Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 192

Ikija kwa wasioamini, je, kanuni iongozayo matendo ya Mungu ni ile ya kutuza mazuri na kuadhibu mabaya? Kuna upekee wowote? (La.) Je, mnaona kwamba kuna kanuni katika matendo ya Mungu? (Ndiyo.) Wasioamini kwa hakika hawamwamini Mungu, hawatii mipango ya Mungu, na hawafahamu ukuu wa Mungu, na hawamtambui Mungu hata kidogo. Zito zaidi, wanamkufuru Mungu, na kumlaani, na ni mahasimu wa wale wanaomwamini Mungu. Japo watu hawa wana mwelekeo huo kwa Mungu, bado uongozi wa Mungu kwao hauachani na kanuni Zake; Anawaongoza kwa njia ya utaratibu kulingana na kanuni Zake na tabia Yake. Je, Mungu anauchukuliaje uhasama wao? Kama ujinga! Na kwa hiyo Amewasababisha hawa watu—wengi wa wasioamini—wakati mmoja kuwahi kupata mwili kama wanyama. Basi wasioamini ni nini machoni mwa Mungu? (Mifugo.) Machoni pa Mungu, ni wa hii sampuli, wao ni mifugo. Mungu anaongoza mifugo, na Anaongoza wanadamu, na Ana kanuni sawa kwa hii aina ya mtu. Hata katika utawala wa Mungu kwa watu hawa na matendo Yake kwao, bado kunaweza kuonekana tabia ya Mungu na sheria za utawala Wake juu ya vitu vyote. Hivyo basi, unaona mamlaka ya Mungu katika kanuni ambazo kwazo Anawaongoza wasioamini ambao Nimezungumzia hivi punde? Je, mnaona tabia ya haki ya Mungu? (Tunaona.) Mnaona ukuu wa Mungu, na mnaona tabia Yake. Yaani, haijalishi Anashughulikia kitu gani kati ya vitu vyote Anavyoshughulikia, Mungu anatenda kulingana na kanuni na tabia Yake. Hiki ndicho kiini cha Mungu. Hangeweza kujitenga kiholela na amri au sheria za mbinguni Alizozipanga kwa sababu Anamwona mtu wa aina hii kama mfugo. Mungu anatenda kulingana na kanuni, bila kuzivuruga hata kidogo, matendo Yake hayaathiriwi na jambo lolote, na haijalishi Anafanya nini, yote ni kulingana na kanuni Zake mwenyewe. Hili ni kwa sababu Mungu ana kiini cha Mungu Mwenyewe, ambacho ni kipengele cha kiini Chake ambacho hakimo kwenye kiumbe yeyote. Mungu ni Mwangalifu na Anawajibika katika kushughulikia Kwake, njia Zake, usimamizi, uongozi, na utawala wa kila chombo, mtu, na kiumbe hai miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba, na Hajawahi kuwa mzembe katika hili. Yeye ni mwenye neema na mkarimu kwa wale walio wazuri; Kwa wale waovu, Anawapa adhabu bila huruma; na kwa viumbe hai mbalimbali, Anafanya mipango ifaayo kwa wakati na kwa njia ya kawaida kulingana na mahitaji mbalimbali ya ulimwengu wa wanadamu katika nyakati mbalimbali, kiasi kwamba hawa viumbe hai mbalimbali wanapata miili kulingana na nafasi wanayochukua kwa njia ya utaratibu, na kuhama kati ya ulimwengu yakinifu na ulimwengu wa kiroho kwa njia ya utaratibu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp