Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 116

Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi

Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko haya kati ya dhana hizi mbili za tabia ya Mungu kwenye suala lili hili yalikuruhusu kuweza kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili na wazi; haijagawanywa hata kidogo. Licha ya kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au chombo kilichofinyangwa kwa udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe mwenye uhai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa sababu ya watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Aliweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi mkosi na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupendelea kutumia sheria bila kumakinika na wanapendelea kutumia sheria ili kuthibitisha na kufafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia fomula ili kujua tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kulingana na himaya ya fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika mara moja kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, dhana tofauti za hali halisi ya Mungu zitaweza kufichuliwa. Kwenye kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye hufichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, upole wa upendo Wake na uvumilivu Wake. Hali hii halisi Yake itafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia yake ya haki hairuhusiwi kushukiwa, kukiukwa, kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi dhana hizi katika kila elementi ya asili na kuzitekeleza kila wakati. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka ya muda au nafasi, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kama inavyoongozwa na mipaka ya muda au nafasi. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kusita kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inayo maneno matupu tu. Wakati Mungu anapoonyesha hasira Yake na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina kosa. Moyo wa Mungu unavutiwa na kutubu kwa watu, na ni kutubu huku ambako hubadilisha moyo Wake. Kuvutiwa kwake, mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote kwa kweli havina kosa kamwe; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu kwa kweli ni uvumilivu; Huruma Yake ni huruma bila kasoro. Tabia yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; hali Yake halisi ni tofauti na chochote kile katika uumbaji. Kanuni za matendo ambayo Mungu anaonyesha, fikira na mawazo Yake, au uamuzi wowote ule, pamoja na kitendo chochote kimoja, vyote havina dosari wala doa. Kama vile Mungu alivyoamua, ndivyo Atakavyotenda, na katika njia hii, Yeye hukamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe chochote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kujitokeza na kuendeleza utekelezaji na uzoefu.

Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, unauona upande ule mwingine wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu? Je, unauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwenu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha hasira nyingi na kuamua kuangamiza au kuleta maafa kwa mwanadamu? Na ni nani amefuzu kutoa huruma, na kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake dhidi ya kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za binafsi za kipekee; Hategemei kudhibitiwa au kuzuiliwa na watu, matukio au mambo yoyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi yeye na kubadilisha uamuzi wowote Wake. Uzima wa tabia na fikira za uumbaji upo katika hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama ataendeleza hasira au huruma; ni hali halisi tu ya Muumba—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hivi. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!

Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni dhana ya hali halisi ya tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua dhana mbili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa na vilevile kushukiwa; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyokosewa; wakati uo huo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, vinavyoweza kubadilisha au kuwakilisha Mungu katika vitendo Vyake, wala hakuna yeyote anayeweza kubadilisha au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp