Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 125

Ndoa: Awamu ya Nne

Wakati mtu anavyokua mzee na kukomaa, mtu huanza kukua na kuwa mbali na wazazi wake na mazingira ambayo amezaliwa na kulelewa, na badala yake mtu huanza kutafuta mwelekeo wa maisha yake na kufuatilia shabaha binafsi kwa njia ya maisha iliyo tofauti na ile ya wazazi. Kwenye kipindi hiki cha muda mtu hahitaji tena wazazi wake, bali mwandani ambaye anaweza kuishi maisha yake na mtu huyo: mwenza, mtu ambaye hatima yake imejipinda kwake ndani kwa ndani. Kwa njia hii, tukio kuu ambalo mtu hukabiliana nalo kufuatia uhuru wake ni ndoa, awamu ya nne ambayo lazima mtu apitie.

1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa

Ndoa ni tukio muhimu katika maisha ya mtu yeyote; ni wakati ule ambao mtu huanza kwa kweli kuendeleza aina mbalimbali za majukumu, huanza kwa utaratibu kutimiza aina mbalimbali za kazi maalum. Watu huwa na picha nyingi kuhusu ndoa kabla ya kuipitia wao wenyewe, na picha hizi zote ni nzuri. Wanawake hufikiria kwamba waume wao watakuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, nao wanaume hufikiria kwamba wataweza kuoa Binti wa Kifalme Anayependeza. Kubuni huku kwa mawazo kunaonyesha kwamba kila mtu anayo mahitaji fulani ya ndoa, orodha fulani ya kile anachohitaji na viwango anavyopenda. Ingawaje katika enzi hii ya maovu watu wanaambiwa kila mara kuhusu ujumbe uliopotoka juu ya ndoa, hali ambayo husababisha hata mahitaji mengi zaidi, pamoja na kupatia watu aina zote za mizigo na mitazamo isiyo ya kawaida, mtu yeyote aliyepitia ndoa anajua kwamba haijalishi ni kiasi kipi ambacho mtu ataielewa, haijalishi pia mtu anao mtazamo gani katika ndoa hiyo, ndoa si suala la chaguo la mtu binafsi.

Mtu hukumbana na watu wengi katika maisha yake, lakini hakuna anayejua ni nani atakayekuwa mwandani wake katika ndoa. Ingawaje kila mtu anazo fikira zake binafsi na mtazamo wake wa kibinafsi kuhusu suala la ndoa, hakuna anayeweza kuona mbele na kujua ni nani atakayekuwa mwandani wake wa kweli hatimaye, na fikira za mtu huwa zinachangia kidogo sana. Baada ya kukutana na mtu unayempenda, unaweza kumfuatilia mtu huyo; kama mtu huyo amevutiwa na wewe au la, kama mtu huyo anaweza kuwa mwandani wako au la, si wewe kuamua. Kiini cha mahaba yenu si haswa mtu ambaye mtaweza kuishi naye katika maisha yako; na huku haya yakiendelea mtu ambaye hukuwahi kutarajia anaingia katika maisha yako na kuwa mwandani wako, anakuwa msingi muhimu sana katika hatima yako, nusu yako ile nyingine, ambaye hatima yako imefungamanishwa naye ajabu. Na kwa hiyo, ingawaje kunazo ndoa milioni kwa milioni ulimwenguni, kila ndoa ni tofauti: Ni ndoa ngapi ambazo hazitoshelezi, ni ngapi zinayo furaha; ni ngapi zinazopatikana Mashariki na Magharibi, ni ngapi Kaskazini na Kusini; ni ngapi ambazo wanandoa wanafaa na wamelingana, na ni ngapi zenye kiwango sawa; ni ngapi zenye furaha na utulivu, ni ngapi zenye maumivu na huzuni; ni ngapi zinaonewa wivu na wengine, na ni ngapi hazieleweki na hazipendelewi kabisa; ni ngapi zimejaa furaha, na ni ngapi zimejaa machozi na zinakatisha tamaa…. Kwenye ndoa hizi zote, binadamu wanafichua utiifu na kujitolea kwa maisha katika ndoa hizo, au pendo, au mtagusano, na hali ya kutotenganishwa, au kukata tamaa na kutoeleweka, au usaliti, au hata chuki. Haijalishi kama ndoa inaleta furaha au maumivu, kazi maalum ya kila mmoja katika ndoa iliamuliwa kabla na Muumba na haitabadilika; kila mmoja lazima aitimize. Na hatima ya kibinafsi inayokuwa katika kila ndoa haibadiliki; iliamuliwa kitambo naye Muumba.

2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili

Ndoa ni awamu muhimu katika maisha ya mtu. Ni zao la hatima ya mtu, kiungo muhimu katika hatima ya mtu; haiundwi kwa misingi ya uamuzi wa mtu yeyote binafsi au mapendeleo yake, na haiathiriwi na mambo yoyote ya nje, lakini inaamuliwa kabisa na hatima za wandani wawili, kupitia kwa maandalizi na kuamuliwa kabla kwa Muumba kuhusiana na hatima za wanandoa hao. Ukiangalia juujuu, kusudi la ndoa ni kuendeleza kizazi cha binadamu, lakini kwa kweli ndoa si chochote ila ni kawaida ya dini ambayo mtu anapitia katika mchakato wa kutimiza kazi yake maalum. Wajibu mbalimbali ambao watu huendeleza katika ndoa si ule tu wa kuleta kizazi kinachofuata; kunao wajibu mbalimbali ambao mtu huwa nao na kazi maalum ambazo mtu lazima atimize kwenye mkondo wa kuendeleza ndoa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu huathiri mabadiliko ya watu, matukio, na mambo yanayomzunguka, ndoa ya mtu itaweza pia kuathiri bila shaka watu hao, na zaidi itawabadilisha kwa njia tofauti.

Wakati mtu anapokuwa huru, mtu huanza safari yake binafsi ya maisha, inayoongoza mtu hatua kwa hatua kuelekea kwa watu, na kwa matukio, na kwa vitu vinavyohusiana na ndoa ya mtu; na wakati uo huo, yule mtu mwengine atakayeunda ile ndoa anakaribia, hatua kwa hatua, kuelekea watu ao hao, matukio na hata mambo. Kwenye ukuu wa Muumba, watu wawili wasiohusiana walio na hatima inayohusiana wanaingia kwa utaratibu kwenye ndoa na kuwa, kimiujiza, familia, “nzige wawili wanaoshikilia kamba moja.” Kwa hivyo mtu anapoingia kwenye ndoa, safari ya mtu katika maisha itaathiri na kumgusa yule mwenzake, na vilevile safari ya mwandani katika maisha itashawishi na kugusa hatima ya yule mwenzake katika maisha. Kwa maneno mengine, hatima za mwanadamu zimeingiliana na hakuna yule anayeweza kutimiza kazi yake maalum maishani au kutekeleza wajibu wake kabisa akiwa huru mbali na wengine. Kuzaliwa kwa mtu kunao mwelekeo kwa msururu mkubwa wa mahusiano; kukua pia kunahusisha msururu mkubwa wa mahusiano; na vilevile, ndoa inakuwepo bila shaka na kuendelezwa katika mtandao mpana na mgumu wa miunganisho ya binadamu, ikihusisha kila mwanachama na kuathiri hatima ya kila mmoja ambaye ni sehemu yake. Ndoa si mazao ya familia za wanachama wale wawili, hali ambazo wao walilelewa, maumbo yao, umri wao, ubora wao, vipaji vyao, au mambo mengine yoyote; badala yake, inatokana na kazi maalum ya pamoja na hatima inayohusiana. Hii ndiyo asili ya ndoa, zao la hatima ya binadamu lililopangwa na lililopangiliwa na Muumba.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp