Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu | Dondoo 175

Uzoefu wa aina tofauti za watu unawakilisha vitu vilivyomo ndani yao. Wale wote ambao hawana uzoefu wa kiroho hawawezi kuzungumza juu ya maarifa ya ukweli, maarifa sahihi kuhusu aina mbalimbali za masuala ya kiroho. Kile ambacho mtu anakidhihirisha ndivyo alivyo ndani—hii ni hakika. Ikiwa mtu anatamani kuwa na maarifa ya masuala ya kiroho na ukweli, anapaswa kuwa na uzoefu halisi. Ikiwa huwezi kuzungumza kwa usahihi juu ya masuala ya kawaida yanayohusiana na maisha ya mwanadamu, basi utawezaje kuzungumzia masuala ya kiroho? Wale wanaoweza kuliongoza kanisa, kurutubisha maisha ya watu, na kuwa mtume kwa watu, wanapaswa kuwa na uzoefu halisi, uelewa sahihi wa masuala ya kiroho, kuukubali kuliko sahihi na kuwa na uzoefu wa ukweli. Watu wa namna hiyo tu ndio waliofuzu kuwa watenda kazi au mitume wanaoyaongoza makanisa. Vinginevyo, wanaweza kuwa wafuasi kama wadogo na hawawezi kuongoza, wala kuwa mtume mwenye uwezo wa kuwapatia watu uhai. Hii ni kwa sababu kazi ya mitume siyo kukimbia au kupigana; ni kutoa huduma ya maisha na kuongoza mabadiliko katika tabia ya mwanadamu. Ni kazi ambayo inafanywa na wale ambao wameagizwa kubeba majukumu mazito na sio kitu ambacho kila mtu anaweza kukifanya. Aina hii ya kazi inaweza tu kufanywa na wale ambao wana maisha ya uwepo, yaani, wale ambao wana uzoefu wa ukweli. Haiwezi kufanywa na kila mtu ambaye anaweza kukata tamaa, anaweza kukimbia au yupo tayari kutumia pesa; watu ambao hawana uzoefu wa ukweli, wale ambao hawajawahi kupogolewa au kuhukumiwa, hawawezi kufanya aina hii ya kazi. Watu ambao hawana uzoefu, yaani, watu wasio na ukweli, hawawezi kuona ukweli kwa uwazi kwa kuwa wao wenyewe hawako katika hali hii. Hivyo, mtu wa aina hii si kwamba anaweza tu kufanya kazi ya kuongoza bali atakuwa mtu wa kuondolewa ikiwa hatakuwa na ukweli kwa muda mrefu. Kuona unakokuzungumzia kunaweza kuthibitisha ugumu ulioupitia maishani, katika suala ambalo umefanyiwa kuadibu na katika jambo ambalo umehukumiwa kwalo. Hii pia ni kweli katika majaribu: Vitu ambavyo mtu anasafishwa kwavyo, vitu ambavyo kwavyo mtu yupo mdhaifu, hivi ni vitu ambavyo mtu ana uzoefu navyo, vitu ambavyo mtu anaelewa njia zake. Kwa mfano, ikiwa mtu amekatishwa tamaa katika ndoa, muda mwingi atakuwa anafanya ushirika, “Asante Mungu, Mungu asifiwe, ni lazima nitimize matakwa ya Mungu, na kuyatoa maisha yangu yote, kuikabidhi ndoa yangu kikamilifu katika mikono ya Mungu. Niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa Mungu.” Kupitia ushirika, kila kitu ndani ya mwanadamu, kile alicho, kinaweza kuwakilishwa. Mwendo wa hotuba ya mtu, kama anazungumza kwa sauti kubwa au kwa sauti ya chini, masuala kama hayo ambayo si masuala ya uzoefu hayawezi kuwakilisha kile alichonacho na kile alicho. Yanaweza kueleza tu iwapo tabia yake ni nzuri au mbaya, au kama asili yake ni nzuri au mbaya lakini haiwezi kulinganishwa na kama ana uzoefu. Uwezo wa mtu kujidhihirisha anapozungumza, ama ujuzi au kasi ya kuzungumza, ni suala tu la mazoezi na haliwezi kuchukua nafasi ya uzoefu wake. Unapozungumza juu ya uzoefu wako binafsi, unafanya ushirika wa kile ambacho unakipatia umuhimu na vitu vyote ndani yako. Usemi Wangu unawakilisha asili Yangu, lakini kile Ninachokisema kiko nje ya uwezo wa mwanadamu. Kile Nikisemacho sio kile ambacho mwanadamu anakipitia, na sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kukiona, pia si kitu ambacho mwanadamu anaweza kukigusa, lakini ndivyo Nilivyo. Baadhi ya watu wanakiri tu kwamba kile Ninachokifanyia ushirika ndicho kile Nimekipitia, lakini hawatambui kwamba ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho. Ni kweli, kile Ninachokisema ndicho kile Nimekipitia. Ni Mimi Ndiye Niliyefanya kazi ya usimamizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Nimeshuhudia kila kitu kuanzia mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu hadi leo; Nitashindwaje kukizungumzia? Linapokuja suala la asili ya mwanadamu, Nimeiona waziwazi, na Nimeiangalia toka zamani; sasa Nitashindwaje kuiongelea? Kwa kuwa nimeiona asili ya mwanadamu kwa uwazi, Nina sifa za kumrudi mwanadamu na kumhukumu, kwa sababu mwanadamu mzima ametoka Kwangu lakini ameharibiwa na Shetani. Kwa ukweli, Nimehitimu kutathmini kazi ambayo Nimeifanya. Ingawa kazi hii haijafanywa na mwili Wangu, ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho, na hiki ndicho Nilicho nacho na kile Nilicho. Kwa hivyo, Ninaweza kudhihirisha na kufanya kazi ambayo Napaswa kufanya. Kile ambacho mwanadamu anakisema ni kile alichokipitia. Ni kile ambacho wamekiona, kile ambacho akili zao zinaweza kukifikia, na kile ambacho milango yao ya fahamu inaweza kuhisi. Hicho ndicho wanachoweza kukifanyia ushirika. Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni udhihirishaji wa moja kwa moja wa Roho na kudhihirisha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado Anaonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na Anadhihirisha kazi ya Roho. Ingawa mwili hauwezi kuifikia, ni kazi ambayo tayari imefanywa na Roho. Baada ya kufanyika mwili, kupitia udhihirishaji wa mwili, Anawasaidia watu kujua asili ya Mungu na kuwafanya watu kuiona tabia ya Mungu na kazi ambayo ameifanya. Kazi ya mwanadamu inawawezesha watu kuelewa kwa uwazi kuhusu kile wanachopaswa kuingia kwacho na wanachopaswa kukielewa; kunahusisha kuwaongoza watu kupata uelewa na kuujua ukweli. Kazi ya mwanadamu ni kuwaendeleza watu; kazi ya Mungu ni kufungua njia mpya na kufungua enzi mpya kwa ajili ya wanadamu, na kuwafunulia watu kile ambacho hakijafahamika kwa watu wenye mwili wa kufa, akiwasaidia kuelewa tabia Yake. Kazi ya Mungu ni kuwaongoza wanadamu wote.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana