Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 154

Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuboreka kila siku,” kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unapopata maarifa zaidi, ndivyo utakavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, kwa wakati sawa wanaposoma maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na mawazo. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanatembea njia ya aina hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na mawazo yao. Hatua kwa hatua, watu bila kujua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani kufikiria kwa watu wakubwa ama maarufu. Wanajifunza pia jambo moja baada ya lingine kutoka kwa matendo ya wengine ambao watu wanachukulia kuwa mashujaa. Mnaweza kujua baadhi ya yale ambayo Shetani anatetea kwa mwanadamu katika matendo ya hawa mashujaa, ama kile anachotaka kuingiza kwa mwanadamu. Ni kipi ambacho Shetani anaingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya rafiki ya mtu ama kwa rafiki. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya Shetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana kuwapata watu, kuchukua chambo polepole. Kwa njia hii, katika mkondo wa kujifunza kwao, wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda thiolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua yalivyo na mambo haya, kila mmoja amepatana nayo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo kuhusu moja yao fulani. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapenda sehemu ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu amependa kwa dhati mojawapo, basi bila kujua anaendeleza mawazo: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, mawazo yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya mawazo na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Mbona Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi katika kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp