Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 197

Inapokuja katika ulimwengu wa kiroho, kama viumbe mbalimbali waliomo watafanya kitu kibaya, kama hawafanyi kazi yao inavyostahili, Mungu pia ana sheria za peponi na amri zifaazo kuwashughulikia—hili halipingwi. Basi, katika maelfu kadhaa ya miaka ya kazi ya usimamizi ya Mungu, wasimamizi wengine ambao walifanya maovu wameangamizwa, wengine, leo, wangali wanazuiliwa na kuadhibiwa. Hili ndilo linafaa kukabiliwa na kila kiumbe aliye katika ulimwengu wa kiroho. Kama watafanya kitu kibaya au kutenda maovu, wanaadhibiwa—ambayo ni sawa na jinsi Mungu anatenda kwa wateule Wake na watendaji huduma. Na kwa hivyo, iwe ni katika ulimwengu wa kiroho au ulimwengu yakinifu, kanuni ambazo Mungu hutekeleza matendo hazibadiliki. Bila kujali kama unaweza kuona matendo ya Mungu au la, kanuni zao hazibadiliki. Daima, Mungu amekuwa na kanuni sawa kwa jinsi Anavyotekeleza matendo kwa vitu vyote na kuvishughulikia vitu vyote. Hili halibadiliki. Mungu atakuwa mkarimu kwa wale walio miongoni mwa wasioamini ambao angalau wanaishi ipasavyo, na kuwapa nafasi wale walio katika kila dini ambao wana tabia nzuri na hawatendi maovu, kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao katika vitu vyote vinavyosimamiwa na Mungu, na kufanya kile ambacho wanafaa kufanya. Vivyo hivyo, kati ya wale wanaomfuata Mungu, kati ya wateule Wake, Mungu habagui mtu yeyote kulingana na kanuni Zake hizi. Ni mwema kwa kila mtu anayeweza kumfuata kwa dhati, na kupenda kila mtu anayemfuata kwa dhati. Ni kwamba tu kwa aina hizi mbalimbali za watu—wasioamini, aina tofauti za watu wenye imani, na wateule wa Mungu—anachowazawadia wao ni tofauti. Chukulia wasioamini: hata kama hawamwamini Mungu, na Mungu huwaona kama mifugo, miongoni mwa kila kitu kila mmoja wao ana chakula, mahali pao wenyewe, na mzunguko wa kawaida wa uhai na mauti. Wanaotenda maovu wanaadhibiwa, na wanaofanya mazuri wanabarikiwa na hupokea wema wa Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo? Kwa watu wenye imani, kama wanaweza kutii hasa maadili ya kidini, kizazi baada ya kizazi, basi baada ya hivi vizazi vyote Mungu hatimaye atatoa uamuzi Wake kwao. Vivyohivyo, kwa wewe leo, awe mmoja wa wateule wa Mungu au mtendaji huduma, Mungu vilevile atakuwazisha na kuamua mwisho wako kulingana na kanuni na amri za utawala ambazo Ameziweka. Miongoni mwa aina hizi kadhaa za watu—aina tofauti za watu wa imani, walio katika dini tofauti—je, Mungu amewapa nafasi ya kuishi? Uko wapi Uyahudi? Mungu ameingilia katika imani yao? Hajaingilia, siyo? Na vipi kuhusu Ukristo? Hajaingilia pia? Anawaruhusu kufuata mipangilio yao wenyewe, na Hasemi nao, au kuwapa nuru yoyote, na, zaidi ya hayo, Hawafichulii kitu chochote: “Kama unafikiria ni sahihi, basi amini hivyo!” Wakatoliki wanamwamini Maria, na kwamba ni kupitia kwa Maria ambapo habari zilimfikia Bwana Yesu; hiyo ndiyo aina yao ya imani. Na Mungu amewahi kurekebisha imani yao? Mungu huwapa uhuru, Mungu hawasikizi, na huwapa sehemu fulani ambapo wataishi. Na kwa Waisilamu na wafuasi wa Budha, je, Yuko hivyo pia? Ameweka mipaka kwa ajili yao, pia, na kuwaruhusu kuwa na mahali pao wenyewe pa kuishi, bila ya kuingilia imani zao. Yote yamepangwa vizuri. Na unaona nini katika haya yote? Kwamba Mungu ana mamlaka, lakini hatumii vibaya mamlaka Yake. Mungu hupanga vitu vyote katika mpangilio taratibu, na ni mwenye utaratibu, na katika hili busara na kudura Zake vinadhihirika.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp