Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 126

Uzao: Awamu ya Tano

Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.

Kama mtu amezaliwa ili kutimiza jukumu la mtoto wa mwengine, basi mtu analea kizazi kijacho ili kutimiza jukumu la mzazi wa mwengine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamfanya mtu kupitia awamu tofauti za maisha kutoka mitazamo tofauti. Yanampa pia mtu mseto tofauti wa mambo mbalimbali ya maisha kupitia, ambapo mtu anajua ukuu ule wa Muumba, pamoja na hoja kwamba hakuna mtu anayeweza kuzidi au kubadilisha kile ambacho Muumba aliamua kabla.

1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake

Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbile yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi. Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni. Lakini wakati wa watu kulea kizazi kijacho unapowadia, wataweza kuweka matamanio yao yote ambayo hayajatimizwa katika nusu ya kwanza ya maisha yao kwenye vizazi vyao, wakitumai kwamba, uzao wao utajaliza sehemu ile ambayo wao wamepitia masikitiko, kwenye nusu ile ya kwanza ya maisha yao. Kwa hivyo watu hujihusisha katika aina zote za fantasia kuhusu watoto wao: kwamba binti zao watakua na kuwa warembo ajabu, watoto wao wa kiume watakuwa wanaume wa kipekee; kwamba binti zao watakuwa na maadili na wenye vipaji nao watoto wao wa kiume watakuwa wanafunzi werevu, na wanariadha sifika; na kwamba binti zao watakuwa watulivu na waadilifu, wenye akili razini, kwamba watoto wao wa kiume watakuwa wenye akili, wenye uwezo na wanaojali. Wanatumai kwamba wawe watoto wa kike au wa kiume wataheshimu wazee wao, watajali wazazi wao, watapendwa na kusifiwa na kila mmoja…. Kufikia hapa matumaini ya maisha yanajitokeza upya, na matamanio mapya yanapata nguvu katika mioyo ya watu. Watu wanajua kwamba hawana nguvu na tumaini katika maisha haya, kwamba hawatakuwa na fursa nyingine, tumaini jingine, la kujitokeza mbele ya watu, na kwamba hawana chaguo lolote ila kukubali hatima zao. Na kwa hivyo wanatazamia matumaini yao yote, matamanio na maadili yao ambayo hayajatimizwa, hadi kwenye kizazi kijacho, wakitumai uzao wao unaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kutambua matamanio yao; na kwamba binti zao na watoto wao wa kiume wataleta utukufu katika jina la familia, kuwa muhimu, kuwa matajiri au maarufu; kwa ufupi, wanataka kuuona utajiri wa watoto wao ukizidi na kuzidi. Mipango na fantasia za watu ni timilifu; kwani hawajui kwamba idadi ya watoto walio nayo, umbo, uwezo na kadhalika wa watoto wao, si juu yao kuamua, kwamba hatima za watoto wao hazimo kamwe katika viganja vya mikono yao? Binadamu si waendeshaji wa hatima yao binafsi, ilhali wanatumai kubadilisha hatima ya kizazi kichanga zaidi; hawana nguvu za kutoroka hatima zao wenyewe, ilhali, wanajaribu kudhibiti zile za watoto wao wa kiume na kike. Je, hawazidishi ukadiriaji wao? Je, huu si ujinga na hali ya kutojua kwa upande wa binadamu? Watu huenda kwa mapana yoyote kwa minajili ya uzao wao, lakini hatimaye, idadi ya watoto aliyonayo mtu, na vile ambavyo watoto wake walivyo, si jibu la mipango na matamanio yao. Baadhi ya watu hawana hela lakini wanazaa watoto wengi; baadhi ya watu ni tajiri ilhali hawana mtoto. Baadhi wanataka binti lakini wananyimwa tamanio hilo; baadhi wanataka mtoto wa kiume lakini wanashindwa kuzaa mtoto wa kiume. Kwa baadhi, watoto ni baraka; kwa wengine, mtoto ni laana. Baadhi ya wanandoa ni werevu, ilhali wanawazaa watoto wanaoelewa polepole; baadhi ya wazazi ni wenye bidii na waaminifu, ilhali watoto wanaowalea ni wavivu. Baadhi ya wazazi ni wapole na wanyofu lakini wana watoto wanaogeuka na kuwa wajanja na wenye inda. Baadhi ya wazazi wana akili na mwili timamu lakini wanajifungua watoto walemavu. Baadhi ya wazazi ni wa kawaida na hawajafanikiwa ilhali watoto wao wanafanikiwa pakubwa. Baadhi ya wazazi ni wa hadhi ya chini ilhali watoto wanaowalea ni wenye taadhima. …

2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao

Watu wengi wanaooa hufanya hivyo karibu kwenye umri wa miaka thelathini, na kwa wakati huu wa maisha, mtu hana ufahamu wowote wa hatima ya binadamu. Lakini wakati watu wanapoanza kulea watoto, kwa kadri uzao wao unapokua, wanatazama kizazi kipya kikirudia maisha na hali zote walizopitia katika kizazi cha awali, na wanaona maisha yao ya kale yakijionyesha kwao na wanatambua kwamba barabara inayotumiwa na kizazi kile kichanga zaidi, kama tu yao, haiwezi kupangwa wala kuchaguliwa. Wakiwa wamekabiliwa na hoja hii, hawana chaguo lolote bali kukubali kwamba hatima ya kila mtu iliamuliwa kabla; na bila ya hata kutambua wanaanza kwa utaratibu kuweka pembeni matamanio yao binafsi, na hisia kali katika mioyo yao inapungua na kuwatoka…. Kwenye kipindi hiki cha muda, mtu ameweza kupita sehemu nyingi zaidi na muhimu katika mafanikio ya maisha yake na ametimiza ufahamu mpya wa maisha, na kuchukua mtazamo mpya. Je, mtu wa umri huu anaweza kutarajia kwa siku za usoni kiasi kipi cha mambo na matarajio yake ni yapi? Ni mwanamke yupi mwenye umri wa miaka hamsini angali anaota kuhusu Kaka Mwenye Mvuto na Haiba? Ni mwanamume yupi wa miaka hamsini angali anatafuta Binti wa Kifalme Anayependeza? Ni mwanamke yupi wa umri wa kati atakuwa anatumai kugeuka kutoka kwa mtoto wa bata mwenye sura mbaya hadi batamaji? Je, wanaume wazee zaidi wangali wana msukumo sawa wa ajira na wanaume wachanga? Kwa ujumla, haijalishi kama mtu ni mwanamume au mwanamke, yeyote anayeishi na kuufikia umri huu anao uwezekano wa kuwa na mtazamo wa kueleweka na kutumika kiasi fulani katika ndoa, familia, na watoto. Mtu kama huyo, kimsingi hana chaguo zozote zilizobakia, hana msukumo wowote wa kukabiliana na hatima yake. Kwa mujibu wa kile ambacho binadamu amepitia, punde tu mtu anapofikia umri huu mtu huanza kwa kawaida kuwa na mtazamo kwamba “lazima mtu akubali hatima yake; watoto wake wanao utajiri wao binafsi; hatima ya binadamu inaamriwa Mbinguni.” Watu wengi ambao hawaelewi ukweli, baada ya kupitia mabadiliko, mahangaiko, na ugumu wote wa ulimwengu huu, watatoa muhtasari wa utambuzi wao wa maisha ya binadamu kwa maneno matatu: “Hiyo ndiyo hatima!” Ingawaje kauli hii inatoa muhtasari wa hitimisho ya watu wa ulimwengu na utambuzi kuhusu hatima ya binadamu, ingawaje inaelezea kutoweza kusaidika kwa binadamu na inaweza kusemekana kwamba inapenyeza na ni sahihi, ni kilio cha mbali kutoka kwa ufahamu wa ukuu wa Muumba, na si kibadala cha maarifa ya mamlaka ya Muumba.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp