Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 88

Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine

Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….

“Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri” (Mwa 1:24-25). Viumbe hai gani ndivyo vinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: ng’ombe, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai kwenye nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.”

Kama tu kwenye siku zile tano za awali, na kwa sauti sawa, kwenye siku ya sita Muumba akashurutisha kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na vikajitokeza kwenye nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anapotekeleza mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure bilashi, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kikajitokeza wakati ule Aliochagua. Muumba aliposema “Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake,” nchi ilijawa mara moja na maisha, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Kwenye jangwa lenye nyasi za kijani, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwengine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kurukaruka…. Mara moja, nchi pana tambarare yenye utulivu ikajaa uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali kulikuwa mandhari ya kupendeza kwenye nchi ile tambarare iliyotulia, na kujitokeza huko kukaleta nguvu zisizo na mipaka…. Wangekuwa wenza wa nchi ile tambarare, na wenyeji wakuu wa nchi ile tambarare, kila mmoja akitegemea mwengine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha ukuzwaji wa milele kwa minajili ya kuwepo kwao …

Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwengine. Hata ingawaje ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka juu kwa juu, wengine wakapepesuka; wengine walichimba wakienda mbele, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine wakaruka juu na chini…. Wote walishughulika kwa kujaribu kujitafutia makao: Baadhi walisukumana na kujipata kwenye nyasi, baadhi walianza kuyachimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, wakiwa wamejificha kwenye msitu…. Ingawaje walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusita kupumzika, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kolevu cha kumetameta yaliwapa mlo wenye utomvu mwingi…. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakusita kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walimilikiwa na nishati ya ajabu pamoja na uchangamfu usio na mipaka, na kwa viumbe vyote wao ndio walikuwa amilifu zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya kazi na wakafanyiza miili yao bidii kwa minajili ya siku zao za usoni, wakiwa wamejishughulisha na kukimbia hapa na pale kwa minajili ya kesho yao ili waweze kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila inchi ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na wakitumia mkondo wao binafsi maalum wa maisha, waliweka alama katika viumbe vyote, na baadaye wakaacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchanga, nyasi, na misitu, na walipatia mchanga nguvu na uthabiti, vivyo hivyo kwenye nyasi, na misitu na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …

Mtazamo wa Muumba ulienea kotekote kwenye viumbe vyote ambavyo Alikuwa ameumba na wakati huu kwa muda huo macho Yake yalitulizia misitu na milima, akili Yake ikigeuka. Huku matamshi Yake yakitamkwa wazi kwenye misitu mingi, na juu ya milima, kulionekana aina ya viumbe fulani vilivyokuwa tofauti na vyovyote vile vilivyokuwa vimekuja hapo awali: Walikuwa wanyama wa mwitu waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Walikuwa wamepitiliza muda mrefu ajabu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, huku kila mmoja wao akiwa na uso wake pekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa wamejikinga, baadhi yao walikuwa na meno ya sumu, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo-ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho—mapana, baadhi walikuwa na mtazamo wa woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakidundadunda kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakirukaruka kwa kwato nne, baadhi walikuwa wakiangalia mbele juu ya mti, baadhi walikuwa wamejilalia tu wakisubiria misituni, baadhi walikuwa wakitafuta vyumba vya chini kwa chini ili kupumzika, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kuonyesha furaha ya kipekee kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi walikuwa wakibweka, baadhi walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti nyororo, baadhi walikuwa na sauti ya kati, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti safi na yenye mdundo wa kimuziki…; baadhi walikuwa wa kuogofya, na baadhi walikuwa warembo, na baadhi walikuwa wakitisha, baadhi walikuwa wa kuvutia, baadhi walikuwa wa kutishia, baadhi walikuwa wasio na hatia ila wachangamfu…. Mmoja baada ya mwengine, wote walikuja. Tazama namna walivyotembea, kwenye uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda kutazamana…. Kila mmoja akiwa na maisha fulani waliyopewa na Muumba, na umwitu wao binafsi, na ukatili, walionekana kwenye misitu na pia juu ya milima. Viumbe vya kudharauliwa kati ya vyote, na vyenye kuamrisha kabisa—ni nani aliyewafanya kuwa mabingwa wa kweli wa milimani na misituni? Kutoka muda ambao Kuonekna kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kuweka madai” hayo katika misitu, na “kuweka madai” kwenye milima, kwani Muumba alikuwa tayari amepangilia mipaka yao na Akaamua upana wa uwepo wao. Hawa ndio waliokuwa mabwana wa kweli wa milimani na misitu, na ndiyo maana walikuwa na umwitu mwingi na kwa hivyo wenye dharau. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wasiowezekana, wenye unyama, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Na ilikuwa kwa sababu waliishi umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na mwanadamu ndiposa waliweza kutimiza wajibu wao waliopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule umwitu wao uliilinda milima na kulinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la uwepo wao na utekelezaji wao. Wakati uo huo, umwitu wao uliendeleza na kuhakikisha usawazisho miongoni mwa viumbe vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na ukitaji mizizi kwenye milima na misitu; kuingia kwao kuliweza kuingiza nguvu na uthabiti zaidi kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia hapa kwenda mbele, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu kule kusihiwa na Muumba ili waweze kushikilia eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kuendeleza usawazisho wa viumbe vyote vilivyoanzishwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp