Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 141

Mungu alimuumba mwanadamu na tangu hapo kamwe Ameongoza maisha ya binadamu. Iwe kwa kuwapa wanadamu baraka, kuwapa sheria na amri Zake, ama kuweka masharti kanuni mbalimbali za maisha, mnajua lengo analonuia Mungu kwa kufanya mambo haya ni nini? Kwanza, mnaweza kusema kwa uhakika kwamba yote anayofanya Mungu ni kwa wema wa binadamu? (Ndiyo, tunaweza.) Mnaweza kufikiria kwamba sentensi hii kwa kulinganishwa ni pana na tupu, lakini kuzungumza hasa, kila kitu anachofanya Mungu ni cha kumwongoza na kumwelekeza mwanadamu kuishi maisha ya kawaida. Iwe ili mwanadamu ahifadhi kanuni Zake ama ahifadhi sheria Zake, lengo la Mungu ni kwa mwanadamu kutomwabudu Shetani, kutodhuriwa na Shetani; hii ndiyo ya msingi sana, na hii ndiyo ilifanywa mwanzoni. Mwanzoni kabisa, wakati mwanadamu hakuelewa mapenzi ya Mungu, Alichukua baadhi ya sheria na kanuni rahisi na kuweka kauli zilizoshughulikia masuala yote yanayoweza kufikiriwa. Kauli hizi ni rahisi sana, lakini ndani yake kuna mapenzi ya Mungu. Mungu anamthamini, Anamtunza na kwa hakika Anampenda mwanadamu. Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo tunaweza kusema kwamba moyo Wake ni mtakatifu? Tunaweza kusema kwamba moyo wake ni safi? (Ndiyo.) Je, Mungu anazo nia zilizofichwa? (La.) Kwa hivyo hili lengo Lake ni sahihi na halisi? (Ndiyo.) Licha ya kauli alizoweka Mungu, katika kazi Yake yote yana athari halisi kwa mwanadamu, na zinaongoza njia. Kwa hivyo kuna fikira zozote za kibinafsi kwa akili ya Mungu? Je, Mungu anayo malengo zaidi kuhusiana na mwanadamu, ama Anataka kumtumia mwanadamu kwa jinsi fulani? (La.) Sivyo hata kidogo. Mungu anafanya Asemavyo, na pia Anafikiria namna hii kwa moyo Wake. Hakuna mchanganyiko wa madhumuni, hakuna fikira za kibinafsi. Hajifanyii chochote, lakini Anamfanyia mwanadamu kila kitu kabisa, bila malengo ya kibinafsi. Ingawa Ana mipango na nia kwa mwanadamu, Hajifanyii chochote. Kila kitu Anachofanya kinafanyiwa mwanadamu tu, kumlinda mwanadamu, kumhifadhi mwanadamu dhidi ya kupotezwa. Hivyo si moyo huu ni wenye thamani? (Ndiyo.) Unaweza kuona dokezo hata kidogo zaidi la huu moyo wenye thamani kwa Shetani? Mnaweza kuliona? (La.) Hamuwezi kuliona dokezo moja la moyo huu kwa Shetani. Kila kitu anachofanya Mungu kinafichuliwa kiasili. Kwa kuangalia njia Mungu anafanya kazi, Anafanyaje kazi? Je, Mungu anazichukua sheria hizi na maneno Yake na kuyafunga pamoja kwa kukaza katika kichwa cha kila mtu kama fingo la pete ya dhahabu, Akizilazimisha kwa kila mtu? Je, Anafanya kazi namna hii? (La.) Kwa hivyo Mungu anafanya kazi Yake namna gani? (Anatuongoza.) (Anashauri na kutia moyo.) Kuna kipengele cha pili. Vingine zaidi? Je, Anatishia? Je, Anawazungumzia kwa njia inayochanganya? (La.) Wakati huelewi ukweli, Mungu hukuongoza vipi? (Yeye huangaza mwangaza.) Anaangaza mwangaza kwako, akikwambia wazi kwamba haya hayaambatani na ukweli, na kile unachofaa kufanya. Kutoka kwa njia hizi ambazo Mungu anafanya kazi, unahisi kwamba una uhusiano wa aina gani na Mungu? Zinakufanya uhisi kwamba Mungu yuko mbali na ufahamu wako? (La.) Hivyo zinakufanya uhisi vipi? Mungu yuko hasa karibu na wewe, hakuna umbali kati yenu. Wakati Mungu anakuongoza, Anapokukimu, Anapokusaidia na kukutunza, unahisi urafiki wa Mungu, kuheshimika Kwake, unahisi jinsi Anavyopendeza, jinsi Alivyo mwema. Lakini wakati Mungu anaposhutumu upotovu wako, ama Anapokuhukumu na kukufundisha nidhamu kwa sababu ya kuasi dhidi Yake, Mungu anatumia njia gani? Anakushutumu kwa kutumia maneno? Anakufundisha nidhamu kupitia mazingira yako na kupitia watu, masuala na mambo? (Ndiyo.) Nidhamu hii imefika kiwango kipi? (Kwa kiwango ambacho mwanadamu anaweza kuvumilia.) Kiwango Chake cha nidhamu kinafikia mahali sawa ambapo Shetani anamdhuru mwanadamu? (La.) Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, upendo, laini na ya kujali, kwa njia hasa iliyopimwa na ni sahihi. Njia Yake haikufanyi kuhisi hisia kali kama vile, “Mungu lazima aniwache nifanye hivi” ama “Lazima Mungu aniache nifanye vile.” Mungu kamwe hakupi mawazo ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika. Sivyo? Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi kwamba Mungu ni mtakatifu na asiyekosewa? (Ndiyo.) Unahisi ukiwa mbali na Mungu nyakati hizi? Unahisi kutishiwa na Mungu? (La.) La, badala yake, unahisi heshima inayomcha Mungu. Je, watu wanahisi haya mambo yote kwa sababu tu ya kazi ya Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo wangekuwa na hisia hizi iwapo Shetani angefanya kazi kwa mwanadamu? (La.) Mungu anatumia maneno Yake, ukweli Wake na uhai Wake kuendelea bila kusita kumtolea mwanadamu, kumtunza mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati mwanadamu anahisi huzuni, Mungu kwa hakika hazungumzi kwa ukali, akisema, “Usihisi huzuni. Mbona unahisi huzuni? Kwa nini uwe mnyonge? Kuna nini ya kuwa mnyonge kuihusu? Wewe ni mnyonge sana, na daima una huzuni. Kuna haja gani ya kuishi? Kufa tu!” Je, Mungu anafanya kazi hivi? (La.) Je, Mungu ana mamlaka ya kutenda namna hii? (Ndiyo.) Lakini Mungu anatenda namna hii? (La.) Mungu hatendi hivi kwa sababu ya kiini Chake, kiini cha utakatifu wa Mungu. Upendo Wake kwa mwanadamu, kuthamini na utunzaji Wake wa mwanadamu haviwezi kuelezwa wazi kwa sentensi moja au mbili. Si kitu kinacholetwa na kujisifu kwa binadamu lakini ni kitu kinacholetwa kwa vitendo halisi; ni ufunuo wa kiini cha Mungu. Je, hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi zinaweza kumruhusu mwanadamu kuona utakatifu wa Mungu? Kwa hizi njia zote ambazo Mungu anafanya kazi, zikiwemo nia nzuri za Mungu, zikiwemo athari ambazo Mungu anataka kutimiza kwa mwanadamu, zikiwemo njia mbalimbali Mungu anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu, aina ya kazi Anayofanya, kile Anachotaka mwanadamu kuelewa—umeona uovu ama ujanja wowote katika nia nzuri za Mungu? (La.) Hivyo, kwa kila kitu Mungu anafanya, kila kitu Mungu anasema, kila kitu anachofikiria katika moyo Wake, na pia kiini chote cha Mungu anachofichua—tunaweza kumwita Mungu mtakatifu? (Ndiyo.) Mwanadamu yeyote amewahi kuona utakatifu huu duniani, ama kwake mwenyewe? Mbali na Mungu, umewahi kuuona kwa mtu yeyote ama kwa Shetani? (La.) Kutoka kwa yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, tunaweza kumwita Mungu wa kipekee, Mungu mtakatifu Mwenyewe? (Ndiyo.) Yote ambayo Mungu anampa mwanadamu, yakiwemo maneno ya Mungu, njia tofauti ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu, kile ambacho Mungu anamwambia mwanadamu, kile ambacho Mungu anamkumbusha mwanadamu kuhusu, kile ambacho Anashauri na kutia moyo, vyote vimetoka kwa kiini kimoja: Vyote vimetoka kwa utakatifu wa Mungu. Iwapo hakungekuwa na Mungu mtakatifu kama huyu, hakuna mwanadamu ambaye angechukua nafasi Yake kufanya kazi Anayofanya. Iwapo Mungu angewachukua watu hawa na kuwakabidhi kabisa kwa Shetani, mmewahi kuzingatia mngekuwa katika hali ya aina gani leo? Nyinyi nyote mngekuwa mmeketi hapa? Kamili na wasioharibika? (La.) Kwa hivyo mngekuwa vipi? Pia mngesema: “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo”? Mngejitamba hivyo, kutokuwa na haya kabisa na kujigamba bila haya mbele ya Mungu, na kuenda dalji mkizungumza kwa njia kama hiyo? (Ndiyo.) Mngeweza kwa asilimia mia moja! Mngeweza kabisa! Mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu unawaruhusu kuona kwamba asili ya Shetani ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kiini chake ni tofauti kabisa na cha Mungu. Kiini kipi cha Shetani ni kinyume cha utakatifu wa Mungu? (Uovu wake.) Asili ya uovu ya Shetani ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Watu wengi zaidi hawatambui maonyesho haya ya Mungu na kiini hiki cha utakatifu wa Mungu ni kwa sababu wanamilikiwa na Shetani, ndani ya upotovu wa Shetani na ndani ya boma anamoishi Shetani. Hawajui utakatifu ni nini ama jinsi ya kufafanua utakatifu. Hata unapoona utakatifu wa Mungu, bado huwezi kuufafanua kuwa utakatifu wa Mungu kwa uhakika wowote. Hii ni tofauti katika maarifa ya mwanadamu ya utakatifu wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp