka ya Mungu na mamlaka haya ni kiwakilishi cha Mungu Mwenyewe, na sifa ya kipekee ya Mungu Mwenyewe.

Je, ufahamu huu umekupa mtazamo mwingine kamilifu wa upekee wa Mungu? Lakini haya ni machache tu kati ya mengi; mamlaka na nguvu za Muumba vinazidi haya yote. Upekee wake hauko hivyo tu kwa sababu Anamiliki hali halisi isiyo kama ya viumbe vingine, lakini pia kwa sababu ya mamlaka na nguvu Zake kuwa zisizo za kawaida, zisizo na mipaka, bora kabisa kuliko vyote, na inapita vitu vyote, na vilevile, kwa sababu mamlaka Yake na kile Anacho na alicho kinaweza kuumba maisha, na kufanya miujiza, na Anaweza kuumba kila mojawapo ya dakika na sekunde iliyo ya kustaajabisha na isiyo ya kawaida, na wakati uo huo, Anaweza kutawala maisha Anayoyaumba na kushikilia ukuu Wake juu ya miujiza na kila mojawapo ya dakika na sekunde Anazoumba.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp