Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 106

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na hawakula. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mkono wao, na kumvuta Lutu katika nyumba walikokuwa, na kuufunga mlango. Na wakawagonga wale watu waliokuwa katika mlango wa nyumba na upofu, wakubwa na wadogo: kiasi kwamba walijichosha kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Kutoka katika mtazamo wa binadamu, Sodoma ulikuwa ni mji ulioweza kutosheleza kikamilifu matamanio ya binadamu na maovu ya binadamu. Ulivutia na uliduwaza, kwa muziki na densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume kufurahia na kuruka kichwa. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na yakawaduwaza hadi kuzoroteka. Huu ulikuwa mji uliokuwa na roho chafu na roho za Shetani zilicharuka hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda dhambi zisizohesabika za ukinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.

Ingawaje mafungu haya mawili hayarekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, ukweli mtupu unaweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, walijaa maovu na walimpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wakatili kwa uwepo wa Mungu, kuja Kwake, adhabu Yake, na hata zaidi, maonyo Yake. Hawakuona chochote kingine chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu uliofichuliwa kwa kweli ulionekana tu kuwa mdogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, sunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha baada ya kifo au roho kuwa mwilini mwao; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika binadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Wakati ule moto ambao Mungu alituma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungesita kuwepo, na vilevile kila kitu ndani ya mji wenyewe. Uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na adhama ya Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la kutowahi kuutazamia mji huo tena” la Mungu ni hasira Yake, pamoja na adhama Yake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo tena. Baada ya mji huo kuacha kuchomeka, huku ukiwa umeacha nyuma jivu pekee, ulikuwa kwa kweli umesita kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma kwa jumla na watu waliokuwa wamejaa dhambi ndani yake, wala kuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji uliokuwa umepatwa na dosari ya dhambi; hata zaidi, moto huu uliangamiza kumbukumbu za maovu na ukinzani wa binadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudio la Mungu kwa kuuchoma ule mji.

Binadamu ulikuwa umepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na kukufuru. Hata wakati watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba; vilevile hawakuacha mwenendo wao wa maovu. Kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na hali yao halisi ya uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba ukinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potovu, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la matusi au kejeli iliyotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingeongeza hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haifai kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliotiririka na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alipenda kuwaondoa watu waliokuwa ndani yake na uzima wa dhambi zao kwa njia kamilifu zaidi, kuwafanya watu hawa wa mji kusita kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa kuongezeka. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kusita kuwepo.”

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp