Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 158

Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikishwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale walioikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na vibaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee huduma na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda wakaadhibiwa. Bila kujali ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na kuyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. Watu walio kwenye mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya, na kwa sababu wameikubali kazi mpya, wanafaa kuwa na ushirika na Mungu na hawafai kuwa kama waasi wasiofanya wajibu wao. Hili ndilo sharti pekee la Mungu kwa mwanadamu. Sio hivyo na watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na adhabu na lawama ya Roho Mtakatifu haitumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi katika mwili, wanaishi katika mitazamo yao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu wala sio ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu wanajinyima uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Mengi ya maneno na matendo yao yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini tu na wala si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kitu cha pekee kinachowaleta pamoja ni dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mikutano ya wote walio miongoni mwao haiwezi kuitwa kanisa bali mkutano mkubwa wa watu wa dini. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinanuka dini, wanachodhihirisha katika maisha yao kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, na zaidi hawajahitimu kupokea adhabu au kupata nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyokuwa na uhai, na funza wasiokuwa na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu na hata zaidi, hawaifahamu kazi ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachoambatana na usimamizi wa Mungu, wala hakiwezi kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajika. Chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu hakihusiani na kazi mpya ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana adhabu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wametokwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui kwake kwa makusudi, na kumkimbia Mungu. Kutoshirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, bila kutaja kutoroka makusudi kwa watu hawa kutoka kwa Mungu. Basi, je, hawatapokea malipo wanayostahili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp