Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 145

Mat 4:5-7 Kisha Ibilisi akamchukua hadi katika mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Naye akamwambia, Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini: kwa kuwa imeandikwa, Atawaamuru malaika wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote. Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Hebu kwanza tuzungumze kuhusu kirai hiki cha Shetani. Alisema “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini,” na kisha akadondoa kutoka kwa maandiko, “Atawaamuru malaika wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote.” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, unaona chochote kwa kile Shetani amesema? (Kuna nia ovu hapo.) Shetani daima amekuwa mjaribu; haongei kwa njia inayoeleweka rahisi, huongea kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anamjaribu Mungu na pia mwanadamu: Anafikiri kwamba Mungu na mwanadamu wote hawajui, ni wajinga, na hawawezi kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona udanganyifu wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? (Ndiyo.) Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Mmesikia watu wakisema kitu kama hiki? (Ndiyo.) Ni jinsi gani unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? Unahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? (Ndiyo.) Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Mungu kamwe haongei namna hiyo. Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya ujinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu, sivyo? Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu.

Hivyo, jibu la Bwana kwa maneno ya Shetani lilikuwa lipi? (Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.) Kuna ukweli katika kirai hiki ambacho Bwana Yesu alisema? (Ndiyo.) Kuna ukweli kwa kirai hicho. Juujuu inaonekana kama amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi sana, lakini ni kimoja ambacho mwanadamu na Shetani wamekiuka mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hivyo, hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo.) Mbona? (Kwa sababu pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Watu mara nyingi humjaribu Mungu, lakini mbona watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? (Ndiyo.) Katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema kirai rahisi, ambacho kinawakilisha ukweli na ambacho watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akigombana na Shetani? Kulikuwa na chochote cha kukabiliana kwa kile Alisema kwa Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? (Ndiyo.) Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa, sivyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? (Bwana Yesu hakutaka kumkiri Shetani.) Kwa nini Hakutaka kumkiri Shetani? (Kwa sababu Shetani daima yuko hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, Shetani alifikiri kwamba, hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, bado angejaribu jambo hili tu. Hata kama angeadhibiwa, angeifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, angeifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? (Ndiyo.) Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, amemwona Mungu? Yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajaongea naye. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo mbona akuwe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? Huyu anaweza kuwa mtu mwenye asili ovu? Haijalishi ni mienendo gani inafanyika duniani, iwe ya kufurahisha, chakula, watu maarufu, watu wenye sura nzuri, hakuna yoyote haya yanayomsumbua, lakini kutajwa mara moja kwa neno “Mungu” na anakasirika; huu si mfano wa asili ovu? Huu unatumika kama ushahidi wa kuridhisha wa asili ovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Huu ni ukweli vipi? Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Huu si ukweli, haya bila shaka ni maneno ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa kwa mioyo yao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu daima yanatajwa kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na busara inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu na maneno haya sio tu ndoto isiyo na msingi, lakini bali yake yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na kuwaruhusu kutembea njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp