Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 129

Kifo: Awamu ya Sita

Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa. Kusikia kwa mtu kunaanza kufifia, meno yake kulegea na kuanza kujiangukia, mwitikio wa mtu unaanza kuchelewachelewa, kutembea kunakuwa ni kwa kujikokota…. Wakati huu mtu ameaga kwaheri kabisa miaka yake ya nguvu ya ujana wake na kuingia katika maisha yake ya kwaheri: umri wa uzee. Kisha, mtu atakabiliana na kifo, awamu ya mwisho ya maisha ya binadamu.

1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu

Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa na maisha ya awali ya mtu, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu ya maisha, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba amepangilia mseto maalum wa hali mbalimbali za kuzaliwa kwa mtu, ni wazi na dhahiri shahiri kwamba amepangilia pia mseto wa hali zisizobadilika kwa minajili ya kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu ambacho hakitarajiwi, na si kuzaliwa, si kufa vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kama vile tu mengi yanaweza kuzungumzwa kuhusu kuzaliwa kwa mtu, hata kifo cha kila mtu kitafanyika katika mseto tofauti katika hali maalum, hivyo basi urefu wa maisha tofauti miongoni mwa watu na njia tofauti pamoja na nyakati tofauti zinaandama vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi wanafarakana na dunia kutokana na sababu zisizokuwa za kawaida, wengine kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia hewani, wengine wakafia chini ya nchi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. … Kila mtu hutaka kuzaliwa kwa heshima, maisha mazuri, na kifo kitukufu, hakuna mtu anayeweza kuendeleza hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Binadamu anaweza kufanya aina zote za mipango ya siku zote za usoni, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawaje watu hufanya kila wawezalo kuepuka na kuzuia kuja kwa kifo chao, ilhali, bila wao kujua, kifo huwa kinakaribia polepole. Hakuna anayejua ni lini atakapofarakana na dunia au ni vipi atakavyofanya hivyo, isitoshe hata pale hayo yote yatakapofanyikia. Bila shaka, si binadamu wanaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa kimaumbile, lakini ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa kimaumbile, lakini athari ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.

2. Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo

Wakati mtu anapoingia kwenye umri wa uzee, changamoto anazokabiliana nazo si kutosheleza mahitaji ya familia au kuanzisha maono makubwa katika maisha yake, lakini namna ya kuyaaga maisha yake, namna ya kukutana na mwisho wa maisha yake, namna ya kuweka kikomo kwenye mwisho wa uwepo wake binafsi. Ingawaje juujuu inaonekana kwamba watu hutilia makini kidogo kwa kifo, hakuna anayeweza kuepuka kuchunguza suala hili, kwani hakuna anayejua ikiwa ulimwengu mwingine uko kule upande mwingine wa kifo, ulimwengu ambao binadamu hawawezi kung’amua au kuhisi, ulimwengu wasiojua chochote kuuhusu. Hali hii huwafanya watu kuwa na wasiwasi kukabiliana na kifo moja kwa moja, wasiwasi wa kukabiliana nacho kama inavyostahili, na badala yake wanafanya kadri ya uwezo wao kuepuka mada hii. Na kwa hivyo mada hii humfanya kila mmoja kutishika kuhusu kifo, huongezea uzito kwenye fumbo hili kuhusiana na hoja hii isiyokwepeka ya maisha, huweka kivuli kisichoisha juu ya moyo wa kila mmoja.

Wakati mtu anapohisi mwili wake unaanza kudhoofika, wakati mtu anapohisi kwamba kifo chake chakaribia, mtu huhisi tishio, woga usioelezeka. Woga wa kifo humfanya mtu kuhisi kuwa mpweke zaidi na asiyejiweza, na kwa wakati huu mtu hujiuliza: Nilitoka wapi? Ninaenda wapi? Je, hivi ndivyo nitakavyokufa, huku maisha yangu yakinipita kwa haraka hivi? Je, huu ndio wakati unaoadhimisha mwisho wa maisha yangu? Ni nini, hatimaye, maana ya maisha? Maisha yana thamani gani, kwa kweli? Je, yanahusu umaarufu na utajiri? Je, yanahusu kulea familia? … Haijalishi kama mtu amewahi kufikiria maswali haya mahususi, haijalishi ni vipi mtu ana woga wa kifo, katika kina cha moyo wa kila mmoja siku zote kuna tamanio la kutaka kuchunguza zaidi mafumbo, hisia zisizoeleweka kuhusu maisha, pamoja na haya yote, ni uhusiano wa karibu na ulimwengu wenyewe, na kutotaka kuuacha. Pengine hakuna anayeweza kufafanua zaidi ni nini ambacho binadamu huogopa, ni nini ambacho binadamu hutaka kuchunguza zaidi, na nini kile ambacho ana uhusiano wa karibu nacho na kinachomfanya kutotaka kuondoka au kukiacha nyuma …

Kwa sababu wanaogopa kifo, watu huwa na wasiwasi mno; kwa vile wanaogopa kifo, vipo vitu vingi ambavyo hawawezi kuachilia. Wakati wako karibu kufa, baadhi ya watu huhangaika kuhusu hiki au kile; wanakuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao, wapendwa wao, utajiri wao, ni kana kwamba kwa kuwa na wasiwasi hivyo wanaweza kuondoa mateso na hofu ambayo kifo huleta, ni kana kwamba kwa kuendeleza aina fulani ya urafiki wa karibu na wale wanaoishi wanaweza kukwepa ile hali ya kutoweza kujisaidia na upweke unaoandamana na kifo. Katika kina cha moyo wa binadamu kunao woga usiokamilika, woga wa kuachwa na wapendwa, woga wa kutowahi kutuliza macho yako kwenye mbingu za samawati, woga wa kutowahi tena kuangalia ulimwengu huu yakinifu. Nafsi pweke, iliyozoeana na wapendwa wake, husita kuachilia mshiko wa maisha na kuondoka, ikiwa pekee, kuelekea kwenye ulimwengu usiojulikana, usiozoeleka.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp