Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 184

Tukiangalia kwa mtazamo wa sheria zilizoamriwa na Mungu kwa ukuaji wa vitu vyote, yote hii si kwa ajili ya mwanadamu, haijalishi ni wa aina gani, anaishi chini ya uangalizi wa Mungu—je, wote hawaishi chini ya malezi Yake? Ikiwa sheria hizi zingeharibiwa au Mungu hakuanzisha aina hizi za sheria kwa ajili ya binadamu, majaliwa yao yangekuwa ni nini? Baada ya binadamu kupoteza mazingira yao ya msingi kwa ajili ya kuendelea kuishi, je, wangekuwa na chanzo chochote cha chakula? Inawezekana kwamba vyanzo vya chakula vingekuwa tatizo. Ikiwa watu wangepoteza vyanzo vyao vya chakula, yaani, ikiwa hawangeweza kupata kitu chochote cha kula, ni siku ngapi wangeweza kuvumilia? Pengine wasingeweza kuvumilia hata kwa mwezi mmoja, na kuendelea kuishi kwao kungekuwa ni tatizo. Kwa hiyo kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa ajili ya watu kuendelea kuishi, kwa ajili ya wao kuendelea kuwepo, kuongezeka, na ruzuku ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya miongoni mwa vitu vyote vinahusiana kwa karibu na haviwezi kutenganishwa na watu kuendelea kuishi. Ikiwa kuendelea kuishi kwa binadamu kulikuwa tatizo, je, usimamizi wa Mungu ungeweza kuendelea? Je, usimamizi wa Mungu bado ungekuwepo? Usimamizi wa Mungu unakwenda sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu wote ambao Anawalea, kwa hivyo haijalishi Mungu anaandaa kitu gani kwa ajili ya vitu vyote na kile Anachofanya kwa ajili ya binadamu, hii yote ndiyo lazima Kwake, na ni muhimu sana kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ikiwa sheria zote hizi ambazo Mungu aliziamua kwa ajili ya vitu vyote zingekuwa zimeachwa, ikiwa sheria hizi zingekuwa zimevunjwa au zimeharibiwa, vitu vyote visingeweza kuwepo, mazingira ya binadamu ya kuendelea kuwepo yasingekuwepo, na wala riziki zao za kila siku, na wala wao wenyewe. Kwa sababu hii, Usimamizi wa Mungu wa wokovu wa binadamu wala nao usingekuwepo pia.

Kila kitu ambacho tumejadili, kila kitu, kila kipengele kimeungana kikamilifu na kuendelea kuishi kwa kila mtu. Mnaweza kusema, “Unachokizungumzia ni kikubwa sana, hatuwezi kukiona,” na pengine kuna watu ambao wangeweza kusema “Unachokizungumzia hakinihusu.” Hata hivyo, usisahau kwamba unaishi kama sehemu tu ya vitu vyote; wewe ni mshirika wa vitu vyote ndani ya kanuni ya Mungu. Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Haijalishi wewe ni mbari gani au unaishi katika ardhi gani, iwe ni Magharibi au Mashariki—huwezi kujitenganisha na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu, na huwezi kujitenga na malezi na uangalizi wa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Ameyaanzisha kwa ajili ya binadamu. Haijalishi riziki yako ni nini, kile unachokitegemea kwa ajili ya kuishi, na kile unachokitegemea kudumisha uhai wako katika mwili, huwezi kujitenganisha na kanuni ya Mungu na usimamizi wake. Baadhi ya watu wanasema: “Mimi sio mkulima, sipandi mazao kwa ajili ya kuishi. Sitegemei mbingu ili nipate chakula changu, kwa hiyo naweza kusema kwamba siendelei kuishi katika mazingira ambayo aliyaanzisha Mungu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Aina hiyo ya mazingira haijanipatia kitu chochote.” Hii ni kweli? Unasema kwamba hupandi mazao kwa ajili ya kuishi, lakini huli nafaka? Huli nyama na mayai? Je, huli mbogamboga na matunda. Kila kitu unachokula, vitu hivi vyote unavyovitaka havitenganishwi na mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoanzishwa na Mungu kwa ajili ya binadamu. Na chanzo cha kila kitu ambacho binadamu anahitaji hakiwezi kutenganishwa na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, aina hizo za mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Maji unayokunywa, nguo unazovaa, na vitu vyote unavyotumia—ni kitu gani kati ya hivi ambacho hakipatikani kutoka katika vitu hivi vyote? Baadhi ya watu husema: “Kuna baadhi ya vitu ambavyo havipatikani kutoka katika vitu vyote hivi. Unaona, plastiki haitokani na vitu vyote hivi. Ni kitu cha kemikali, kitu kilichotengenezwa na mwanadamu.” Hii ni sahihi? Plastiki imetengenezwa na mwanadamu, ni kitu cha kemikali, lakini vijenzi asilia vya plastiki vilitoka wapi? Vijenzi asilia vilipatikana kutoka katika vitu ambavyo kwa asili vilitengenezwa na Mungu. Vitu ambavyo unavifurahia, ambavyo unaona, kila kitu ambacho unatumia, vyote vinapatikana kutoka katika vitu vyote ambavyo vilitengenezwa na Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, haijalishi ni mbari gani, haijalishi ni riziki gani, au ni katika aina gani ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo watu wanaishi, hawawezi kujitenganisha na uangalizi wa Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp