Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 156

Kile kinachohusisha maono kimsingi hurejelea kazi ya Mungu Mwenyewe, na kile kinachohusisha vitendo ni sharti kifanywe na mwanadamu, na hakina uhusiano na Mungu. Kazi ya Mungu hukamilishwa na Mungu Mwenyewe, na vitendo vya mwanadamu hufikiwa na mwanadamu mwenyewe. Kile ambacho ni sharti kifanywe na Mungu Mwenyewe hakihitajiki kufanywa na mwanadamu, na kile kitendwacho na mwanadamu hakihusiani na Mungu. Kazi ya Mungu ni huduma Yake Mwenyewe na haina uhusiano na mwanadamu. Hii kazi haihitaji kufanywa na mwanadamu, na hata zaidi, mwanadamu hatakuwa na uwezo wa kufanya kazi ambayo ni ya kufanywa na Mungu. Kile ambacho kinafaa kutendwa na mwanadamu ni sharti kitimizwe na mwanadamu, iwe ni kujitoa kafara au kuwasilishwa kwake kwa Shetani ili kushuhudia—haya ni lazima yatimizwe na mwanadamu. Mungu Mwenyewe anatimiza kazi Yake yote, na kile ambacho ni wajibu wa mwanadamu, mwanadamu hufunuliwa na kazi iliyobaki huachiwa mwanadamu. Mungu hafanyi kazi ya ziada. Anafanya ile kazi iliyo katika huduma Yake na kumuonyesha mwanadamu na kumfunulia njia tu bali hampambanulii njia; hili lazima lieleweke kwa mwanadamu. Kuweka ukweli katika vitendo kunamaanisha kuweka neno la Mungu katika vitendo, na haya yote ni wajibu wa mwanadamu, ni kile kinachofaa kufanywa na mwanadamu, na wala halihusiani na Mungu. Iwapo mwanadamu atataka Mungu apitie masaibu na utakaso katika ukweli sawa na mwanadamu, basi mwanadamu atakuwa hatii. Kazi ya Mungu ni kuendeleza huduma Yake, na wajibu wa mwanadamu ni kutii uongozi wote wa Mungu, bila pingamizi yoyote. Kinachotakiwa kufikiwa na mwanadamu anawajibika kutimiza, bila kujali ni namna gani Mungu hufanya kazi au kuishi. Ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayeweza kumwekea mwanadamu matakwa, ambayo ni kusema, ni Mungu Mwenyewe tu ndiye anayestahili kumwekea mwanadamu matakwa. Mwanadamu hastahili kuwa na jingine, hastahili kufanya chochote ila tu kutii kikamilifu na kutenda; hii ndiyo busara ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo. Punde kazi ifaayo kufanywa na Mungu Mwenyewe itakapokamilika, mwanadamu anatakiwa kuipitia, hatua kwa hatua. Iwapo mwishowe, baada ya usimamizi wote wa Mungu kukamilika, mwanadamu atakuwa hajafanya anachotakiwa na Mungu kufanya, basi mwanadamu anafaa aadhibiwe. Ikiwa mwanadamu hatimizi matakwa ya Mungu, basi hili ni kwa sababu ya uasi wa mwanadamu; haimaanishi kuwa Mungu hajakuwa makini vya kutosha katika kazi Yake. Wale wote wasioweka neno la Mungu katika vitendo, ambao hawatimizi matakwa ya Mungu na wale wote wasiokuwa na uaminifu na kutimiza wajibu wao—wataadhibiwa wote. Leo hii mnachohitajika kufikia si madai ya ziada, ila ni wajibu wa mwanadamu, na kile kinachofaa kufanywa na kila mtu. Kama hamuwezi hata kufanya wajibu wenu, au kuufanya vizuri, hamuoni mnajiletea masaibu nyinyi wenyewe? Hamwuoni mnajitakia kifo? Mtatarajiaje maisha ya baadaye na matarajio? Kazi ya Mungu ni kwa ajili ya wanadamu, na ushirika wa mwanadamu ni kwa minajili ya usimamizi wa Mungu. Baada ya Mungu kufanya yale yote Anayopaswa kufanya, mwanadamu anapaswa kufanya vitendo bila kukoma, na kushirikiana na Mungu. Mwanadamu hapaswi kulegeza kamba katika kazi ya Mungu, lazima aonyeshe uaminifu na asijitie katika mawazo mengi au kukaa akisubiri kifo bila kufanya kitu. Mungu Mwenyewe anaweza kujitolea kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asiweze kuwa mwaminifu kwa Mungu? Mawazo na moyo wa Mungu vipo kwa mwanadamu, basi ni kwa nini mwanadamu asijitolee katika ushirika? Mungu huwafanyia wanadamu kazi, basi ni kwa nini mwanadamu asifanye wajibu wake kwa minajili ya usimamizi wa Mungu? Kazi ya Mungu imefika umbali huu, bado mnaona ila hutendi, mnasikia ila hamsogei. Je, si watu kama hawa wanafaa kuangamizwa kabisa? Tayari Mungu amejitolea kikamilifu kwa ajili ya mwanadamu, basi ni kwa nini siku hizi mwanadamu hafanyi wajibu wake kwa dhati? Kwa Mungu, kazi Yake ni ya kipaumbele Kwake, na kazi ya usimamizi Wake ni ya umuhimu wa hali ya juu. Kwa mwanadamu, kuweka maneno ya Mungu katika vitendo na kutimiza mahitaji ya Mungu ndiyo kipaumbele kwake. Ni lazima nyote myafahamu haya. Maneno mliyoambiwa yamefika kiini halisi cha nafsi yenu, na kazi ya Mungu imefika katika maeneo ambayo hayakuwa yamefikiwa awali. Watu wengi bado hawafahamu ukweli na uongo wa njia hii; bado wanasubiri na kutazama na hawafanyi wajibu wao. Badala yake huchunguza kila neno na tendo la Mungu, wanalenga juu ya Anachokula na Anachokivaa na mawazo yao huwa hata ya kuhuzunisha zaidi. Si watu wa aina hii wanafanya msukosuko bure? Hawa wanawezaje kuwa watu wamtafutao Mungu? Wanawezaje kuwa watu wa kumnyenyekea Mungu kwa kudhamiria? Wanasahau uaminifu na wajibu wao na badala yake kujishughulisha na mahali alipo Mungu. Wanaghadhabisha! Ikiwa mwanadamu amefahamu yale yote anayopaswa kufahamu na kuweka katika vitendo yale yote anayopaswa, basi Mungu atampa mwanadamu baraka Zake, kwa sababu kile ambacho Yeye huhitaji kutoka kwa mwanadamu ni wajibu wa mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anastahili kufanya. Ikiwa mwanadamu hawezi kufahamu yale yote anayopaswa kufahamu na hawezi kutia katika vitendo yale anayopasa kuweka katika vitendo, basi mwanadamu ataadhibiwa. Wasioshirikiana na Mungu wana uhasama Naye, wasioikubali kazi mpya wanaipinga, hata kama watu kama hao hawafanyi chochote ambacho ni cha pingamizi dhahiri. Wale wote wasioweka ukweli unaohitajika na Mungu katika vitendo ni watu wanaopinga kwa makusudi na ni waasi wa maneno ya Mungu hata kama watu kama hawa hutilia maanani maalum kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wasiotii maneno ya Mungu na kumnyenyekea Mungu ni waasi, na wapinzani wa Mungu. Watu wasiofanya wajibu wao ni wale wasioshirikiana na Mungu, na watu wasioshirikiana na Mungu ni wale wasioikubali kazi ya Roho Mtakatifu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp