Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 101

Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, mtu yeyote anaweza kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya machipuko, kiangazi, mapukutiko na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti huweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika mapukutiko inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha dhana moja ya mamlaka ya Mungu? Mungu alisema “Iwe Nuru,” na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa ajili ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha hali yao halisi na kazi? Kuna yeyote anayeweza kutibua mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, Shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—na ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, au sio? Kuna yeyote anayeweza kumfanya simba kulima ardhi kama afanyavyo ng’ombe? Je, yupo yeyote anayeweza kubadilisha ndovu kuwa punda? Je, yupo anayeweza kubadilisha kuku akapaa hewani kama tai? Je, yupo anayeweza kumfanya mbwamwitu kula nyasi kama kondoo? Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Na kwa nini hamna? Kwa sababu Mungu aliwaamuru kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka vipimo vya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na kipimo cha kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kupitishwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi jangwani, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ngo’mbe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawaje ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, ni aina tofauti, kwani waligawanywa kwenye aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawaje kuku ana miguu miwili, na mbawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.

Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemekana kwamba inanawiri, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kukua mkubwa zaidi, lakini kunao ushindi mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vibebaji vya ndege, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu ya teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwake na mzunguko wa maisha na kifo wa kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemekane kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kunazo bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliwekea mipaka kila mojawapo ya bahari hizo; zilikaa popote pale Aliziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kusongasonga ovyo. Bila ya ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia ni suala na uamuzi wa mamlaka ya Mungu.

Ili kuweka wazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” yanamaanisha kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni wajibu wa Mungu, na wala si wajibu wa binadamu; na wala haiwezi kubadilishwa na binadamu. Haiwezi kusongeshwa kwa mapenzi ya binadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na hii ni kweli ambayo haiwezi kukataliwa na binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, ile inayoonekana na isiyoonekana kwa binadamu—yote haya yapo, yanafanya kazi, na kubadilika, bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na shurutisho za Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Si hata mtu mmoja au kifaa kimoja kinaweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na ishara ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Yanaweza kuigwa, kughushiwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp